Gharama za Mafuta kuwa juu nchini.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Jamani wana Jf naomba msaada wenu.
Kuna jamaa yangu wa karibu ameniuliza hili swali nimeshindwa kumpa jibu.
Alipata bahati ya kutembelea nchi za jirani na Tanzania zikiwemo Rwanda, Burundi, Congo na Zambia.
Ameniambia huko amekuta bei ya mafuta yaani Petrol, disel na mafuta ya taa ipo chini kuliko huku kwetu wakati nchi hizo zinasafirisha mafuta hayo kwa kupitia bandari yetu ya Dar es salaam, hivyo inawacost gharama za usafirishaji lakini sisi ambao bandari hiyo ipo nchini kwetu lakini bado gharama zipo juu kuliko wao.
Tatizo hapo ni nini?
 
Tatizo ni kwamba Ridhiwani wa Kikwete nae ni mmbia kwenye hiyo biashara ya mafuta. Familia hiyo inatafuta hela za kwenda Ikulu wakale Bata . Halafu si unajua ufisadi wa Tanzania chini ya familia hiyo? I am serious.
 
Hii ni miradi ya watu waliokaa kiwiziwizi na ndio maana inakuwa hivyo.
 
Nafikiri tofauti kubwa ni kiwango cha kutoza kodi kwenye mafuta husababisha bei ya mafuta kuwa chini au juu.Kama kodi inayotozwa kwenye mafuta ni kubwa basi bei ya mafuta huwa juu.Vilevle,kama kodi inayotozwa kwenye mafuta ni ndogo basi,bei ya mafuta huwa chini pia.Inavyoonekana kodi inayotozwa kwenye mafuta nchini Tanzania ni kubwa sana,ukilinganisha na ile inayotozwa nchini Rwanda na Burundi.
 
kwa kweli serikali yetu imekithil kwa wizi,huo ni wizi tu.yaani hata haya hawana .utadhani wanaongoza watu wasio na akili.hebu wajilekebishe jamani.wanataka nini kifanyike ndo wajue kuwa watanzania wanaelewa kila kitu?
 
Nadhani kama walivyoongelea wachangiaji wengine kodo kubwa kwenye mafuta ndio sababu ya bei kuwa juu. Zaidi ya hayo ni kwa serikali kukosa creativity ya kutafuta vyanzo vipya vya kodi bali kubakia na vile vile sigara, bia, soda, mafuta etc miaka nenda miaka rudi.

La pili ni wrong mentality iliyokuwepo enzi za ujamaa kuwa ......kwa na gari ni luxury (anasa) wakati siku hizi ni njia ya kurahisisha usafiri tu, ukichukulia kuwa usafiri wa umma si mzuri hivyo.
 
Back
Top Bottom