Gharama za kuwa mkweli

Gerald Robert

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
337
219
7bdbfed9e60d7e3cde999645a04cef10.jpg


Ukitaka kuishi maisha ya kuusimamia ukweli ni vema ukawa mwaminifu katika huo ukweli bila upendeleo wowote.

Ukweli unagharama zake katika maisha ya mwanadamu,

Wapo waliofukuzwa kazi kwa kuusimamia ukweli.

Wapo waliopoteza maisha yao kwa kuusimamia ukweli.

Wapo wenye vilema vya maisha sababu ya kusema yaliyo ya kweli.

Wapo waliofungwa gerezani kwasababu tu walisema ukweli, nk

Unapotaka kuusema ukweli usichague mahali pa kuisemea ukweli huo.

Ukweli usiishie kwenye nyumba za ibada tu bali tunapaswa kuwa wakweli mpaka Makazini mwetu na hata siasa safi nazo zi ahitaji ukweli.

Japokuwa UKWELI unaumiza lakini ukweli unaponya jeraha za moyo na kumfanya mtubkuwa mwenye amani pasipo hofu yeyote.

KWELI NI NENO LA MUNGU, Mtu yeyote anayesimamia ukweli huyo muhubili mzuri wa neno la Mungu.

Imeandikwa.

YOHANA 17:17, UWATAKASE KWA ILE KWELI, NENO LAKO NDIYO KWELI.

Kwakuwa KWELI ni neno la Mungu basi ni vema watu wote tukasimamia hiyo kweli bila kujali itikadi zetu za kidini,kidhehebu, na hata kisiasa kwakuwa hata siasa safi zinahitaji ukweli usio na hila ndani yake.

Mtu Muongo hawezi kuwa jasiri katika kunena na hata kufanya maamuzi ya haki yanayozingatia viwango vya ukweli halisi.

Ukisoma Biblia yako katika kitabu kile cha MARKO 6:17 utaona kwamba YOHANA MBATIZAJI alikufa kwasababu ya kumwambia ukweli mfalme Herode kwamba SI HALALI WEWE KUWA NA MKE WA NDUGUYO (mana Herode alikuwa anashiriki mapenzi na mke wa nduguye .

Kwa kosa hilo la kusema ukweli Yohana alitiwa gerezani na baadae kuuawa katika sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Herode.

Yohana Mbatizaji ni Mtumishi wa Mungu lakini hakuogopa kumwambia ukweli Mfalme Herode maana ndilo jukumu la utumishi wake.

Lakini wati wa leo hawapendi watumishi wa Mungu waseme ukweli juu watawala watawalao kwa udhalimu na hata kwa wale wanaojipatia ajira kwa njia za udanganyifu kinyume na sheria husika.

Shedrack , Meshaki na Abednego walisimama katika kweli kwa kukataa kutii amri dhalimu ya Mfalme Nebukadrineza hata wakatupwa katika tundu la simba lakini kweli iliwaweka huru na kutoka salama katika vinywa vya simba wenye njaa.

Nawaacha na ujumbe huu

Ahsante
 
Back
Top Bottom