Gervas Mkili is NO MORE

Next Level

JF-Expert Member
Nov 17, 2008
3,153
176
Nasikitika kuwajulisha kuwa Ndugu Gervas Mkili hatunaye tena. Mkili alifariki jana Jumapili pale Hospital ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu ya Moyo, tatizo lililogundulika siku moja kabla ya kifo chake.

Kwa wale waliopitia UDSM, bila shaka hawazi kumsahau kijana huyu machachari pale mlimani miaka ya 2000 mpaka 2004 hivi.....! Kama mtakumbuka kijana huyu aliwekwa mahabusi pamoja na vijana wengine kwa sababu ya kuongoza harakati za kudai haki za wanafunzi pale mlimani, ikiwa ni pamoja na BUMU kuongezeka. Na mtakumbuka kutokana na juhudi zake, tuliweza kuongezewa bumu kutoka Tshs 2000 hadi 2500....na kutokana na hili, kuna mgomo uliandaliwa ili kuhakikisha Mkili anatoka SERO, na hili lilifanikiwa baada ya Mzee Luhanga mwenyewe kwenda kumtoa kijana huyu na kutuletea pale Nkrumah na ndip mgomo ukasitishwa!

Mkili mpaka anafariki alikuwa Principal wa shule za Green Acres na alikuwa na mke na mtoto mmoja!

Mwili wa marehemu unatajiwa kusafirishwa leo kuelekea Shinyanga kwa mazishi, kwa walio Dar es Salaam msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach na sasahivi maandalizi ya safari yanafanyika Muhimbili Hospital!

Pole sana dada Deodatha (mjane), pole sana Mama Deo, pole sana Eddie, pole sana Mranda, pole sana Josephine, pole sana Baba Carol, pole sana David (Daz Mwalimu)!

Rest in peace man MKILI......I will indeed miss you!

There is no way out to escape such a divine gift, we loved you brother but God has loved you the most! Umetangulia sisi nasi tutakinywa kikombe hicho. Jina la bwana lihimidiwe milele na milele. Amen
 
Poleni sana wafiwa.
Tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu kwa sala na maombi.
Pumnzika kwa amani Gervas Mkili.
Amina
 
Nakumbuka sana baada ya Kukimbia kwa Lusajo amabaye alikuja kuajiriwa na chuo kama afisa accommodation. Mkili alisimama kidete kutetea haki za wanafunzi. TShs 500 iliyongezeka mwaka 2000 ilikua chini ya uongozi wake thabiti kwa wanafunzi pale DARUSO. Katika mgomo huo yeye alikamatwa pia Akina Zito Kabwe na baadae wakapigwa fine ya kutokukanyaga chuo kwa mwaka mmoja. Tumempoteza kijana mtetea haki za watu. Sitasahau jitihadha zake. Tulikua nae bega kwa bega katika ukombozi huo

Hatutamsahau kamwe. Mungu ailaze Mahali pema Peponi Roho ya marehemu.Amina
 
Nakumbuka tulivyokaa chini pale utawala mpaka marehem Chachage akafanikiwa kututoa tukaenda Nkrumah. Tulikua tunabadilisha song tu za kumuenzi baba wa Taifa. That time bwana it was UD kweli: Akina Zitto, Ruge,Kivugo,Kashube,Makabwe na wengineo tuliokua tunaungurumisha song za "kama sio nguvu zake Mwalimu"
RIP Mkili.
 
OOh. RIP Man.
Nakukumbuka sana pale UDSM during mgomo.
Nimesikitika sana.
 
alikuwa kiongozi shupavu na asiyetetereka wala kuhongeka kwa chochote, umeondoka lakini mazuri uliyopigania yatabaki daima, na utakumbukwa daima.
RIP Commander!
 
Poleni sana wafiwa. Faraja ya MUNGU wa mbinguni iwe juu yenu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu hasa kwa mke wake mpenzi.
Sote tuko njia moja na yatupasa kumwomba MUNGU atusaidie kuzichunguza njia zetu kama ziko sahihi mbele zake ili tuondokapo hapa duniani basi tukaishi maisha ya furaha milele mbinguni.
 
Nimepata shida sana kukubali taarifa hii, namkumbuka Mkili kwa mengi lakini muhimu kama mpiganaji hodari aliyekuwa bado natakiwa katika jamii hii. Tuliumbwa kwa udongo, nasi mavumbini tutarudi. katika hili hatuna hiari ila kumshukuru Mungu. MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU GERVAS MKILI. AMEN!
 
Duuh ina pain kwelikweli...namfahamu MKILI toka Ujiji seminary hizo harakati za mlimani hakuanzia hapo..aliendesha kunji Ujiji seminary na wakafukuzwa pale na kwenda kumalizia shule private...alipokuja mlimani ilikuwa mwendelezo tu..tumepoteza mpiganaji hodari kabisa..RIP MKILI.
 
Kapumzike kwa amANI ,Kamanda Mkili.Kunji la 2004 linatukumbusha mengi na hasa unafiki wa Muhingo Rweyemamu WAKATI HUO AKISOMA Tumaini Iringa, ambaye sasa ni DC wa Handeni na mbeba mabegi wa fisadi Manji.

Tangulia kamanda Mkili na kawasalimia wazalendo wa nchi hii na Afrika wachache tu ni Mzee wetu Mwl, Mzee wetu Sokoine, Lumumba, Azikiwe, Mboya, maskini wote wa Afrika waliotangulia mbele ya haki kwa sababu ya tamaa ya viongozi manyang'au na mafisadi ya Tanzania na Afrika.

Nenda kamanda, nenda kamanda kwa heri kamanda tutaonana paradiso.
 
Back
Top Bottom