Gereji za Wachina hazitoi risiti, zakwepa kodi

Kagosaki

JF-Expert Member
Feb 11, 2010
208
56
Jamani hici majuzi nilikwenda kutengeneza gari langu pale gereji ya wachina iliyoko karibu na Rose Garden. Baada ya matengenezo yaliyodumu saa 4, gari ilitulia kabisa na wakaniambia gharama ambapo nililipia ndani dirishani. Then nikawa nimesubiri hapo risiti. baadae wakaniambia risiti haiko. Nikauliza kulikoni? Wakasema hawatoi risiti. hapo kuna watu wanatengeneza magari na wanalipa hadi milioni 4! Mimi najiuliza, Rose garden sio mbali, ni mjini hapa hapa. Iweje serikali inashindwa kufuatilia mambo haya?
 
Usilaumu serikali kwa kila kitu. Jiulize wewe umechukua hatua gani ili upatiwe risti ambayo ni haki yako. Toka hapo kwenda TRA si mbali pia. Hii tabia ya kulalamika imewafanya watu wengine mshindwe kufuatilia mambo mengine ambayo yapo chini ya uwezo wenu. Sawa serikali imeonesha uzembe mkubwa wa kukusanya kodi lakini ni mara ngapi mmeambiwa kudai risti zetu mnapopewa huduma zenye kuhitaji kupatiwa risti au kufanya manunuzi.
 
Tunalaumu misingi mibaya....kama TRA wako karibu wao hawaoni? Kwani hao Wachina wamekuja leo?
 
Usilaumu serikali kwa kila kitu. Jiulize wewe umechukua hatua gani ili upatiwe risti ambayo ni haki yako. Toka hapo kwenda TRA si mbali pia. Hii tabia ya kulalamika imewafanya watu wengine mshindwe kufuatilia mambo mengine ambayo yapo chini ya uwezo wenu. Sawa serikali imeonesha uzembe mkubwa wa kukusanya kodi lakini ni mara ngapi mmeambiwa kudai risti zetu mnapopewa huduma zenye kuhitaji kupatiwa risti au kufanya manunuzi.

Kaka kaka tema mate chini ndugu yangu, hao wanakula na wakubwa so ukiona hata yule anaekamatwa ni kwamba vigezo na masharti ya wakubwa yanakuwa hayajazingatiwa
 
Hawa wana mtu anayekula nao serikalini. Maana vitendo kama hivyo vinaripotiwa lakini serikali inajifanya haijui. Hivi ndivyo utawala wa sasa unavyowasikinisha watu wetu huku ukiwatajirisha wageni. Hata wafanya biashara wengi wa kihindi unaosikia ni maarufu na matajiri wengi wamefika hapo kwa kutolipa kodi. Wawekezaji ndiyo usiseme. Bongolalaland sasa ni sawa na shamba la bibi tena bibi mwenye kipofu, kichaa na bubu. Hayo ndiyo maisha bora tuliyoahidiwa.
 
Hawa inawezakana wamepewa kibali cha uwekezaji, tena uwekezaji mkubwa na msamaha wa kodi juu (tax holiday). Wewe hujiulizi mtu yuko kwenye nchi ya watu na hataki kufuata sheria, tena anajibu simple tuu.. rist hakuna? na hata ukijifanya kimbelembele sijui unapeleka taarifa TRA, utashangaa itakavyokula kwako. Nchi hii inahitaji kuwa overhaul, ni mabadiliko tu na maombi ndiyo yatakayo okoa kizazi kijacho!
 
Back
Top Bottom