George Yambesi Interview on Public Service Reforms: Je haya maboresho yanaonekana?

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Sijui kama hii ilishakuja humu jamvini (mtanisamehe kama ni repetition) ila nilikuwa naisikiliza hii interview ya George Yambesi na Jamaa wa Princeton University kuhusu maboresho ya utumishi wa umma. Ingawa ni ya zamani, lakini nimejaribu kujiuliza, hivi ukilinganisha fedha zilizotolewa na wafadhili toka mwaka 2000 kwa ajili ya haya maboresho ya utumishi wa umma na haya maboresho ambayo bwana Yambesi anayoyaongelea humu kwenye hii interview (see below) vinaendana kweli. Ingawa anasema kuwa kuna maboresho kwenye public servants salaries, accountability and improvement of systems, hivi kweli ni kwa kiwango tulichokitegemea?

Je swala la Ethics kwenye utumishi wa umma limezingatiwa kweli? Kwa mawazo yangu, weakness kwenye public services management ndio imezaa yote haya tunayoyaongelea kuhusu ufisadi na wizi uliokithiri ndani ya serikali yetu. Fedha hizi zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya miradi ya PSRP (public service reform program) zingetumiwa vizuri kuaddress the issue of ethics kwenye public service nafikiri tungekuwa mbali.

Niliwahi kusikia tetesi kwamba wafadhili wameamua kusitisha huu mradi kwa vile hela zao zilikua zinaliwa tu na kuna watu walitumia mradi huu kujinufaisha (poor us). Hawa wafadhili ndo maana wanatuona sisi mabwege tu. Tunasifika kwa kupewa misaada ya kila aina lakini inaishia tumboni kwa wachache tu. Ni lini tutaamka tuwe serious? Hii wizara ni ya muhimu sana lakini sidhani kama inajitambua.

Sikiliza live hapa

George Yambesi -   Innovations for Successful Societies

au download pdf ya hiyo script hapa

http://www.princeton.edu/successful...y/E15_George_Yambesi_id125/George_Yambesi.pdf
 
Back
Top Bottom