Genetically-modified food

klf

Member
Jun 12, 2009
58
11
Hivi karibuni niliulizwa jinsi ya kuandika maneno haya kwa Kiswahili! Naomba msaade jamvini hapa. Labda vijisehemu hapo chini vitafaa kwa njia moja au nyingine kufanya hii:

1. kuathirika kijenetiki
2. ufundi wa kinasaba
3. teknolojia ya vinasaba
4. kuumba viumbe kwa njia ya vinasaba.
5. ufundi wa kutumia chembe za jinsia na za uzazi
6. teknologia ya viinitete
 
Nadhani kwa tafsiri ya Kiingereza "Genetically Modification (GM)" au "Genetically Modified Organisms (GMOs)" Inahusisha teknologia ya ubadilishaji wa vinasaba vya viumbe hai (GM- techology).

Hakuna tafsiri linganifu na kisayansi iliyo rasmi kwenye Kamusi ya Kiingereza kwa Kiswahili (TUKI") kuyatambua kwa lugha ya Kiswahili baadhi ya maneno yanayoibuka sasa kutokana na kukua sayansi ikiwemo hii ya bioteknologia mpya ( Modern biotech technology)

Binafsi huwa siiamini sana hiyo Kamusi ya kiiingereza kwa kishwahili kwani imekuwa ikitoa tafsiri nyingine ambazo ni vigumu kueleweka kiaalamu kwa kuunganisha maneno mawili tofauti ili kupata neno moja . Hata hivyo. kutokana na matumizi ya baadhi ya maneno katika sekta, tafsiri ifuatayo ndiyo nimekuwa nikielewa kwa baadhi ya maneno japo napo bado ni mkanganyiko tupu:

"Genetic" = Nasaba
"Genetically Modified Organisms (GMos) = viini tete
"Genetically Modified Foods" = Vyakula vilivyobalidilishwa vinasaba , vyenye viinitete
"Technology" = Teknologia
" DNA" or deoxyribonucleic acid = chembe za jinsia za uzazi= vinasaba
"Organisms" = Viumbe.

Mkanganyiko:

1. Neno "nasaba" kisanyansi lina maanisha "viasili" vya viumbe hai "mimea" au wanyama . Hata hivyo, "nasaba" pia linatumika kwenye kiswahili kumaaanisha "vizalia" Kwa mfano hii methali isemayo "Mtaka nyingi nasaba"………

2. "Neno Mabadiliko" kishwahili linatumiwa kumaanisha "Modification" = Lakini unapotaka tafsri ya "GMO" kiswahili kina maanisha "Viini tete" japo katika Kamusi hiyo ya Kishwahili bado utakuwa tena kuwa tasfiri ya neno "Kiini na neno "tete" (Labda nadhani tafsiri ilitokana na jinsi teknolojia husika inavyotumika na athari …siju!)
3. Neno "viumbe " lina maana ya "organisms " lakini ukitaka tafsri ya "Genetically Modified Organisms" inakuwa ni aidha "viini tete" au "teknologia ya kubadilisha vinasaba"

4. Kwenye "nasaba" kuna chembe hai (ndio inatengeneza maisha), kwa lugha ya kiswahili neno "DNA" linaonekana kutumika kama "nasaba" au "genetic". Kwa mfano, katika maepndekezo ya Sheria ya "Human DNA" ilitoa tafsiri ya "vinasaba za binadamu " kumaanisha " human genetic" na sio "viini au chembe za uzazi " kama ilivyo katika tafsri ya "GMOs" ambapo "genetic" inatumika kama "viini tete".


Huu ni mtazamo binafsi !.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom