Gen. Mrisho Sarakikya aliwahi kuhusishwa na Uhaini?

comrade joka kuu,

..., hilo eneo liliitwa farm 17, lipo mtwara, pale, ilikua ni training camp ya wapiganaji wa msumbiji, zimbabwe na south africa(anc)...,

lipo NACHINGWEA, Mtwara - ni kati ya mashamba aliyoyaanzisha mwingereza kwa ajili ya kilimo cha karanga baada ya vita kuu kulisha viwanda vya mafuta vya kwao. Mashamba mengine ya aina hiyo yalikuwa na yapo Urambo Tabora na Kongwa. hata hivyo mafanikio hayakuwepo na badala yake akapandikiza nyoka na scorpions wengi Nachingwea katika harakati za kuwakabili panya - toto tundu kwa karanga
 
ninachojua nyerere alimbadili sarakikywa kwa sababu huyu jamaa alikua msomi na mwanajeshi hodari nyerere akawa anamgwaya pasipo ushahidi wowote ndio mana akambadili na juha aliyekua na darasa sifuri yule twalipo ili aweze kumcontrol vizuri kwa sbabu enzi hizo rais yoyote usalama wake ni kumiliki jeshi vinginevyo mapinduzi yalikua yanakuja!!!!
 
ninachojua nyerere alimbadili sarakikywa kwa sababu huyu jamaa alikua msomi na mwanajeshi hodari nyerere akawa anamgwaya pasipo ushahidi wowote ndio mana akambadili na juha aliyekua na darasa sifuri yule twalipo ili aweze kumcontrol vizuri kwa sbabu enzi hizo rais yoyote usalama wake ni kumiliki jeshi vinginevyo mapinduzi yalikua yanakuja!!!!


Hapana; maoni yako ni speculations tu. Nyerere alimpandisha Sarakikya cheo zaid ya mara tatu kati ya mwaka 1964 hadi 1972 huku akimurusha ngazi kwa spidi kubwa sana: kutoka 2nd Lt kuwa Major, na halafu kutoka major kuwa Lt Col, na baadaye kutoka Lt Col kuwa Brigadier, na mwishoni kutoka Brigadier kuwa Major General.

Angekuwa anamgwaya asingefanya hivyo kwani alikuwa na absolute power. Mbona hakufanya hivyo kwa wengine.

Mwaka 1972 Sarakikya aliteleza ama kwa kuchelewa kutolea maamuzi kuhusu tetesi za mapinduzi ya kijeshi alizokuwa amepata au kwa kuwa mshiriki nyuma ya tetesi hizo. Kuna watu wanajua taarifa hizo kikamilifu, ila tuziache hapa kwa vile hakuna official reports. CIA hutoa ripoti za siri zote baada ya kipindi fulani lakini Tanzania ni siri siri tu.

Hata wale wanajeshi ambao Nyerere aliwapa command mbalimbali baada ya hapo, kwa mfano Walden, Mayunga, Marwa, na Kiwelu walikuwa ni wanajeshi hodari; wote walipata vyeo vya 2nd Lt kipindi kimoja na Sarakikya baada ya training za Kijeshi. Huwa nashangaa sana wale wanaodai kuwa Gen Marwa alipewa madaraka bila kuwa na elimu yoyotewakati alipandishwa kuwa 2nd Lt na Brigadier Douglas mwingereza (aliyekuwa akijali sana taaluma ya kijeshi) kipindi kimoja na Sarakikya na Kavana waliokuwa wametokea Sandhurst. Afisa pekee aliyekuwa amewatangulia waswahili wote na Captain Nyirenda tu, ambaye kipindi hicho alikuwa ni Adjutant 2i/c; hawa makamanda waswahili wengine wote walikuwa ni platoon commanders.
 
Let me speculate, the Northern Corridor struggle for Power! I will not be suprised to hear that Chief Marealle was behind this.

Kuna jamaa wengi Wameru waliokuwa Jeshini ambao walibidi watimke baada ya Sarakikya kupigwa mtama.

The question becomes, was the campaign to instal a Notherner (Chaga, Meru, Maasai, Pare) and get rid of Nyerere?


Nasikitika xana kujua kuwa mtaka kuandika paper na baadhi ya wachangiaji wanaongozwa na ombwe la uchaguzi 2015 "In one way or another mwaweza kuwa wafuasi wa mtoto wa kigogo aliyewahi kusema atahakikisha rais hatoki kaskazini".

Itakeni demokrasia miyoyoni mwenu...msiongozwe na chuki juu ya mtu fulani, kabila au kanda fulani...na kutaka kuwaaminisha wanajamvi kuwa watu wa kanda fulani hawafai kuingoza nchi. Tuachane na ukabila, udini, na ukanda maana ni vikwazo ktk kuijenga Tanzania yetu...tuijenge nchi yetu kwa demokrasia ya kweli kwa kumtaka kiongozi mwenye maadili na mapenzi mema na nchi yetu...haijalishi ni Mhadzabe, Mmalila, Mgogo, muha, mchaga or mngoni1!!!
 
Kati ya nyuzi za JAMBOFORUMS zilizokuwa tamu sana.....still.....ni tamu....
 
Wakuu, nani anafahamu [kiundani] kuhusu uhaini wa aliyewahi kuwa the first Chief of Defence Forces, General Mrisho Sam Hagai Sarakikya...? Niliwahi kusimuliwa zamani kuwa huyu jamaa alipanga kuipindua nchi/ua Nyerere enzi hizo[Lugalo], na kwamba mtu pekee aliyeokoa hayo mapinduzi alikuwa ni General David Musuguri. Je, ni kweli?

P.S. Kuna paper ninayoaandika kuhusu hali aya kisiasa nchini Tanzania tangu tulipopata uhuru mwaka 61 mpaka leo hii, hivyo I want to get the facts straight kabla sija-submit hiyo paper. So help me by posting down anything you know about uhaini wa huyu jamaa. Just anything.
Peace!

Tembelea makao makuu ya jeshi na maelezo sahihi ya utafiti wako.
 
laiti kama JF ingekuwa na kitufe cha ku-rate mabandiko,hili bandiko la 1st September 2008 ningelipa nyota 5.nimesoma posts zote mwanzo mwisho na zote ni BABKUBWA.natamani thread iendelee kwani nahisi mengi hayaja jadiliwa. S/O Kichuguu Moshe Dayan JokaKuu
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Asante mzee mwafrika kwa ufafunuzi wako wa kina; ila nina swali hapo: Hivi, ni nini kilichosababisha Mwalimu akamtupa Sarakikya kuwa balozi wa tanzania [kama sijakosea, Nigeria]; na kumpachika Musuguri kuwa mkuu wa majeshi?

Kanali Abdalla Twalipo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi ndie alichukua nafasi ya Sarakikya
 
jokaKuu,
Hii ya Sarakikya kuondolewa jeshini haikuwa na mizengwe. Julius alimwita pale Msasani akampasha juu ya njama zake za kupindua serikali, Sarakikya akabaki mdomo wazi. Lakini ukiangalia taratibu, utaona Mkapa somehow aliwatafuta wote wale waliogombana na Nyerere, kukiwemo Bibi Titi, Mzee Fundikira, na kujaribu kuwasogeza karibu naye. Nimejiuliza juu ya hili na hitimisho langu bado siwezi kuliweka hapa.

Mkapa anadhaniwa kuwa alihusika na kifo cha mwalimu...
 
sarakikya hakuwa amestaafu rasmi jeshi kwa sababu hakuwa na barua ya kustaafu ndio maana aliweza kupandishwa cheo kuwa jenerali kamili. pia sarakikya hakuomba kupandishwa cheo kwani ni kinyume cha utaratibu, alipandishwa cheo kwa sababu tuhuma zilizomfanya awe nje ya jeshi kwa muda mrefu hazikuwa na ushahidi wala mashiko. mwisho sarakikya alipandishwa cheo siku JWTZ linatimiza miaka 40 kama heshima na kuthamini mchango wake jeshini. ikumbukwe alikuwa mkuu wa majeshi wa kwanza na alipata cheo cha brigedia akiwa bado kijana wa miaka thelathini na kwa maana hiyo sarakikya angetakiwa kuwa mtu wa kwanza kuwa jenerali kamili kama sio mizengwe ya wakati huo.
 
Jasusi,

..sijui kwanini Mwalimu hakumchukulia hatua za kisheria "mhaini" Sarakikya pamoja na "wahaini" wenzake.

..matokeo yake ni "mhaini" anakuja kuwa 4-star general, na taifa linaingia gharama ya kumhudumia "mhaini" mpaka kifo chake.

..kama hiyo siyo MIZENGWE basi tutafute definition nyingine ya neno hilo.

..halafu ni Mwalimu ndiye aliyemsamehe Bibi Titi na kumtoa kifungoni. tena hata kuna mkutano wa hadhara ambao walikuja ku-appear pamoja.

..Mzee Mwinyi naye alikuja kumrudishia Bibi Titi nyumba yake iliyotaifishwa kutokana na azimio. utaona basi Mkapa alikuwa anaendeleza pale alipoachia Mwalimu na Mwinyi.

..Chifu Fundikira sijui matatizo yake na Mwalimu yalikuwa yapi. there are a lot of stories going around.

..Mkapa aliwateua Fundikira,na Makongoro Nyerere, kuwa wabunge ktk mazingira ya kutatanisha sana.

..kwa mtizamo wangu Mkapa alipaswa kumpa "mkono wa pole" Balozi Christopher Kasanga-Tumbo. sielewi ni sababu gani za msingi zilizosababisha akawekwa kizuizini kwa miaka zaidi ya 25.

NB:

..ni kitu gani kilimpelekea Sarakikya kutaka kufanya mapinduzi ya kijeshi?
Sarakikya
 
Mmoja wap
Mkuu naomba katika research yako ufuatilie na issue hii nadhari akuna mahali popote ambapo imezungumzwa au kuandikwa lakini kwa kweli iliumiza watu wengi sana katika miaka ya 1978 ambapo watu wengi ambao walikuwa wasomi (elite) jeshini na Usalama wa Taifa waliachishwa kazi bila sababu yeyote ya msingi na wakatakiwa warudi Vijijini kwao walipo zaliwa. Wengi wa watu walioachishwa walikufa kwa msongo wa mawazo kwa sababu waliachishwa kazi bila sababu na hawakupewa staili zao wanazostahili baada ya kuachishwa kazi, wengi walikuwa wasomi wakubwa tu kwenye Taasisi ya Jeshi na Usalama wa Taifa na wengine ndo kwanza walikuwa kwanza wametoka kwenye masomo katika nchi za Ulaya (Romania, Urusi, East Germany) na ata wengine waliachishwa kazi wakiwa huko huko masomoni. Mchakato wote huu ulisimamiwa na Sokoine. Mkuu huu si uzushi ni ukweli mtupu, fuatilia hii issue na utabaki mdomo wazi. Na mbaya zaidi wale wote walioachishwa kazi walikuwa wanafuatiliwa huko Vijijini na watu wa Usalama, wengi wa watu hawa (Elite) walikufa kwa mawazo, so fuatilia hii ili watanzania waelewe ukweli watakaposoma "PAPER" yako.
wapo babu yangu mdogo alikuwa kichaa mpaka anafariki wakati wote alikuwa anaongea tu kiingereza na kunywa pombe sikuwahi kumsikia mke wake wala mtoto wake
 
Ajawai kuwa na tuhuma hizo.
1, Baada ya Matilda kuwa CDF.
2.Kuteuliwa kuwa waziri wa michezo na Utamaduni. Na kuleta dhahabu ya kwanza Tanzania Michael ya minutia ya madola na michezo AU Kwa pamoja na Olympic Mosko.
3. Kuwa balozi. Tukumbuke akuwai kutoka jeshini hadi alipokumbishwa Rais. Akiwa bado balozi 9jeria, mamma ya Mustafa. Neill Rais Mkapa, kwa sababu anamjua tangu Mkapa akiwa waziri mambo za njee. Akampandisha cheo na kuwa Gen na staahil zote za CDF Mstaafu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom