Gen. David Musuguri apewe fadhila yungali hai

Sidhani kama ni zaidi ya std 7. Anyway, kwa mambo ya medani apewe maua.
wakati tupo mujibu wa sheria op vyama vingi 92 makutupora kuna afande alikua anasema hili sio Jeshi la msuguri la darasa la saba, itakua alikua ni drs la saba
 
Kuna ngazi nyingine ya elimu-jeshi imebaki zaidi ya (kuliko) ujenerali?

Magufuli aliamua kuiingiza Tanzania Military Academy TCU, hivi sasa digrii inazotoa pale ikiwemo ya Military Science inatambuliwa na TCU.
'Ujenerali' sio ngazi ya elimu bali ni cheo. Sina uhakika kama Tanzania military academy 'inatambuliwa' na tcu (I mean accreditation). Nadhani iko chini ya NACTVET.
 
Gen. David Bugozi Musuguri (103) rtd CDF amezawadiwa nini kwenye sherehe za miaka 62 ya uhuru? Miaka 44 ya vita ya Kagera? Miaka 46 ya utumishi jeshini (1942-1988)?

Vita alivyopigana:-

1. WW II 1942
-Battle of Madagascar

2. Uganda - Tanzania 1978-1979
-Battle of Simba Hills
-Battle of Masaka
-Battle of Lukaya
-Operation Dada Idi

NB.
Pana haja ya serikali kumpa alama ya kumbukumbu (souvenir) kufuatia pia kuwa ndiye Kamandaa pekee wa TPDF aliyepigana Kagera ambaye yungali hai na mwenye umri mkubwa kuliko muasisi wa taifa hili. Kiongozi huyu ni alama na fahari ya Tz, KAR na TPDF.

Ramani inaonyesha jinsi TPDF ilivyosambaza vita Uganda nzima na mishale kuonyesha njia za wapiganaji wa jeshi la adui la Uganda walipotorokea.

View attachment 2845166

Ramani kwa hisani ya Goran tek-en.
Mimi nadhani hawa watumishi wa umma walishalipwa mshahara haki yao walipokuwa kazini. Isitoshe hawa watu wa rank za juu kama cdf na wengine, retirement benefits zao ni kubwa sana, kuliko hata inavyopasa kuwa kulingana na uchumi wetu. Fikiria: rais, makamu, pm, spika, deputy, jaji mkuu, cdf na maofisa wengine kadhaa; kila mmoja nyumba, gari, fuel, matibabu, watumishi, etc. Tutajenga shule, hospitali na miradi mingine kwa tabu sana.
 
Kwani wewe huwajui wabongo wengi wanavyopenda kuwashobokea watu bila kuangalia mifumo ikoje?

Ume raise point muhimu sana.

Uchuminwetu mdogi, bado watu wanataka shobo kwa wastaafu.

Kama watu wanataka kumuenzi Msuguli, waipe kambi moja ya jeshi jina lake.

Tunatakiwa kupunguza mzigo kwa walipakodi kwa kupunguza haya mafao manono sana ambayo yanakuwa endelevu mpaka mtu anapokufa.
 
Mwaka jana ma CDF wote wastaafu walipewa magari mapya Landcruiser haya ya kisasa.
right, walipewa, ambayo ni kuvunja sheria na ni ufujaji wa mali ya umma.

Wamepewa Landcruisers kutoka bajeti gani? Kutumia sheria gani? Kwa uhitaji gani ? CDF Mabeyo aliyestaafu leo kesho yake akapewa ulaji mwingine, anahitaji gari lako? CDF Mwamunyange ni jirani yangu kwa baadhi ya assets zake, ni kufuru kwa kwenda mbele, filthy rich. Kakwambia anataka V8 lako?

Mtu anaeweza kugawa gawa ma Landcruisers kwa whims (emotions, mzuka ) wake mwenyewe bila kuhojiwa anashindwaje kujigawia mwenyewe na watoto wake bila kuhojiwa???

Ulaya huwezi kusikia Rais anazuka tu anagawa mali ya umma kwa wastaafu.

Shukrani zote kwa mchango wa wastaafu zimo kwenye sheria ya mafao ya viongozi!

V8 VX moja linatosha ku stock vitanda vyote vya maternity ward Mwananyamala, Amana na Temeke, ambako amini usiamini bado wanalala chini. Watu wa Third Word tunadhalilishwa na kusalitiwa sana na tunaowapa dhamana.
 
Hawa wanajeshi wa zamani walikuwa ni wajeshi wa uwanja wa vita, sio maofisa wa darasani kama walio wengi wa wanajeshi sasa...

Mfano Jenerali Musuguri kashapigana vita vingi akiwa askari wa mstari wa mbele...
Operation Kawe ukwamani.
 
Mimi nadhani hawa watumishi wa umma walishalipwa mshahara haki yao walipokuwa kazini. Isitoshe hawa watu wa rank za juu kama cdf na wengine, retirement benefits zao ni kubwa sana, kuliko hata inavyopasa kuwa kulingana na uchumi wetu. Fikiria: rais, makamu, pm, spika, deputy, jaji mkuu, cdf na maofisa wengine kadhaa; kila mmoja nyumba, gari, fuel, matibabu, watumishi, etc. Tutajenga shule, hospitali na miradi mingine kwa tabu sana.
Mkuu usemayo ni kweli, lakini utaratibu huu umeleta utulivu wa viongozi!

Mkuu utaratibu huu umeondoa mawazo na uwezekano mtu kutaka kuchukua madaraka kwa njia haramu ile apate maslahi, manufaa na maokoto zaidi!

Ni mbinu nzuri kwa amani na mustakabali wa taifa letu!
 
..Natofautiana kidogo na mtizamo wako.

..mbona wanakwiba wanapokuwa madarakani kana kwamba hawana penshen nono baada ya kustaafu?

..Na wengine wamekuwa hata na mawazo ya kubadilisha katiba waendelee kukaa madarakani wakati mafao ya kustaafu ni mazuri?

..Mafao ya viongozi wakuu yapunguzwe. Na ikiwezekana yawe kwa muda fulani, na sio wabebwe mpaka Mungu atakapowachukua.
 
Gen. David Bugozi Musuguri (103) rtd CDF amezawadiwa nini kwenye sherehe za miaka 62 ya uhuru? Miaka 44 ya vita ya Kagera? Miaka 46 ya utumishi jeshini (1942-1988)?

Vita alivyopigana:-

1. WW II 1942
-Battle of Madagascar

2. Uganda - Tanzania 1978-1979
-Battle of Simba Hills
-Battle of Masaka
-Battle of Lukaya
-Operation Dada Idi

NB.
Pana haja ya serikali kumpa alama ya kumbukumbu (souvenir) kufuatia pia kuwa ndiye Kamandaa pekee wa TPDF aliyepigana Kagera ambaye yungali hai na mwenye umri mkubwa kuliko muasisi wa taifa hili. Kiongozi huyu ni alama na fahari ya Tz, KAR na TPDF.

Ramani inaonyesha jinsi TPDF ilivyosambaza vita Uganda nzima na mishale kuonyesha njia za wapiganaji wa jeshi la adui la Uganda walipotorokea.

View attachment 2845166

Ramani kwa hisani ya Goran tek-en.
Kwa navyoelewa huyu mzee anapewa heshima na anatambulika kama inavyotakiwa sasa cjui unatakaje specifically
 
Kweli kabisa... Ila ikitokea ametangulia mbele ya haki L/Cruiser ya leo itamtambulishaje kwa mjukuu wako, kitukuu chako na kilembwe chako wewe kwamba nchi yetu ilikuwa na jenerali Musuguri!?
Kuna maandishi nikimaanisha history ndo mtambuzi wa kweli wa mashujaa wote.
 
CDFs wetu Mungu amewajalia maisha marefu. CDF Sarakikya naye bado yupo hai. Mungu azidi kuwapa uzima na uhai.
 
Back
Top Bottom