Excel
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 19,745
- 10,078
Elpidius Edward, mkazi wa Mtaa wa Katundu mjini Geita amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la uharibifu wa mali zenye thamani ya zaidi shilingi milioni 48.2 za Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki Geita.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imemtia hatiani Elpidius baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka katika shtaka la pili.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Johari Kijuwile.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilifikishwa mahakamani Machi 6, 2023, mshtakiwa akidaiwa kutenda kosa la kuvunja na kuingia kwenye Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo la Geita.
Pia soma: Aliyevamia Kanisa la RC Geita na kuharibu mali za Tsh. Milioni 48 alikuwa na akili timamu