Gazeti la Uhuru - Mhariri wake na waandishi walisoma wapi?

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
531
225
Wana JF heshima mbele.

Najua kuwa gazeti la Uhuru ni la CCM. Najua pia kuwa ni jukumu lake kulinda na kutetea maslahi ya chama chake yaani CCM. Lakini kinachotokea kwenye hili gazeti ni zaidi ya propaganda. Ni ujuha wa kiuandishi. Nashindwa kuelewa inakuwaje hili gazeti linaandika upotoshaji wa habari za wazi kabisa ambazo watu wameona na kusikia lakini linaandika vitu vya uongo kiasi kwamba napata shida kuelewa kama hawa waandishi wamesoma au hawajasoma. Yako magazeti mengi yanayofanya propaganda au kutetea vyama fulani lakini gazeti la uhuru ni rubbish kabisa pale kunapokuwa na habari zinazohusu CDM.


Mifani ipo mingi, lakini nikichukulia mfano wa jana ambapo Mh. Ngeleja alikuwa anatokwa mapovu kuwashambulia CDM kwa hoja ambayo ni mfu kuwa kwnye bajeti yao hawajaonyesha vyanzo vya mapato ya ndani lakini wakaonyesha jumla chini. Hoja hii ilishatolewa ufafanuzi siku mbili kabla na Mh. Zito. Katika mjadala ule Tundu Lissu alitoa ufafanuzi mzuri na Mh. Halima Mdee akapigilia msumari wa mwisho kuwa suala lilikuwa ni typing error na lilishatolewa ufafanuzi siku mbili kabla pale bungeni lakini kutokana na utoro wa Ngeleja ndio maana hakujua kinachoendelea. Baada ya kauli hii Ngeleja na magamba wenzake waliokuwa wanamshangilia wakafyata. Lakini cha kushangaza leo gazeti la Uhuru limeiona hii ni habari ya Front Page na kusema eti Ngeleja awahenyesha CDM: Mbowe, Lissu na Mdee wapwaya! Huu ni ujuha, wananchi wa leo wanajua kinachoendelea bungeni.

Kwa mtindo huu gazeti la Uhuru linasaidia kuchimba kaburi la CCM kwa kwa nguvu zake zote. Najiuliza Mhariri wake na waandishi wake walisoma wapi!
 
Kama unaona linapotosha, basi anzisha la kwako ambalo halitakuwa linapotosha.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Hivi wewe bado unasoma hilo gazeti??mimi hata niwe nasafiri naenda tunisia na hakuna gazeti zaidi ya Uhuru mimi nitachukua uamzi wa kulala!!kuliko kupoteza enegy yangu kusoma Upuupu!
 
huyu ngeleja alikuwa wapi? halafu alivyo maliza akawa anacheka, kama ukiwa unamwangalia lazima utacheka, ni kama wehu. kitu kishakwisha halafu unakirudia tena kwa hasira
 
Swali lako linatakiwa kwenda sambamba na wale wa Tanzania Daima.......

Uhuru = Tanzania Daima = CCM = CHADEMA
 
Hivi wewe bado unasoma hilo gazeti??mimi hata niwe nasafiri naenda tunisia na hakuna gazeti zaidi ya Uhuru mimi nitachukua uamzi wa kulala!!kuliko kupoteza enegy yangu kusoma Upuupu!

Mkuu ntaipata wapi hiyo t-Shirt, ukidesign na top for ladies itakuwa poa, please I need the Dhaifu tshrt
 
Lile gazeti haliitajia wasomi, wengi ni darasa la saba. halafu walisomea TYL.
 
Mwenyekiti dhaifu, kamati kuu uchwara, wabunge wanafiki, chama cha uchizi. Unakijua? Gazeti lake hovyo kabisa.
 
Unalinganisha vitu viwili tofauti kabisa! Tanzania Daima lingekua gazeti la hovyo kama Uhuru lisingekua ktk magazeti 3 ya kila siku yanasomwa kwa wingi Tanzania.
Swali lako linatakiwa kwenda sambamba na wale wa Tanzania Daima.......

Uhuru = Tanzania Daima = CCM = CHADEMA
 
Like JK, like Nape, like Mukama, like Uhuru Newspaper, like you (CALCULATOR)...

Mlitakaje labda??? Mbona hamjui nidhamu za demokrasia??? Zile propaganda za Tanzania Daima huwa hamzioni?? Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha. Aise mnaboa sana nyie watu.
 
Back
Top Bottom