Gavana wa Benki Kuu afafanua hali ya uchumi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
February 29, 2020

Prof. Florens Luoga, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) aongea na kujibu maswali mbalimbali kuhusu hali ya kiuchumi, bei za mazao, biashara na fedha Tanzania.

PART I

  1. Thamani ya Shillingi ya Tanzania na exchange rate kimataifa
  2. Mfumuko wa bei unacheza 3% kwa muda mrefu
  3. Bei ya chakula na mazao kupanda / shuka
  4. Umuhimu wa kusindika mazao ili kuhimili panda shuka ya bei
  5. Mkulima na mikopo / bima / insurance ya mazao
  6. Kilimo bora kikubwa cha umwagiliaji
  7. Mambo mengi kama sera kabambe za kiuchumi hayajatekelezwa ili kuleta utulivu wa kiuchumi
  8. Nini maana ya Tanzania ya viwanda na viwanda viwe vya kuchakata mazao ya kilimo ndiyo jibu la kutatua misukosuko ya kiuchumi
PART II
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

Sera ya BoT ya sarafu safi, mzunguko wa fedha, kusimamia mabenki, noti bandia.



Source: Millard Ayo

====

Akizungumzia malalamiko ya wananchi kuhusu pesa kupungua kwenye mzunguko, Prof Luoga amesema:


“Haiwezekani kuwa na upungufu katika mzunguko. Benki Kuu kila asubuhi lazima tukutane kuangalia hali ya ukwasi katika mabenki, na kila benki sisi tunaiona ina pesa kiasi gani. Kama kuna benki yoyote ambayo tunaona haina pesa ya kutosha kuweza kufanya malipo, mara moja tunachukuwa jukumu la kutoa mkopo kwa benki ile. Tunaweza hata kutoa mkopo wa masaa tu.”

Kuhusu pesa bandia


“Itabidi tuendelee kuongeze elimu ya utambuzi wa noti ili ujue pesa zilizopo kwenye mzunguko ni pesa halali ama ni pesa bandia, kwasababu tumeshapata tatizo na tumewakamata watu wasiopungua sita, saba.”
 
Huyu gavana anatakiwa kupata interview ya angalau dakika 50 itakayofanywa na waandishi mahiri wenye uzoefu maeneo ya kiuchumi na fedha maana toka uteuzi wake sijaona interview ya kina kama ambazo alifanyiwa Prof. Benno Ndulu, gavana aliyepita, na alikuwa anazitoa hapa nchini na kimataifa.
 
Huyu gavana anatakiwa kupata interview ya angalau dakika 50 itakayofanywa na waandishi mahiri wenye uzoefu maeneo ya kiuchumi na fedha maana toka uteuzi wake sijaona interview ya kina kama ambazo alifanyiwa Prof. Benno Ndulu gavana aliyepita na alikuwa anazitoa hapa nchini na kimataifa.
Anazikimbia huyu. Hata ukimsikia tu hapo anachoongea hakieleweki. It seems siyo mchumi.
 
Huyu nadhani anasubiriwa astaafu tu akale pensheni. Sidhani kama ana kitu cha ziada cha kuikwamua nchi.

Uko sawa boss,hapo anawaza Mungu amsaidie astaafu salama akunje mafao yake mfukoni basi mambo ya nyanya kupanda bei watajijua wakulima.

Nilishangaa kumuona mkurugenzi mstaafu wa Tbc ndg mshana ni mwenyekiti wa mtaa kule bunju daah,ndio wastaafu wetu hao.
 
Prof. Sasa hapo anaongelea nini? Zaidi anaongea mambo ambayo anatamani yafanyike lakini hana solutions viable.

Atakuwa hajui risk kwenye business.
Well said
Amejaribu kuangalia investimate but hajaangalia kwa kina risk ya viwanda anavyo jaribu kuvielezea.

Nadhani ni maeneo machache sana kwa hapa Tz wanaunza/kununua nyanya supermarket .

%kubwa tunanunua local market kwa ajili ya udogo wa bei.

Also hajaongea kwa kunyumbulisha ni jinsi gani yeye gavana anaweza kuwezesha watu wa kipato cha chini kuwekeza kwa viwanda vya namna hii.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi anasema nini hapa? Anaongea kama yuko kwenye kijiwe cha kahawa.Yani anakubali alafu anakataa.Tangu nipate akili, Semb na dona haviajwahi kuwa at par kwenye bei.


Wale maharagwe na nyama havijawahi kuwa na uwiano wa 1:2.Sasa anataka kusema na nini. Angeongea na Ndulu au Balali wamwelekeze maujanja.
 
Mkuu labda tuwaulize wachumi, huenda kuna uchumi wa serikali na kuna uchumi wa RAIA.
Uchumi wa serikali unaweza kuwa unakua huku wa RAIA unashuka
Uchumi unakuwa kwenye makaratasi lakini tukirudi kwenye uhalisia huku mitaani hali ni mbaya biashara hazitoki, vitu bei juu wataalamu haya masuala msiyaangalie kwenye vitabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom