Gavana BoT: Baada ya Arusha sasa ni Dar, hakuna haja ya kuwa na Bureau de change zaidi ya 100

UDHIBITI WA BIASHARA YA FEDHA ZA KIGENI- Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga amesema hakuna haja ya jiji la Dar es Salaam kuwa na maduka 100 ya kubadilisha fedha (Bureau de Change) na badala yake kuwa na maduka hayo mipakani na kwenye hoteli za kitalii.

--------
Mwezi uliopita, Benki kuu ya Tanzania (BoT) iliyafunga zaidi ya maduka 100 ya kubadili fedha jijini Arusha kwa kutokukidhi masharti ikiwemo kutokuwa na leseni halali za biashara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gavana wa BoT Profesa Florens Luoga amesema operesheni hiyo haitakoma, na huenda mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam ukafuata baada ya Arusha.

"Hatuhitaji maduka 100 ya kubadilisha fedha Dar es Salaam, kwani kuna benki za kutosha. Tunahitaji maduka ya fedha kwenye sehemu muhimu kama kwenye mahoteli ya kitalii na mipakani," amesema Luoga kwenye mkutano wa Rais John Magufuli na Wakuu wa Mikoa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

"Udhibiti utaendelea kuwa mkali. Hii ni moja ya hatua zitakazoendelea, kanuni ambazo zilikuwepo ziliongeza udanganyifu na maduka yakazidi kuongezeka kiholela," ameongeza Luoga.

Katika operesheni iliyofanyika Arusha mwezi uliopita BoT ilitumia askari kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kutumika kwa askari wa JWTZ kwenye msako huo kulishtua watu wengi na ikamlazimu Luoga kutoa ufafanuzi baadaye.

Kwa mujibu wa Luoga BoT ilitumia wanajeshi "kufuatia askari wengi wa Jeshi la Polisi kuwa katika usimamizi wa mitihani ya kidato cha pili," na taasisi yake ilihusisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wasio na silaha ili kuongeza nguvu katika kufanikisha zoezi hilo.

Kabla ya operesheni hiyo ya kushtukiza, kulishafanyika operesheni nyengine mbili za awali na maofisa wa BoT ambazo hazikuzaa matunda.

Wakati msako wa Arusha ukifanyika, thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ilikuwa imeshuka maradufu na kufikia Sh2,300 kwa dola moja. Mara ya mwisho kwa kiwango hicho kufikiwa ilikuwa Julai 2015 na BoT ililazimika kuchukua hatua mahususi kukabiliana na anguko hilo.

Kwa mujibu wa tovuti ya BoT dola moja ya Marekani kwa hii leo Sesemba kumi imekuwa ikibadilishwa kwa shilingi 2,290.

Wiki mbili zilizopita, BoT ilizipiga marufuku benki tano kuendesha biashara ya sarafu za kigeni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukiuka sharia.

Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara, kwa mujibu wa Alexander Ng'winamila, mkurugenzi wa masoko ya fedha katika benki kuu.

"Benki zilizopigwa marufuku aidha zilifanya biashara nje ya viwango vya masoko au hazikuwasilisha kwa Benki Kuu rrekodi za biashara zao, suala ambalo ni kinyume na sheria," Ng'winamila aliliambia shirika la Reuters.

Chanzo: BBC
Baada ya dhuluma za Arusha wenye akili walishaziondoa hela zao kwenye hayo maduka nchi nzima , na wala si Dar pekee , wamebakisha mabango na vidola uchwara tu
 
Arusha kulikuwa na maduka 37 ya kubadilishia fedha ambayo hayana leseni wala kutambulika, leo yamefungwa halafu kuna watu wanalalamika hivi ni nani aliyewaroga?
Unamaanisha maduka yote yale hayakuwa na leseni...!!!!!!!!
Ila ujue pia unapingana na kauli ya gavana,maana yeye alitangazia umma kuwa amesitisha leseni je ni leseni zipi ikiwa wewe unasema hayakuwa na leseni

......aibu kwako
 
Mkuu hao ndiyo vijana wa chakubanga
Unamaanisha maduka yote yale hayakuwa na leseni...!!!!!!!!
Ila ujue pia unapingana na kauli ya gavana,maana yeye alitangazia umma kuwa amesitisha leseni je ni leseni zipi ikiwa wewe unasema hayakuwa na leseni

......aibu kwako
 
mtongwe haujanielewa,maduka 37 kati ya yale yaliyokaguliwa yalikuwa hayana leseni wala usajili.Sijasema maduka yote bali 37 kati ya yote.
Mengine(tofauti na hayo 37) yalifutiwa leseni.
Hii habari hukuipata au umeamua kukaza kichwa?
 
Hhahaaaaaaa ! Ujue Pombe anauma meno kwa hasira akiisoma hii comment yako , anatamani akulipue na kombora la kutungulia ndege..........nasikia nayeye huwa yupo humu
natamani akutane na comment zangu
maana hawa TISS hawawezi kuzipeleka hizi comment zaidi ya kujaribu kuomba email na ip address ili wakufuatilie wakuteke..
2015 tulimzomea live huyu babu maana tuliona hatari ya kutawaliwa na wahamiaji wa kihutu..
 
Gavana kazi yake ni ku gavan(kudhibiti) uchumi.

Dola itazidi kupanda
 
Jamani hawa washamba na malimbukeni wanataka kutufikisha pabaya sana. Kwanini wanataka wa control kila kitu? Hawajui hii ni nchi ya watu milioni 55. Dat yenyewe ina watu million 5, yaani watu wengi kuliko wa new zealand wote waliotapakaa duniani. Mji wa Sidney una watu million 4 tu na mabenki zaidi ya 1000, sembuse bureau de change
 
Dictatorship = Control everything & everybody.

Jamani hawa washamba na malimbukeni wanataka kutufikisha pabaya sana. Kwanini wanataka wa control kila kitu? Hawajui hii ni nchi ya watu milioni 55. Dat yenyewe ina watu million 5, yaani watu wengi kuliko wa new zealand wote waliotapakaa duniani. Mji wa Sidney una watu million 2 tu na mabenki zaidi ya 1000, sembuse bureau de change
 
Back
Top Bottom