Gari latumbukia Baharini Coco Beach

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,092
Kuna clip inazunguka kwenye Watsap kuwa kuna Gari limetumbukia COCO BEACH mchana huu

====


Gari aina ya Toyota Land Cruiser Prado limetumbukia katika Bahari ya Hindi eneo la ufukwe wa Coco huku polisi wakieleza kusubiri afya ya dereva wa gari hilo kuimarika ili waanze uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai ameieleza Mwananchi Digital leo Jumanne Oktoba 5,2021 kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokana na ajali hiyo baada ya mtu huyo kuokolewa.

Amesema wanasubiri afya yake iimarike ili wafanye uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa dalili zinaonyesha alikuwa ni mtu mwenye mawazo au tatizo la akili.


 
Back
Top Bottom