Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Jeshi la Polisi la Polisi Mkoani Mwanza limekamata gari moja la wizi kutoka nchini Kenya likiwa na mabango ya picha za mgombea ubunge jimbo la Nyamagana jijini Mwanza, ambaye pia ni waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha.
Gari hilo aina ya Rav4 lilikamatwa Septemba 29 mwaka huu majira ya saa 7 mchana, katika kituo cha kuoshea magari kilichopo barabara ya Makongoro jijini hapa, ambapo ilikuwa limeibiwa na watu wasiojulkana jijini Nairobi, nchini Kenya.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Nonosius Komba aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa gari hilo liliingia nchini siku hiyo hiyo (sept 29) likiwa na namba bandia za T 274 ACM.
Kamanda Komba alisema gari hilo ni mali ya Peter Nisiah wa jijini Nairobi, namba zake halisi ni KBK 222 A, na kwamba kukamatwa kwake kulitokana na mawasiliano ya Satelaiti kati ya jeshi la polisi Mwanza na Nairobi Kenya ..
Alisema namba hizo za bandia zilizotumiwa na ambazo zipo hadi sasa hivi kwenye gari hilo la wizi zinaonekana kwenye kumbukumbu ni gari moja aina ya Toyota Mac III lenye injini Na. IAZ4483564 linalomilikiwa na raia wa Kichina aliyetajwa kwa jina la Young Fredyong anayeishi jijini Dar es Salaam.
Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa mabango ya kampeni ya picha za Waziri Masha yaliyobandikwa kwenye gari hilo la wizi, kamanda Kova alingaka na kukataa kuzungumzia juu ya mabango hayo.
Usiniulize suala la mabango ya waziri Masha kuwepo kwenye gari hilo, wewe tambua tu kwamba tumelikamata, sisi hatujui hayo mabango yapo kwa minajili ipi, alisema kwa ukali.
Gazeti hili lilishuhudia kuwepo kwa picha moja ya Masha ambayo imebandikwa mbele ya gari hilo la wizi, huku mabango kadhaa yakiwa yamewekwa ndani ya gari hilo karibu na kiyoo cha mbele.
Waziri Masha alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo ya kuwepo kwa mabango ya picha zake katika gari hilo la wizi hakuweza kupatikana mara moja.
Chanzo: Tanzania Daima.