........
Kweli wazo zima la uchumi bado halijaeleweka kwetu sisi Waafrika, nafikiri hata hatujui ni nini maana ya uzalishaji!
Gambian President Yahya Jammeh has decreed a four-day working week for public officials, making Friday a day of rest to allow residents in the small West African state more time for prayer and agriculture.
....
Hili wazo kwa nchi masikini sijui sana kama lina tija kwani kwa umasikini tulokuwa nao unahitaji kufanya kazi kwa bidii sana. Majuzi nimesikia kuna kundi moja limedai hata sisi tuwe na siku ya ijumaa ya mapumziko, sijaelewa kama twaweza kujenga uchumi ulio bora sana katika ulimwengu wa leo.
Kikubwa kilichopo na ninachokiona kwa walio wengi wetu wanaendekeza swala zima la starehe zaidi kuliko kuwaza jinsi ya kutoka. Uchumi unahitaji kujituma sana na si vinginevyo.
Tusiwahukumu Wagambia kwa kudhani sisi tunajua zaidi ya kwao. Inawezekana kabisa wanafanyakazi wanajihusisha na ujasiria mali na hivyo kupewa siku tatu za kufanya shughuli zao. Hapa kwetu wanafanya kazi siku tano mshahara kiduchu na wafanyakazi wanaishia kufanya ufisadi tu. Kama wafanyakazi watazitumia siku tatu za mapumziko kwa kilimo kwa mfano, nchi ikapata mazao mengi ya chakula na biashara, huo umasikini unaweza kupungua sana.
hivi unafahamu saa 2 hadi saa 9:30 maana yake effectively ni masaa mangapi?Yes naona kuna logic. Kwa kufanya kazi kwa siku 4 kwa wiki tangu saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni Nisawa na tunaofanya siku 5 kwa wiki tangu saa 2 hadi saa 9.30. Masaa ni yaleyale. Nothing strange
kama lengo lingekuwa ni kuongeza uzalishaji basi angepaswa kuongeza masaa ya kufanya kazi na sio kupunguza!
unaweza kuonekana ni uamuzi mbaya kwa nje, lakini na sisi wenyewe tukiutumia mpango huo tunaweza kujiwezesha, kama alivyo sema kutumia muda huo kwenye kilimo, na tukitilia maanani kwamba chakula ni aghali kuanzia mihogo , unga na mboga mboga hivyo muda huo tunaweza kuweka kibustani cha mboga na chumi zetu bado zipo kwenye kilimo, hivyo hata nafasi za kazi ni haba na pia kujenga maana ujenzi wetu ni wa kibinafsi sio makandarasi
hivi kuongeza muda wa kufanya kazi ina maana kuongeza uzalishaji?
mimi nadhani muhimu ni kutafuta njia za kuongeza ufanisi katika kazi.
tatizo nilionalo kwa alhadji, prof. dr. gen. jammeh ni kwamba anawalimisha wafanyakazi wa serikali
kwenye mashamba yake. sasa huenda hayo mabadiliko ni kuwapa wafanyakazi kuhudumia mashamba
yao na pia kwenda hudumia mashamba ya rais. (kweli afrika ina kila aina ya watawala)
kuna njia nyingi za kujenga uchumi, inategemea na mode ya production yako ikoje na products, sasa sisi hatuko industrialised, hivyo opportunity bado ni kidogo, kwenye service industry pia bado tuko nyuma, na utumiaji wa nyenzo ili kuongeza ufanisi bado tuko nyuma matokea yake tija ipo chini na creativity ya watu pia ipo nyuma , matokeo yake serikali au wenye viwanda wana kulipa mshahara wa mlo moja, sasa wewe unaweza kuendelea kufanya kazi zaidi ukapata ziada au huo muda wa ziada ukajilimia mchicha wako nk utakuwa ume save shs ngapi? au umejiongezea kiasi gani kwenye pato lako kwa kulima?Ndio maana nikasema somo la Uchumi au misingi ya Uchumi ambao Dunia nzima inaufuata bado haujaeleweka kwetu Afrika na ndio maana wewe pamoja na Waafrika wengi hawaoni tatizo katika huo uamuzi wa Raisi wa Gambia, lakini kama uamuzi kama huo ungechukuliwa na kiongozi mwingine yoyote nje ya Afrika hata Afrika ya Kaskazini tu ungeona huo moto wake wa watu kulalamika na kusababisha huyu kiongozi kupoteza kazi yake!
Hivyo inaonyesha na kudhihirisha kwamba sisi bado sana!
Hilo unaloliongelea wewe ni hatua ya pili ya maendeleo (yaani ufanisi), ambayo sisi hatujafikia bado, kwa hiyo katika ngazi ya chini ya maendeleo kama yetu ambapo ufanisi hauna nafasi au una nafasi ndogo sana ni kufanya kazi tu kwa masaa mengi ndio suluhisho na sio kupunguza!
Ngoja nikupe mfano chukulia Kiwanda cha chuma kama M.M steel, wafanyakazi wake wengi ni vibarua ambao hawana ujuzi (watu wa kupakia na kushusha mizigo, n.k), hivyo kazi zao ni za mikono na ngumu, kwa hiyo namna ya kuongeza uzalishazi M.M Steel ni kwa kuamua wafanyakazi wafanye kazi masaa mengi tu zaidi, unaweza ukapunguza tu masaa ya kufanya kazi kama watu wako wanaofanya kazi wana ujuzi wa kutosha, nikimaanisha kwa upande wa MmM steel kuna metallurgist wa kutosha, wakemia wa kutosha, watu wa kuendesha mashine wenye ujuzi wa kutosha, sasa hapo ndipo unaweza kuingiza hoja ya ufanisi na flexibility kwa maana kazi ile ile ambayo ingefanywa na watu 15 sasa anafanya mtu mmoja, hivyo hauhitaji tena vibarua, lakini ktk nchi ambazo hata mapinduzi ya viwanda hazijaanza bado kama za Afrika huo ufanisi haupo, hivyo kilichopo KWA SASA ni nguvu kazi tu na misuli ya watu, hivyo unavyoamua kupunguza masaa ya kazi inamaana unapunguza uzalishaji na matokeo yake hata wale wachache walioajiriwa kama vibarua pia wanapoteza kidogo walicho nacho!