FT: Vodacom Premier League, Ruvu Shooting 0 Vs 3 Simba SC uwanja wa Uhuru, Dar es salaam

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Vumbi la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara VPL, kuendelea tena leo ambapo Ruvu Shooting wakiwa wenyeji kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam, wanawaalika vinara wa ligi hiyo Mnyama, Simba SC.

Ruvu Shooting wanaingia dimbani kwa Presha kubwa baada ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa kipigo cha mabao 7-0 dhidi ya Simba SC huku ikiwa ni miaka minne imepita haijawahi kupata hata sare mbele ya Simba.

Habari mbaya zaidi kwa Ruvu ni kwamba, yule kinara wa mabao Emmanuel Okwi (Okwinho) aliyewapiga magoli manne yuko moto akiwa na John Bocco na wakiunda kombinesheni hatari zaidi inayoshika kasi VPL, baada ya kufunga mabao 19 mpaka sasa.

Je, Ruvu Shooting atapindua matokeo na kuwafunga Simba SC?

Kaa nasi kukuletea yatakayojiri. Usikose ukaambiwa. Kumbuka mechi hii itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 2 na kwa upande wa radio TBC Taifa itapeperusha matangazo hayo kuanzia saa 10: 00 jioni.

Vikosi vya timu zote tukianza na wenyeji wa mchezo Ruvu Shooting;

Abdalah Rashid, George Aman, Mau Bofu, Damas Makwaya, Rajabu Zahir, Baraka Mtuwi, Abdulrahaman Mussa, Adam Ibrahim, Issa Kanduru, Fully Maganga, Shaban Mjala.

Sub; Bidii Hussein, Yusuph Nguya, Hamis Kasanga, Hamis Saleh, Khamis Mcha, Jamal Soud, Ishala Juma.

Na upande wa wageni Simba SC wageni wa mchezo huo;

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, Yussuf Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Emmanuel Okwi, John Bocco, Mzamir Yassin.

Sub; Ally Salum, Mohamed Hussein, Paul Bukaba, Mwinyi Kazimoto, Nicolas Gyan, Moses Kitandu, Laudit Mavugo.

0' Naam mpira umekwisha anza hapa uwanja wa Uhuru

Ruvu Shooting 0-0 Simba SC

20' Go goooal, John Boccooooo anaweka kimiani kona ya Kichuyaaaaa.

Ruvu Shooting 0-1 Simba SC

Kadi nyekundu kwa Mau Bofu. Baada kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi.

Alikuwa na kadi ya njano hapo mwanzo

43 ' Okwi anakwenda kwenye benchi na nafasi yake anachukua Laudit Mavugo.

45+3' Wakati wowote mpira utakuwa mapumziko.. Naam mpira ni mapumziko hapa uwanja wa Uhuru Dar es salaam. Ambapo Simba wanakwenda wakiwa mbele ya goli moja dhidi ya Ruvu.

Ruvu Shooting 0-1 Simba SC

46 ' Kipindi cha pili uwanja wa Uhuru Dar es salaam kimeanza. Ruvu Shooting 0-1 Simba Sports

69' Kichuyaaaaa anakwenda.... Mzamir goooooooooaal Mzamir anaipatia goli la pili Simba SC baada ya kazi mzuri ya Kichuyaa

Ruvu Shooting 0-2 Simba SC

75 ' Goooooooooaal goooooooooaal John Bocco anaandika bao la tatu upande wa Simba SC

85' Ruvu Shooting 0-3 Simba SC

90+3' Naam mpira umekwishaaaaaaaa. Kutoka uwanja wa Uhuru Dar es salaam.... mpira umekwisha ambapo Simba SC imeibuka na ushindi wa goli tatu bila majibu dhidi ya Ruvu Shooting, John Bocco akipachika goli mbili na Mzamir Yassin akiandika bao moja. Man of the Match ni John Bocco Adebayor.

Ruvu Shooting 0-3 Simba SC

Asanteni.. Ghazwat
 
01' mpira umekwisha anza hapa uwanja wa Uhuru

Ruvu Shooting 0-0 Simba SC
 
04' Go go la la, namna gani hapa John Bocco, anakosa bao la wazi hapa
 
Back
Top Bottom