FT: Kombe la Shirikisho: Rivers United 0-2 Young Africans. 23, 04, 2023

Carasco Putin

JF-Expert Member
Apr 23, 2022
8,825
26,393
Mabingwa wa kutandaza soka tamu, soka la kuvutia, soka la kumtoa nyoka pangoni, soka ice cream, soka lenye viwango vya Dunia. Hapa nawazungumzia Young Africans.

Baada ya kupokea kichapo kikali toka kwa mahasimu wao simba Sports Club leo mida ya saa 10:00 jioni, Wananchi wenye nchi yao Young Africans watashuka pale dimba la Estadio de Dodswill Akpabio nchini Nigeria kutafuta alama tatu za ushindi mnono ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia nusu fainal kwa mara ya kwanza katika Fainali ya Michuano ya Shirikisho Barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa hawa walishakutana katika michezo miwili huko, Timu ya Rivers United iliichakaza vibaya sana Wananchi kwa kuwafunga nyumbani na ugenini. Mchezo wa leo utakuwa mkali kwa timu zote.

Kila la kheri Yanga.

==========
Updates..

Yanga Rivers.jpg
Mchezo umeanza
5' Bado mchezo hauna kasi kubwa, timu zote zinasomana
9' Rivers wanakosa nafasi ya wazi, mpira unamkataa mshambuliaji wao karibu na lango la Yanga
12' Mashabiki si wengi uwanjani
15' Yanga wanafanya shambulizi kali, lakini wanashindwa kuweka mpira wavuni
26' Azizi Ki na FaridI Mussa wanapata nafasi ya kufunga lakini wanakosa umakini
38' Mashambulizi ni makali na timu zinapokezana kushambulia
41' Yanga wanaonesha ubora wa kuzuia mashambulizi ya Rivers
45' Zinaongezwa dakika 2

MAPUMZIKO: Matokeo bado ni 0-0

Mabadiliko kwa Yanga, wanaingia Kibwana Shomari, Moloko na Tuisila Kisinda wametoka Lomalisa, Djuma na Faridi Musa

Kipindi cha pili kimeanza
47' Bado mambo ni magumu kwa timu zote
68' Mayele anakosa nafasi nzuri akishindwa kumalizia kazi nzuri ya Azizi Ki
74' Fiston Mayele anafunga
VAR: Mwamuzi anapitia kama kuna OFFSIDE, mchezo umesimama kwa muda
Mwamuzi anaruhusu mchezo uendelee kuwa ni goli halali
78' Natoka Mudathir anaingia Zawadi Mauya
81' Mayelee anafunga goli la pili kwa Yanga, ni bada ya Rivers kushindwa kufunga ndipo Yanga wakafanya shambulizi la kushtukiza
90' Zinaongezwa dakika 6
Full Time
 
Leo yanga tunaweza tukafungwa amini usiamini ila kuchomoka na ushindi leo ni ngumu sanaaaa.

Nina was was na mentality ya wachezaji toka tupigwe na kitu kizito kwenye mechi ya derby.wachezaji morali haiko juu kama pale awali.

Kama uchawi wa bagamoyo tu ulituchapa goli 2 sasa uchawi wa nigeria je??????
 
IMG_6203.jpg


ANAITWA NAZIRU AUWALU mshambuliaji wa TIMU YANGU YA UTOTONI YA RIVERS UNITED ya Nigeria huko huyu anafunga hata akiwa benchi anakabwa na mabeki 7 mechi 10 anagoli 48 kacheza Aston Villa kila la kheri RIVERS UNITED amesema asipofunga leo anaacha kucheza mpira RIVERS UNITED NGUVU MOJA
 
Leo yanga tunaweza tukafungwa amini usiamini ila kuchomoka na ushindi leo ni ngumu sanaaaa.

Nina was was na mentality ya wachezaji toka tupigwe na kitu kizito kwenye mechi ya derby.wachezaji morali haiko juu kama pale awali.

Kama uchawi wa bagamoyo tu ulituchapa goli 2 sasa uchawi wa nigeria je??????
Yanga haina watu matutusa kama wewe, jitaje timu yako rasmi, hata ushoga unaanzaga hivihivi kwa kutamani jinsia ya Pili.
 
Yanga haina watu matutusa kama wewe, jitaje timu yako rasmi, hata ushoga unaanzaga hivihivi kwa kutamani jinsia ya Pili.
Kwann akil zenu ziko negative sana..Kwann uwaze specifically USHOGA?? why not other stuffs? Are you a gay brother?
Why not honor your integrity if u really are a gentleman?
Have been infected by gaysm brother?
 
Leo yanga tunaweza tukafungwa amini usiamini ila kuchomoka na ushindi leo ni ngumu sanaaaa.

Nina was was na mentality ya wachezaji toka tupigwe na kitu kizito kwenye mechi ya derby.wachezaji morali haiko juu kama pale awali.

Kama uchawi wa bagamoyo tu ulituchapa goli 2 sasa uchawi wa nigeria je??????
Usihofu Nabi ni Profesa wa soka sisi Utoh tunashinda uwanja wowote mbona waarabu tuliwatoa kwao. Game ya derby ya Simba ni ya mauzauza na Wala Yanga haikuwauma kupoteza sababu goli si halali Kona pia haikuwa halali alietoa mpira ni mchezaji wa Simba kama kungekuwa na VAR goli lingefutwa mechi ingekuwa vingine na hata huyo Kibu asingefunga halafu we uliona wapi refa kwanza ni Mwanamke kapewa bahasha na wakati kageuka upande mwingine anaelekeza wachezaji wanaogombana huko nyuma mpira umeanzishwa Tena mpira wa Kona bila filimbi ya mwamuzi. Na kwa kawaida tunaona ulaya refa akipanga wachezaji kwenye 18 kabla ya Kona kupigwa mshika kibendera husimama mbele ya mpira Ili Kona isipigwe bila mwamuzi kuwa tayari na kuruhusu ila mechi ya Simba haikuwa hivyo Simba walivizia Yanga hawajajipanga na bila filimbi ya mwamuzi aliekuwa akiangalia kwingine wakaanza mpira kihuni huni tu na kufunga na kuwatoa mchezoni Yanga ambao kutokana na uchawi mzito wa kukafini maiti hawakuwa wakielewa wako uwanja wa taifa au chamazi! Kwa mara ya kwanza tangu Bangala aje Yanga kwenye derby aliomba kutolewa akisema mpira hauoni!! Magoli ya kichawi Huwa ya ajabu ajabu mnashtukia tu mmefungwa!

Tangu Prof Nabi atue Jangwani Simba Haina msuli wa kuifunga Yanga kihalali bila makandokando mechi ya mwisho Kigoma tulicheza kumi baada ya mukoko kutolewa kwa red ya mchongo na mechi ya juzikati mpira umeanzishwa wakati refa Yuko anapanga wachezaji sio football Ile ni uhuni tu kuhakikisha angalau Simba wanapata kombe moja nalo ni kuifunga Yanga maana kabati lao la makombe limejaa vumbi mwaka wa pili Sasa!!

Kosa la kiufundi la Yanga kwenye derby ni kumuweka nje Mudathir kama ambavyo Mashabiki tulitegemea kivuruge Huyu ataanza wakamuweka benchi na alipoingia uliona nusu uwanja Simba hawakuonana Tena. Pia mechi ya Simba ilifaa Baka na Nondo ndo wacheze double sentahafu.

Nigeria tunashinda Leo Prof Nabi Huwa harudii makosa! Hii ni mechi ya kisasi itakuwa na balaa kubwa la Moloko na Mudathir!
 
Usihofu Nabi ni Profesa wa soka sisi tunashinda uwanja wowote mbona waarabu tuliwatoa kwao. Game ya derby ya Simba ni ya mauzauza na Wala Yanga haikuwauma kupoteza sababu goli si halali Kona pia haikuwa halali alietoa mpira ni mchezaji wa Simba kama kungekuwa na VAR goli lingefutwa mechi ingekuwa vingine na hata huyo Kibu asingefunga halafu we uliona wapi refa kwanza ni Mwanamke kapewa bahasha na wakati kageuka upande mwingine anaelekeza wachezaji wanaogombana huko nyuma mpira umeanzishwa Tena mpira wa Kona bila filimbi ya mwamuzi. Na kwa kawaida tunaona ulaya refa akipanga wachezaji kwenye 18 kabla ya Kona kupigwa mshika kibendera husimama mbele ya mpira Ili Kona isipigwe bila mwamuzi kuwa tayari na kuruhusu ila mechi ya Simba haikuwa hivyo Simba walivizia Yanga hawajajipanga na bila filimbi ya mwamuzi aliekuwa akiangalia kwingine wakaanza mpira na kufunga na kuwatoa mchezoni Yanga ambao kutokana na uchawi mzito wa kukafini maiti hawakuwa wakielewa wako uwanja wa taifa au chamazi!

Kosa la kiufundi ni kumuweka nje Mudathir kama ambavyo Mashabiki tulitegemea kivuruge Huyu ataanza wakamuweka benchi na alipoingia uliona nusu uwanja Simba hawakuonana Tena. Pia mechi ya Simba ilifaa Baka na Nondo ndo wacheze double sentahafu.

Nigeria tunashinda Leo Prof Nabi Huwa harudii makosa!
Shukrani mkuu umenipa sababu za kujiamini.Tuombe ikawe kheri
 
Back
Top Bottom