FT: CAF Confederation Cup | TP Mazembe 0-1 Yanga | Stade Tp Mazembe | 02.04.2023

mwarabu feki

JF-Expert Member
Feb 16, 2023
682
1,461
Mabingwa wa kutandaza kandanda safi barani Afrika, kandanda lilioenda shule, kandanda lenye viwango vya UEFA hapa nawazungumzia Young Africans leo wanashuka dimbani huko Lubumbashi nchini Kongo kumenyana na Tp Mazembe katika mchezo wa mwisho wa kundi D kombe la shirikisho barani Afrika.
Ikumbukwe mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es Salaam Yanga ilishinda goli 3-1 hivyo Tp Mazembe wataingia wakiwa na kiu ya kulipa kisasi.

Yanga wanaongoza kundi D wakiwa na point 10 na tayari wametinga hatua ya robo fainali hivyo nao watataka washinde ili kujihakikishia uongozi wa kundi lao.

Mechi hii itapigwa katika uwanja wa Tp Mazembe na itaanza mida ya saa 10:00 jioni na itarushwa Azam Sports kupitia channel yake ya ZBC2

Tuwe wote Kwa dakika 90 za mchezo huu..........

Kikosi cha YANGA kinachoanza
FstXalwWAAE46fy.jpg
Metacha
Job
Lomalisa
Bacca
Mwamnyeto
Bangala
Mudathir
SureBoy
Moloko
Musonda
Mayele


Wananchiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii


Stay tuned

Mchezo umeanza licha ya kuwa idadi ya mashabiki ni wachache, inavyoonekana ni kama wamekata tamaa baada ya Mazembe kuwa na matokeo mabaya
1' Ngoma imeanza
20' Kasi ya mchezo si kubwa sana, timu zote zinapeana zamu kumiliki mpira
35' Mazembe wanajaribu kutengeneza nafasi lakini Yanga wapo makini
40' Timu zinapeana zamu kumiliki mpira
45' Zinaongezwa dakika 2

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
50' Mazembe wanafanya shambulizi kali langoni mwa Yanga lakini shuti linatoka nje
54' Mabadiliko kwa Yanga, Farid Mussa anaingia anatoka Mudathiri Yahya
56' Mazembe wameongea kasi ya kushambulia tofauti na kipindi cha kwanza
65' Farid Mussa anafunga goli baada ya kipa wa Mazembe kuutema mpira ndani ya eneo la 18
80' Anatoka Musonda anaingia Clement Mzize
88' Beki wa Mazembe anapata kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Mayele

Full Time

Fstp0qOXsAIxCcC.jpg
 
Unatuletea updates za kombe la mbuzi halafu unatuambia stay tuned!, nani ana muda huo
 
Jamani mimi nilikuwa nanjilinji kulima ufuta na yanga wakati natoka alikuwa klabu bingwa na kwa ninavyofahamu mechi za klabu bingwa zimeisha jana.

Sasa uto leo anacheza michuano gani na kule klabu bingwa baada ya kumtoa zalan ilikuwaje?
 
Jamani mimi nilikuwa nanjilinji kulima ufuta na yanga wakati natoka alikuwa klabu bingwa na kwa ninavyofahamu mechi za klabu bingwa zimeisha jana.

Sasa uto leo anacheza michuano gani na kule klabu bingwa baada ya kumtoa zalan ilikuwaje?
Michuano anayocheza leo ukawaulize mashabiki wenzako wa Simba kuwa waliwasha moto viwanja vya watu ili wavuke stage kwenye michuano ipi?
 
Back
Top Bottom