Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 20,739
- 45,188
Habari zenu mabibi na mabwana!
Leo ni sikukuu kubwa barani Ulaya na Duniani kwa ujumla. Ni mchezo wa Fainali ya Uefa Champions League kati ya Liverpool Vs Real Madrid.
Awali fainali hii ilipangwa ifanyike jijini Saint Petersburg, nchini Urusi. Ila kutokana na Urusi kuivamia Ukraine Uefa wakahamisha fainali hiyo jijini Paris nchini Ufaransa.
Hii itakuwa fainali ya tatu kuzikutanisha timu hizi mbili, ambapo mara ya kwanza walikutana mwaka 1981 hapahapa jijini Paris na Liverpool kubeba ndoo hiyo kwa 1-0.
Fainali ya pili kuzikutanisha timu hizi ni mwaka 2018 kule jijini Kiev ambapi Madrid alishinda kwa mabao 3-1 shukrani za pekee zilimuendea Sergio Ramos kwa kumtengua bega Mo Salah.
Kwahiyo hii itakuwa Fainali ya kisasi baina ya timu hizo mbili. Huku mashabiki wakisubiria kwa hamu mtanange huo.
Uwanja huu wa Stade de France, umewahi kuandaa fainali mbili tangu uanzishwe ile ya mwaka 2000 ambapo Real Madrid alitwaa kombe kwa kumfunga Valencia. Na mara ya pili kwa uwanja huu kuandaa mchezo wa fainali ya UCL ni pale Barca alipotwaa ubingwa dhidi ya Arsenal mwaka 2006. Kwahyo tuseme uwanja huu unazibeba sana timu za Spain.
Liverpool wataingia katika mchezo huu wakitafuta ubingwa wao wa 7 wa UCL baada ya kuzitoa timu kama Inter Milan, Benfica na Villareal, wengi wakisema Liverpool alipitia njia nyepesi.
Real Madrid watashuka dimbani kutafuta ubingwa wao wa 14 wa UCL baada ya kuzitoa timu ngumu kama PSG, Chelsea na Man City na wengi wakisema wamepitia njia ngumu.
Refarii wa mchezo huu ni Clement Turpin kutoka nchini Ufaransa. Mwamuzi huyu mwaka 2021 alichezesha Fainali ya Europa League kati ya Villareal Vs Man Utd ambapo Villareal walitwaa ubingwa kwa mikwaju ya penati. Mwamuzi huyu ana miaka 40 hivyo atalimudu vyema pambano hilo.
Mchezo huu utapigwa majira ya saa 4:00 Usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki na utakuwa live kupitia Dstv chaneli namba 223 kifurushi cha Compact. Bila kusahau Canal nao watakuwa mubashara.
Tukutane hapa kwa updates huku mimi nikiwapa nafasi Real Madrid kutwaa ndoo! Karibuni sana...
============================
UEFA: REAL MADRID YATWAA UBINGWA, YAIPIGA LIVERPOOL 1-0
Real Madrid imeendelea kuuonesha Ulimwengu kuwa Ufalme wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ni wao baada ya kutwaa kombe hilo kwa kuifunga Liverpool goli 1-0 katika fainali, usiku wa kuamkia leo Mei 29, 2022.
Goli pekee la Vinícius Júnior katika dakika ya 59 lilitosha kuipa ubingwa Real Madrid ambapo hilo ni taji lao la 14 katika michuano hiyo wakati timu inayofuatia kwa kubeba kombe hilo mara nyingi ni AC Milan ambayo imelibeba mara 7. Liverpool yenyewe imebeba kombe hilo mara 6.
2021/22 umekuwa msimu mzuri wa Real Madrid kwa kuwa imeumaliza vizuri ikiwa pia imebeba taji la Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Liverpool yenyewe imeshika nafasi ya pili UEFA na imemaliza ikiwa katika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya England.