Freeman Mbowe: Kupona kwa Mhe. Lissu ni Mpango wa Mungu, Watanzania tuendele Kumuombea

Miradi yenyewe haipo!
Wakandarasi wapo hoi!
Kama huamini we tangaza kandarasi ya kufukuza na kumkamata kuku. usishangae utitiri wa makampuni utakaoibuka!
Tena makampuni class 1, 2 na 3.
Mkuu upo nchi gani? Hvi flyover ya TAZARA na Ubungo, standard gauge, Stieglers gorge, REA, Bomba la hoima, upanuzi wa barabara morogoro rd. N.k hii siyo miradi? Hao wakandarasi unaowaongelea watakua wale wa kampuni za dili za mifukoni.
 
Mkuu upo nchi gani? Hvi flyover ya TAZARA na Ubungo, standard gauge, Stieglers gorge, REA, Bomba la hoima, upanuzi wa barabara morogoro rd. N.k hii siyo miradi? Hao wakandarasi unaowaongelea watakua wale wa kampuni za dili za mifukoni.
Miradi hiyo inachota hela kupeleka nje, haiongezi mzunguko wa hela nchini, hii ni hasara.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Msigwa na Lema wanajihudia hapo hapo!!
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Mchawi utamjua tu
 
Ugua pole TL.
Mbowe inabidi afahamu kitu kimoja,kama mabalozi wenyewe wakienda ikulu wanakunywa juisi na pipi,maana yake huko wapinzani hamna tena zile zama za kwenda kunywa maziwa na cocoa ikulu ,hela zote zinaenda kwenye miradi.
Chato
 
Kupona kwa Mhe. Lissu ni mpango wa Mungu, nawaomba Watanzania wenzetu waendelee kumuombea kwa Mungu pamoja na kuchangia gharama za matibabu, kwa kuwa gharama zake ni kubwa ambazo chama pekee hakiwezi kuzimudu bila ya misaada kutoka kwa watu mbalimbali.

Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya.

Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika.

UPINZANI NI KAZI NGUMU

Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.

Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.

Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatenegeneza hasira kubwa ndani ya jamii.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Kadai ulizotoa, sisi tutaendelea kuchanga tu mpaka kieleweke.
 
Mpelekee nayo Mbowe zoazoa. Atawapiga sana mwaka huu. Kama sahizi amepanga kwenda Marekani, mkachanga, kesho atasema anampeleka Mbinguni.

Mwambie arudi asiteketeza hela zetu kwa kutuona sisi fala.
Ni lini umekuwa na hela wewe?
 
Leo yapata majuma mawili na siku kadhaa sisi wana wako tulipokuja mbele zako kwa vilio na kwikwi tukimuombea nusra mja wako Tundu Lissu.

Mungu Baba Mwenye Enzi kuu tunakushukuru.
Tunakushukuru kwakuwa umeendelea kutenda muujiz wako kwa ndugu yetu kipenzi chetu na Baba wa familia yake ukimponya na kumuimarisha siku adi siku.

Tunakushukuru kwakuwa waovu umewakatalia mbali na unaendelea kuwaaibisha siku hadi siku, na kuanzia sasa watakutii na kukujua vyema kwakuwa hawatofanikiwa kwa matendo yaliyo kinyume na mapenzi yako.

Jina lako litukuzwe, sifa na utukufu ni vyako wewe pekee milele na milele.

Ni katika jina la Bwana Yesu Kristu jina lipitalo majina yote, tumekushukuru.
Aamina.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Subiri umiminiwe risasi arobaini mwilini mwako ndio utajua ghalama halisi.
 
Mimi ni mzee kwa sababu umri wangu naruhusiwa kutibiwa bure.

Bado najiuliza, Hawa Wazungu waliotuletea Demokrasia ya vyama Vingi, najiuliza vyama Tawala na vyama vya upinzani vinafanyanya nini wakati wa uchaguzi na baada ya kupatikana mshindi?

Ninavyojua toka Mama Clinton ashindwe, pamoja na kuwa aliibiwa kura kwa kutumia Taifa kubwa, lakini huyu Mama hatujamsikia akipingana na Rais aliyeko madarakani. Amekaa kimya akijiandaa na kujenga chama chake kulingana na katiba ya chama na ya INCHI. Wanaopingana na Rais aliyeko madarakani ni Taasisi za kupigania haki za Binadamu anapoenda kinyume na haki za binadamu

Tanzania inaonekana hakuna tufauti kati ya kipindi cha kampeni na baada ya kupata mshindi.

Kwa nini haya tunayotaka kuyasema, hatuyasemi kwa utaratibu, upendo,ushirikiano nk.
Tunaowasemea ni wanainchi, kwa hiyo kama waliowengi wanakubaliana na Kiongozi aliyeko amdarakani, tuungane nao.

Kilichoko sasa kati ya Viongozi walioko madarakani na wale walioshindwa ni coflict of interest na kiutawala tunaiita ni swala la 'Personalities'.

Kwa mfano ukigundua kuwa mke wa rafiki yako yuko Guest House na mtu, je unasababu ya kwenda kutoa taarifa Polisi?

Kama utaenda Polisi au utakimbia mbio kwenda kutoa taarifa kwa rafiki yako, wewe ni mpumbavu.

Wanainchi walio wengi tunao sema tunawapigania hawana taarifa na wala hawaijui hii vita.

Wanachojua ni kuwa Walichagua Rais, Mbunge, Diwani na Mwenyekiti wa kitongoji.
Hata kama hawampendi, watasema, uchaguzi ujao huyu hatumpi kura tena.
Uendeshaji wa siasa hufuata katiba ya nchi husika, ni pale utakapotuwekea hapa katiba na sheria ya vyama vya siasa ya marekani ili tuzifananishe na tujikosoe.
 
Nimeiona.Unajua wengine wako kwa ajili ya kuhakikisha Lissu hapati michango ya kutosha na mawazo yao makubwa kuishi kwake kwao ni adhabu.

Hivyo wenye moyo wa kuchanga tutaendelea kuchanga
Hope he will be back on his feet
 
06e390c38555e025e59071966696d895.jpg

Huyu ni mjumbe wa baraza la congress nchini marekani alipigwa risasi wakati walipokuwa kwenye michezo ya baseball. Leo amehudhuria kikao kwa mara ya kwanza baada ya kutoka hospitalini.
Tuzidi kumuombea na ndugu yetu Tundu Lissu, atarudi, yes akiwa mzima wa afya njema aendelee kulijenga taifa lake.
Tumuombe, maombi yana nguvu ya ajabu sana tusichoke wala tusife mioyo.
 
Back
Top Bottom