Bashatu
JF-Expert Member
- Nov 8, 2015
- 834
- 885
Nadhan kakwelewa. Ni kweli hata ufanyeje, hata uwasaidieje watu bado kuna watakaosema hawajasaidiwa au anajiosha.Mbona yote watu washafanya sana humu.
Mbona wote tunajifunza hapa, kwani kuna guru wa forex hapa?
Kuna mtu kalalamika kapewa kitabu lugha hajui.
Sasa mtu hajui Kiingereza anatakakufanya Forex, turudi kuanza kumfundisha Kiingereza?
Mbona na mimi najifunza humo humo kwenye vitabu na online na nimepiga hela nzuri last week, wiki hii nimeanza kupigwa GBP/USD nikabadili gia angani AUD/JPY mpaka sasa napiga?
Hakuna mtu hata mmoja aliyenifundisha zaidi ya kusoma mambo mwenyewe tu.
Mtu kama hana ubishi na utashi wa kujua hata umfundishe vipi hataweza, na mwenye ubishi na utashi wa kutaka kujua hata ukimpa kitabu hajui Kiingereza ataenda kukisoma kwa kamusi ya Kiswahili na Kiingereza mpaka ajue.
Mi sikuwahi hata kuandika definition ya forex lakini nimeanza kwa demo account, nimedownload videos youtube, nimetoa vitabu mpaka google scholars.
Hivi sijui watu wanataka walishw vipi