Food For thought: Kwanini Watu Sasa wanazikwa Usiku, tena na vyombo vya Serikali?

Mida hii ndio wanafanya maandalizi ya kushusha mzigo mpya. Yaani siku hizi ukifa unazikwa kinyonge sana, watoto wako wadogo na ndugu hawapati nafasi ya kukuaga kwa mara ya mwisho. Unazikwa usiku kwa usiku kama mhalifu wa kivita. Nimeandika kwa hisia sana!
 
Sisi tunachapa kazi usitufundishe uvivu

Huku tukichukua tahadhari zinazotolewa na viongozi wetu wa Afya kuhusu kupambana na corona

Nyie chadema jifungieni
Siku akianguka mtu wako wakaribu ndiyo utajua ushabiki unao fanyaga hauna maana. Hapo utajua Dunia inafanya kazi vipi.
 
Nimeuliza swali lakini nia yangu ni kutoa Wito kwamba tuchukue hatua Sasa kujiokoa tumwache Rais Magufuli Akae Kwao Chato, nadhani kwake familia na Mama Mzazi wake wakati huu ni muhimu kuliko nchi...Ndugu, tuamke tunakwisha


Haya ni Makaburi ya Ununio Dar es Salaam, mmoja wa waliozikwa juzi Usiku ni Bernard Ngoyai Lowassa, sina Hakika kama ni Mwanafamilia wa Familia ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa
View attachment 1434665
Watanzania msijizoeshe kulalamikia watawala kwa jambo ambalo hawajafanya wao.
Juzi hapa mkalalamika kwamba watu ni wengi wanaoumwa pia waliofariki ila serikali haitoi maelezo, leo PM Majaliwa katolea ufafanuzi hayo mambo lakini tena mmeanza kuzua mambo mengine.

Watu kuzikwa usiku sio tatizo, jaribuni kuhoji nini chanzo cha tatizo watu kufa wengi kipindi hiki kama taifa na majibu yapatikane.

Watu mnaleta siasa na ujuaji mwingi kumlaumu Magufuli kama ndio aliyeileta Korona.

Marekani, Italy, Spain, UK n.k wameweka total lockdown lakini kila siku watu maelfu wanakufa huko kwao, Tanzania watu wakifa mnamlaumu Magufuli kwa lipi?

Korona ni ugonjwa wa dunia nzima sio Tanzania pekee na watu wengi wanaofariki sana ni watu wazima na wenye matatizo mengine ya afya, Tanzania inawezekana watu wakafa wengi zaidi sababu kwa East Africa kama nchi sio ndio wengi zaidi kwa idadi hasa kwa Jiji kama DSM,
pili ni nchi ambayo ni Coridor kwa maana watu wa mataifa mengi walikua wanapita hapa
pia inawezekana tukafa wengi sababu ya mfumo wetu wa maisha.

Mimi siamini kama Corona inaambukiza kwa Kushikana au kutovaa Barakoa sababu ukiangalia wengi wa waliofariki ni watu wasiojichanganya sana na watu mitaani.

Hivyo tuache kumlaumu Magufuli sababu hata nchi ambazo ziliweka total lockdown bado maambukizi yapo juu na mifani ipo.

Kenya kutokua na vifo vingi sio sababu kuweka lockdown sababu hata lockdown yao ya kihuni tu.
Nenda North Nigeria tangu juzi watu wengi wamekufa sana sasa Tanzania watu wakifa mnalaumu Magufuli

Badilikeni na hiyo mitazamo ya kisiasa na kitoto kwa kila kitu kuhusu Corona kumlaumu Magufuli

Serikali inajitahidi kuwazika watu kwa heshima lakini bado mnalaumu.

Korona ni ugonjwa wa dunia nzima sio Tanzania peke yake


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo sio kubwa kama mnavyoli-potray.Mko very misinformed na vyombo vya habari ambavyo nia yao ni ku-create panic na kutaka ionekane kwamba Waafrika tunakufa.Kwa bahati mbaya their wish has not materialized,sasa wanatumia kila mbinu iwezekanayo kuonyesha kwamba hali ni mbaya.Hali sio mbaya,10 people dead hata kama ingekuwa kwa the so called C-19 is nothing out of 56 million people.Acheni ujinga.


Fuata link zifuatazo ujifunze,acha kutisha watu.


Stop the panic, end the total isolation | SOTN: Alternative News, Analysis & Commentary


The Illusory Pandemic and the Diagnostic Tests | SOTN: Alternative News, Analysis & Commentary

Worth reading


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wapi nimecreate panic .... mimi nimecoment tu.

Wanaocreate panic ni wale wanaoficha data kwa week nzima halafu wanakuja na danganya toto!! Mwambieni atoke Chato labda watu watapata amani ....!!
Kuficha data kunaleta panic!Nipe maelezo ya msingi,not nonsense yanayo onyesha kwamba ukificha data unaleta panic.Wewe umetumwa sio bure.
 
Upuuzi huu utakuisha Siku ukisikia ndugu yako kakutoka na wanaopaswa kuzika ni 10
Niambie upuuzi wangu ni upi hapo.Yaani mnatumika bila kujijua.Yaani ni kama akili zenu zimetolewa Halafu mkaingiziwa akili zingine vile....!
 
Worth reading


Sent from my iPhone using JamiiForums
Please go ahead and follow the links,they will greatly open up your mind.People are so much misinformed about C-19,that is why there is so much panic and fear and this is on purpose.The "Deep State" is creating this situation for a much bigger agenda.
 
Kuuficha ukweli ni sawa na kujaribu kulizuia jua kwa sahani ya plastiki.
Mwisho wake ni aibu.
Heshima aliyojijengea Magufuli kwa miaka minne na miezi kadhaa, yaweza kuyeyuka Ndani ya usiku mmoja na akadharaulika milele Ndani na nje ya mipaka yetu.
Kufa na Corona sio aibu, aseme ukweli
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kwanini Serikali hii ya awamu ya tano hawapendi ukweli?? Je wana miiko fulani ktk hilo?? Je ni dharau yao kwetu sisi wananchi?? Je kuna wanalofaidi kwa kuficha ukweli hata kwa jambo lisilo na maana au tija kwa Taifa??

Wanazika usiku ili iweje?? Wanaogopa nini?? Hawajui kwamba hili ni janga la Kimataifa?? Hofu yao imelenga nini hasa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaju
Kwa hii picha hata kama unataka kuthibishia umma kama watu walizikwa usiku, inaweza kutumika kama ushahidi?
Unajua wewe unaposikia neno serikali unajua ni watu fulani hv wametulia Ikulu hawako kwenye jamii. Kwa taarifa wanaoenda kuzika (serikali) ni wafanyakazi wa afya walioajiliwa na mamlaka za serikali za mitaa, ni watumishi wenzetu, wengine ni baba zetu au jirani zetu au watoto wetu au kaka zetu au mama zetu n.k wanasema wazi usiku fulani akiwa zamu kazika wangapi kwa vifo vya aina gani. Kwa hiyo ndugu usiumize sana kichwa kutetea serikali wakati haya mambo yanjulikana, watu wanachosema kinatoka humohumo serikalini. Hayo mambo ya ushahidi hatuko mahakamani hapa, watu wanatoa raw data hawasubiri zenu za kupikwa hizo.
 
Unaju
Unajua wewe unaposikia neno serikali unajua ni watu fulani hv wametulia Ikulu hawako kwenye jamii. Kwa taarifa wanaoenda kuzika (serikali) ni wafanyakazi wa afya walioajiliwa na mamlaka za serikali za mitaa, ni watumishi wenzetu, wengine ni baba zetu au jirani zetu au watoto wetu au kaka zetu au mama zetu n.k wanasema wazi usiku fulani akiwa zamu kazika wangapi kwa vifo vya aina gani. Kwa hiyo ndugu usiumize sana kichwa kutetea serikali wakati haya mambo yanjulikana, watu wanachosema kinatoka humohumo serikalini. Hayo mambo ya ushahidi hatuko mahakamani hapa, watu wanatoa raw data hawasubiri zenu za kupikwa hizo.
Mh...
 
Back
Top Bottom