Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
Umeongelea mambo mengi nje ya hoja yangu ya msingi kusema kuwa JK aende kwa umakini mkubwa, ila naomba nipingane na wewe kuwa mpaka sasa dalili nyingi za kwamba hizi ni nyakati mpya bado hazijaonekana kwenye sanduku la kura.
Ni mpaka hilo litakapotoea ndipo wanasiasa watakuwa wanawaogopa wananchi na hawa mafisadi watakuwa nao tumbo joto kwani hawataweza tena kushinda Ubunge kwa kugawa khanga na pilau.2007 & 2008 yametokea mengi lakini tukijiuliza iwapo Lowassa, Chenge, Msabaha na Karamagi wataweza kurudi tena bungeni 2010; kweli tunaweza kusema haiwezekani? Si tutatukuwa tunajidanganya?
Ndugu yangu wewe unakuwa kama sio mtanzania. Uchaguzi wetu mara nyingi unakuwa ni janja yetu ya kuwazuga watu wa nje lakini ukweli ni kuwa kura mara nyingi(sio mara zote) hazireflect will of people. Unajua kabisa kuwa NEC, udiwani,Ubunge na hata Urais ujanja mwingi sana unafanywa. Sisi ni third world country ambako baadhi ya familia ndio zina haki ya kuwa watawala na nyingine ni wasaidizi na wasindikizaji.
Kwa msingi huo pamoja na kuwa ni wachache sana watakopenda kuona Maramba, Karamagi, Lowassa, Chenge etc etc wanaendelea na siasa lakini uwezekano huo ni mkubwa, naungana na wewe kuwa wanaweza kuendelea kuwepo 2010 kama sio kwa "kuchaguliwa" hata kwa njia nyingine, au kupewa nyadhifa za juu. This is how things work around here.