First time's an accident. Second time's a coincidence. Third time's a trend!

Mchukia Fisadi kwa nini tuachane nayo hii falsafa mimi binafsi naona hii falsafa ni valid leo, kesho, keshokutwa , milele na milele. Nchi yenye utajiri kama huu what more do we need, watu tumesomeshwa angalau kidogo, std 10 mambo yalikwenda kwelikweli sasa hivi qualifications kibao hata kulima tunamuita muarabu, mkenya , MsouthAfrica , mzimbabwe jamani tumelogwa. Ukiuliza oh wawekezaji utajiri wote huu wawekezaji wa nini tunashindwa nini sisi wenyewe.

Siasa tunyoamini hivi sasa ni nini, hakuna kiongozi anayejua, katiba anasema ibara ya 3 (1) Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.https://www.jamiiforums.com/#cite_note-Cranford-2

Katiba ya chama cha mapinduzi nayo inasema kuwa imani ya CCM ni : Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru. Wakati huohuo malengo na madhumuni yao ni :Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea kwa mujibu wa Azimio la Arusha.

Sasa tujiulize viliandikwa vitabuni ndivyo vinavyofanyika? Mimi binafsi naona ni tofauti kabisa siasa ya sasa hivi ni mchanganyiko wa madudu mengi tu ambayo hayapo kwenye chama wala katiba ya nchi.

Ngambo ngali ukisoma vizuri utanielewa. Tupo wote mkuu.
 
Mkuu tatizo pia lipo kwenye WATU kwa sababu hata kama wakifika BILIONI lakini kama wamejaa uswahili na ubabaishaji kama wa kwetu sisi basi hata hao viongozi bora hatuwezi kuwapata! Lazima tuanze kubadilika kuanzia huku level ya chini...

WATU - Hili ni mama wa matatizo yote.
WATU - hutoa viongozi kwa maana ya wagombea na wenye kuchagua
WATU - Hutengeneza Siasa safi au chafu - uongozi bora au bora uongozi - RUSHWA, UBADHIRIFU,WIZI/UFISADI ETC
WATU - Hutumia rasilimali kama ardhi ili kuzalisha utajiri na pesa ( value) ambayo tuliambiwa siyo msingi wa maendeleo.

TUFANYE NINI KUWA NA WATU WENYE KUWEZA KULETA MABADILIKO CHANYA?
 
WATU - Hili ni mama wa matatizo yote.
WATU - hutoa viongozi kwa maana ya wagombea na wenye kuchagua
WATU - Hutengeneza Siasa safi au chafu - uongozi bora au bora uongozi - RUSHWA, UBADHIRIFU,WIZI/UFISADI ETC
WATU - Hutumia rasilimali kama ardhi ili kuzalisha utajiri na pesa ( value) ambayo tuliambiwa siyo msingi wa maendeleo.

TUFANYE NINI KUWA NA WATU WENYE KUWEZA KULETA MABADILIKO CHANYA?

it's a slow process and might take a generation or two.....or even three. the best way is for you as a mother or father to raise your children in the right way, teach them patriotism and love for country and bring them up in faith. If we all can do that then certainly the future is bright.
 
Back
Top Bottom