First born msichana theory.........

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Jamani nimekutana na watu wengi sana sasa wanaoamini kuwa

familia zinazoanza na first born msichana huwa zinapata bahati au baraka zaidi hasa

kwenye kipato......

Katika mazungumzo na watu....nimekuja kugundua kuwa hii imani ipo kwenye baadhi ya

jamii hasa pwani zanzibar,pemba,na jamii za wahindi pia....

Kuna dokta mmoja aliniambia yeye alipozaliwa mtoto wake wa kwanza msichana

akapata scholarship nje.....

Halafu mkewe akajifungua watoto wakiume watatu na hakusafiri tena

mpaka mkewe alipojifungua msichana tena....

Na wengine wanasema ndoa ikianza na mtoto wa kiume ni ishara ya matatizo

kwenye familia wakati wa kike ni ishara ya neema....

Swali hapa je umewahi kukutana imani hiii???????

Unalionaje hili jambo ukilinganisha na watu unaowajua
wenye watoto wa kwanza wasichana na wenye watoto wa kwanza wavulana???????
 
Mimi nawajua watanzania nawahindi wenye imani hii....
Nafikiri ni universal...........
 
Kimsingi nimeleta hapa ili watu wajadili kulinganisha na uzoefu wao.....

Swala la kweli au si kweli sio muhimu.....

Muhimu wewe una uzoefu gani kwa hili...
 
Yaanihiyo imani ipo sana,
uliza wahindi,wapemba,waunguja na wengineo..
 
<br />
<br />
sijawahi mimi naona mtoto ni mtoto tu.

mtoto ni mtoto kweli but
kuna imani mbali mbali kulingana na jamii husika....

Wanasema kwa kuwa mwanamke ndio anaezaa hiyo ni ishara
ya kuongezeka since utajiri....

Na kwa kuwa mwanaume ni mtafutaji ni isharaya
kutafuta since shida....

So ni imani za watu.....najaribu ku share tu hapa nawatu wengine
 
niliwahi kusikia ila sikuzingatia sana wala kuchunguza.

Mara kadhaa nimesikia kuwa mtoto wa kwanza akiwa msichana, ni ishara ya upendo na amani! Na nimeona watu wakiita watoto wao wa kwanza wasichana -Pendo, Upendo na majina mengine ya lugha za makabila yenye maana ya upendo.

Kuhusu utajiri na neema sijui ila ninachoweza kusema ni kwamba, mtoto wa kwanza msichana huweza kuwa msaada mkubwa sana kwa familia kama hatapatwa na mikasa kama ujauzito usiotarajiwa etc.
 
Mi kwangu hili ni jipya kabisa na I strongly refute the claim.....mtoto wa kwanza wa JK hivi ni msichana ama mvulana?
 
Back
Top Bottom