Fikra kikwazo kikubwa Tanzania


FIKRA KIKWAZO KIKUBWA TANZANIA – LEMA


Katika mambo yote yanayoonekana Duniani , kwa namna moja au nyingine yamezaliwa na uwezo wa kufikiri ama CHANYA au HASI . Na hii ndio tofauti kubwa sana kati ya Binadamu na Binadamu, Elimu tunayoiona leo imezaliwa katika FIKRA .

Hivyo basi kama kuna tatizo kubwa sana linaloikabili Dunia kwa sasa na Nchi yet ni kukosekana kwa TABIA YA FIKRA NA TAFAKARI CHANYA

Watu wengi wanafikiri Ugaidi , Uharibifu wa Mazingira , na tabia mbaya zinazoharibu Jamii ni tishio kubwa . Haya yote yanayoitwa leo majanga , yamezaliwa na FIKRA hasi katika utaratibu wa kufikiri .

Kutenga muda wa kufikiri na kutafakari ni jambo muhimu ambalo Watu wengi na Dunia imeshindwa kuliona kama msingi wa mabadiliko , lakini pengine jambo jema lingeweza kuzaliwa katika ukimya wa Tafakari na kufikir chanya .
Nimekaa Bungeni kwa kipindi nilichokaa na nimeona na pia nimejifunza Mitaani , na hivi ndivyo ninaamini “PAMOJA NA MABADILIKO YA KISIASA TUNAYOTAKA TANZANIA , MUHIMU KUELEWA KUWA TANZANIA HAIWEZI KUBADILIKA KAMA TABIA YA KUFIKIRI HAITABADILIKA KUTOKA KATIKA MTAZAMO HASI KWENDA MTAZAMO CHANYA”


Watu wengi wanafikiri na wanataka kuona matokeo makubwa ya mabadiliko ya Utawala mwaka huu , hata Mimi nafikiri hivyo, lakini Mimi ninatambua mabadiliko ya Mtanzania ya msingi ni “ KUBADILI FIKRA KUTOKA MTAZAMO HASI KWENDA CHANYA “ Tanzania itabadilika kama Watu watabadilika kufikiri , ni jambo kubwa sana hili lakini wapumbavu hawawezi kuelewa .

Tatizo kubwa sana la msingi la Nchi hii sio uwezo wa Elimu wa Taifa letu bali ni uwezo wa FIKRA za Watu wetu, ndio maana hata Mataifa mengine ya Afrika kama Nigeria , South Afrika yenye vyuo vikuu vingi na Taasisi nyingi za Elimu bado yameshindwa kuthibitisha uwezo wao katika mambo mbali mbali muhimu . Ulaya na Amerika pia wameshindwa kuthibitisha uwezo wao kwenye baadhi ya mambo yaliokosa FIKRA CHANYA , ndio maana leo katika ukuaji wao wa demokrasia wanafikiri Mwanaume kufunga ndoa na Mwanaume mwenzake ni jambo linalotuk misingi ya haki , usawa na demokrasia

Vita dhidi ya Umasikini , Maradhi na Ujinga ni vita inayohusu FIKRA zaidi kuliko Siasa , Siasa inayoharibu Utawala bora ni Uongozi uliokosa FIKRA CHANYA .

Matumaini makubwa ya Watu ni kuwa, mfumo wa demokrasia wa Vyama vingi utabadili maisha yao , ni kweli unaweza , lakini Mfumo wa Tabia ya FIKRA kutoka FIKRA hasi kwenda CHANYA utasaidia mfumo wa demokrasia wa vyama vingi kuwa muhimu zaidi katika mabadiliko ya Taifa.

Kushinda Uchaguzi na Kutawala ni jambo moja , Kutawala katika FIKRA CHANYA ni jambo jingine na muhimu zaidi . Kiongozi yeyote anayetaka kuleta mabadiliko katika Taifa lake ni lazima ajue umuhimu wa hiki ninachokieleza


Wakati Fulani namtafakari John. F. Kennedy , pindi alipopewa proposal ya Watu kutaka kwenda mwezini kufanya utafiti , jambo hili halikuwa raisi hata kidogo ,lakini ni nini kilimfanya aamini kuwa utafiti na jambo hili vinawezekana ? ni uwezo wa kuwa na FIKRA CHANYA. Hivyo basi hakika waliopaswa kubadilisha mtazamo wa FIKRA ni Viongozi kwa mienendo yao , Kauli zao ,Matendo yao na uwezo wao katika maamuzi , ndio maana ninasema “ PAMOJA NA MABADILIKO YA KISIASA TUNAYOTAKA TANZANIA , MUHIMU KUELEWA KUWA TANZANIA HAIWEZI KUBADILIKA KAMA TABIA YA KUFIKIRI HAITABADILIKA KUTOKA KATIKA MTAZAMO HASI KWENDA MTAZAMO CHANYA”


Wakati Mabunge ya wenzetu yanajadili uwezekano wa Binadamu kuishi Sayari ya Mars , sisi kwetu kwa miaka 54 ya Uhuru tunajadili Kujenga vyoo shule za msingi .


Hatuwezi kubadili Nchi hii bila kubadili namna tunavyofikiria ,
Umasikini wa Nchi unasabibishwa na uzembe mkubwa katka FIKRA kuliko ukosefu wa mitaji , ndio maana sehemu kama Mwanza ambako Maji yamezunguka Mji bado Maji ni tatizo kwenye makazi ya Watu.

Hatuwezi kubadili Nchi hii bila kubadili namna tunavyofikiria ,
ndio maana sehemu kama Singida na Same maeneo yenye Upepo mkali , Tanzania inaona ajali na kutoa tahadhari , lakini kumbe ni Umeme unapotea bila maamuzi .

Hatuwezi kubadili Nchi hii bila kubadili namana tunavyofikiria ,
kinyesi cha binadamu kinapomwaga panaitwa Bwaa la maji machafu (Mavi) , lakini kwa wenzetu wenye FIKRA CHANYA ni Kiwanda cha kutengeneza gesi na mbolea .

Hatuwezi kubadili Nchi hii bila kubadili namana tunavyofikiria ,
sehemu za Dodoma na Tabora na Singida zenye jua kali wakati mwingi kwa mwaka , Nchi yetu inalalamika ukame katika maeneo haya , ingekuwa ni Nchi kama Israel wangezalisha umeme wa Jua ( SOLAR VILLAGE ) na kuweza kuingiza kwenye Umeme wa Taifa na kusaidia kunguza gharama kali za maisha .

Hatuwezi kubadili Nchi hii bila kubadili namana tunavyofikiria ,
wakati Nchi nyingine Viongozi anachaguliwa kwa sifa na uadilifu hapa kwetu Viongozi wanachaguliwa kwa rushwa na fedha , hili ni jambo la kawaida sana na hakuna anayeshangaa tena , tabia zimekuwa za ajabu, Nchi hii kuishi nje ya mfumo wa rushwa ni jambo lisilowezekana na ni jambo la hatari kama utajaribu kwani ndio mfumo unaofanya kazi katika sekta zote kuliko ule mfumo uliokusudiwa katika utawala wa Nchi.

Tumefika mahali katika Nchi hii mfumo wa rushwa na wizi ni halali kila mahali katika ofisi za Serikali na binafsi na
ndio maana hata ukihudumiwa mahali fulani ,hata bila kuombwa rushwa bado unafikiri ni muhimu kushukuru kwa njia ya pesa .

Dreva Taxi akikupakia wakati anakuomba malipo , atakuuliza niandike kiasi gani ? au nikupe risti utaandikia mwenyewe ? hizi ni fikra za uhalifu wa rushwa


Kuna tatizo kubwa , Askari wa usalama barabarani anapotumwa kukusanya mapato huwezi kutarajia uadilifu wake katika kukemea uzembe barabarani ili kuepusha majanga ya ajali bali makosa kwake ni chanzo cha mapato kama alivyoagizwa na Wakuu wake . Huu ni uhalifu wa FIKRA

Hili ni Taifa ambalo Vijana wengi ambao wanafikiri wanamaisha ya kati wanashinda Bar muda mwingi kuliko nyumbani na Familia zao wakijadili ngono na pombe na kufurahia anasa . Hii ni Nchi ina umasikini mkubwa wa fikra na ndio tatizo kubwa sana la umasikini wa mwili.

Hili ni Taifa ambalo muda kwake sio kitu cha thamani , unapanga na Mtu mkutane saa kumi jioni na yeye anaona sawa kuja saa moja jioni masaa matatu baadae , wewe unayemsubiri hauoni kama ni shida na yeye wala haoni kama kuna mahali amekosea .
Hili ni Taifa ambalo unaweza kuwa Rais kwa kuandikwa kwenye magazeti sana na mitandao mbali mbali ya kijamii hata kama una sifa .

Hili ni Taifa ambalo kuna wakati demokrasi inakuwa na akili kuliko maadili , hata kama hufai kuwa Kiongozi lakini umetengeneza mbinu za demokrasi kukupigia makofi basi hata wale wanaosimamia demokrasia watashindwa kufanya maamuzi kwa sababu demokrasia ina akili kuliko wao na maadili kwao ni upuuzi.
Hata hivyo yako mengi yanayoleta mashaka ya FIKRA CHANYA katika Taifa letu , huwezi kuandika yote pengine unahitaji kitabu kikubwa zaidi .

Mimi ndio sababu ninasema “ PAMOJA NA MABADILIKO YA KISIASA TUNAYOTAKA TANZANIA NI MUHIMU KUELEWA KUWA TANZANIA HAIWEZI KUBADILIKA KAMA TABIA YA KUFIKIRI YA HAITABADILIKA KUTOKA KATIKA MTAZAMO HASI KWENDA MTAZAMO CHANYA”

GODBLESS LEMA(MB) 2015-2020

Ni kweli, sisi kama taifa kwenye ile dhana ya umoja wa kitaifa hatujawekeza vizuri katika elimu tafakuri. Vilvile hata huko vyuoni na mashuleni wanafunzi wanashinda njaa hivyo ni dhahiri hawawezi kujikita katika elimu tafakuri.
 
Siku zote ninaamini Lema ni kati ya watu wenye upeo mkubwa wa kufikiri. Anastahili kuwa kwenye baraza la mawaziri la UKAWA.
 
Hivi hii tarehe 30 mwezi huu pale Amri Abeid kwenye jiji kuu la mapinduzi kuanzia azimio la Arusha hadi mapinduzi ya kuing'oa CCM inawezekanaje? ......nasubiri nchi kusimama kutokea jiji kuu la mapinduzi kama tunavyohaidiwa ........
 
Ni ngumu kutegemea embe kutoka mnazini, "so far thinking na actual living" ya viongozi wa kisiasa inafanana saana tu ukiondoa matamshi yao . . . . . .

Control your ambitions. . . . . .
Mkuu jaribu kutafakari japo kidogo ccm wanatupeleka wapi kwanza
 
ni ukweli mtupu kiongozi. mimi naongezea kwa kuomba MUNGU atusaidie vinginevyo hapa tulipokwama hatuwezi kutoka hata AKILNGOZA NANI.
 
Lema bwana umenichesha sana pale uliposema "Hili ni Taifa ambalo vijana wengi ambao wanafikiri wana maisha ya kati wanashinda Bar muda mwingi kuliko nyumbani na familia zao wakijadili ngono na pombe na kufurahia anasa" Kwa tabia hizi ndiyo maana Waswahili huwa hatuwezi kuishi katika ndoa na wazungu!

On a serious note to change the society from negative to positive thinking it is a slow process.

Sasa inatokea je, through education, you need first to empower the society through education.

But that is not enough, you need also to have committed leadership with clear vision and mission.

Tanzania we are lucking both, appropriate education and committed leadership! That is why we are doomed.
 
Mkuu jaribu kutafakari japo kidogo ccm wanatupeleka wapi kwanza

Natafakari sana ndio maana nasema kwa sasa tofauti yao "actual life" ni ndogo sana. . . . kama tunakopelekwa siko haimaanishi tuchukue dereva mwingine bila tahadhari na upembuzi. . . . .

So far tofauti zao ni zipi??!!!
Fikra ya mtu huonekana dhahiri kwa matendo yake kimaisha. . . .
 
Nakubaliana kwa kiwango kikubwa na Mh. Lema. Ni kweli kabisa ni watu wachache katika nchi hii wanaotenga muda wao kufikiri mambo. Wakati mwingine huwa najiuliza hivi ktk nchi yetu tuna think tank kweli? Tumeshindwa hata kutambua kwamba nchi za wenzetu zimeendelea through thinking critically and investing in technology.

Kama tukiendelea na uzembe wa kufikiri hatutaondoa umaskini.
 
kuna uzi wa Mwanakijiji ulikuwa hapa alikuwa anauliza tunataka mmojawapo wa walewale tuliowazoea atakayekuja na mambo yaleyale walioshindwa kuyafanya au tunataka wapya kabisa ambao wataingia na mambo mapya kabisa,
Mh Lema nataka ujuwe kwamba nchi yetu ni ya kuonea huruma kwa sababu Wenye nchi yao yaani Watanzania bado sana kujitambua,na hilo swala la fikra wasomi wa vyuo vikuu ndiyo wangeweza kutupa jibu lakini nao fikra zao ni za hovyo kuliko wale ambao hawakwenda huko,nchi hii inaitaji msukosuko kidogo ili tuweze kushtuka la sivyo tutabaki hapa hapa tulipokwama miaka mingine ishirini ijayo,Mh Lema vipi kuhusu tume huru ya uchaguzi je mmeamua kutupeleka tena kwenye uchaguzi utakaosimamiwa na ccm??mnajiamini nini hasa mpaka mkubali kufika hatua kama hiyo,kwa nini tusipambane muda huu mfupi uliobaki tuachane na katiba mpya tupigie kelele tume mpya ya uachaguzi?maumivu ya tume ya ccm ya uchaguzi anayajua Mh Mbowe tulivyopambana na kufunga barabara ya Arusha Moshi kushinikiza mkurugenzi atangaze Mbowe kashinda Hai,kwa kweli mimi bado natafakari tunakoelekea miaka mingine mitano ya kutawaliwa na ccm
 
Back
Top Bottom