hivi kwenye shamba la michikichi kuna utaratibu gani wa malipo ya fidia kwenye mazao yaliyokuwa shambani. nina shamba la michikichi ambalo serikali wamekuja kupima viwanja lakini kuna michikichi ya kimo mbali mbali kuanzia michanga mpaka iliyozeeka sasa sijui ni namna gani ya fidia kulingana na umri wa miti ya michikichi au yote inalipwa sawa tu.