Female financial economics! Jinsi wanawake tunavoteketeza mamillion kwenye vitu visivyo na tija!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,116
IGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wanawake wengi haswaa wa mjini, tena tunaofanya kazi , na kupenda kwenda na wakati kimjini mjini mishahara yetu HAIONEKANI! Unaweza hisi umetupiwa chuma ulete! Kumbe walaa wenyewe tu!

Si jambo la kushtua wala kushangaza kukuta mkaka mmeajiriwa wote mnalipwa 400,000 kwa mwezi, ila mkaka ana kijumba Mbezi Luis na mkopo wa gari anakaribia kuumaliza, ana mke, watoto na ndugu kibaoooo, na anaishi maisha mazuri tu. Ila wewe bi dada mwenzangu na mie umeolewa pesa yako ni yako ama hujaolewa umepanga zako, miaka nenda rudi huna kitu chochote to show that you worked and invested. Holaaaaaaa! Mimi nilivojiriwa fresh from school nilikuta watu wan 5 to 6 years kazini haswaa wadada ila hawana cha kuonesha pamoja na mshahara na vibuzi vyote! Ila wakaka hela hio hio wamejenga, wengine hadi nyumba 2. 3 years na mimi nimejikuta in similar situation! Ndo nilipojiundia jopo la kujichunguza Pesa yangu inaenda wapi? Nikaanzisha DAFTARI/DIARY!!!!!!!!!

Hamaaaaaad! Laki si pesa millioni deni! Kila nachonunua naandika afu mwisho wa mwezi nikajumlisha! Mmmmmmmh! Usitake hata kujua outcome coz ni mambo ya aibu! Ila nimegundua wadada wengi pesa inaishia huku

Nguo, Viatu, Mipochi, Perfume Vipodozi!!!!!!!! Ile zana coz unafanya kazi unakuwa obsessed kuvaa vitu vya ukweli daily, midosho na supra za kariakoo za bei chee huzitaki ndo pesa inakomalizikia. Saivi pamba claassic za town gown 50,000- 80,000, viatu ni 40,000-70,000, suruali na skirt kwenye 20,000/=, mipochi imesimamia 50,000 mpaka 150,000, perfume designer feki original zinasimamia 70,000 mpaka 150,000. Yaani laki si pesa million deni! Ukijilipua shopping kuteketeza 300,000 sio ishu, sasa hapo si kimshahara kimeisha!!!? Afu trend hazidumu, nguo ikakaa kidogo inaisha fashion inabidi uanze upya ku update closet ama wardrobe yako. Ndo mwaka unaisha unafanya kazi ya kufukuza upepo wa fashion!

Kumaintain Class fake ile mtu unakuwa matawi ya juu. Wanaume hawana hizi. Lunch wanatafuta cheapest wanakula lunch, ila sie sasa kazi ipo! Lazima ule sehemu yenye hadhi kidogo! Sasa pale unaacha 8000 hadi 10000 kila mchana! Matoke katikati ya mwezi diet inaanza, mwishoni inaisha! Hapo coz unakula juu unajiona wa maana kinoma unasahau wanaokula vichochoroni wana nyumba 2 wakati mie banda sina! Usipite mchango wa harusi usichange! Simu gani ikupite? Birthday lazima ushushe party la nguvu! In the end 5 years kazini nothing to show for it. Budget ili usave ndo new agenda!

Kutoa pesa ovyo na ukarimu kupitliza! Wanaume pesa yao haitoki ovyo ovyo ni kwa mahesabu, ila wadada sasa, mtu akikuomba ushamkirimia 20, mdogo wako akikupiga kizinga umemkirimia msimbazi, bi mkubwa akikohoa umezama kwenye wallet. Sherehe ukialikwa ushazama kwa mchango na zawadi, kuterat marafiki weekend, kufanya mabo ambayo pesa inatoka hakuna inachoingiza! Matokeao yake wale uliwakirimia wanaanza flani hamna kitu pale, unaona mdogo wake keshajenga, huyo dogo hawapi hata kumi.

All in all wadada tuna spending issues! Yaani unashika hela ila haionekani, it better tukajifunza bajeti kali kama wenzetu. Mwnaume nguo alizo nazo hakuna inayozidi, zote zinavaliwa, ila sisi nguo hujaivaa miezi 3 na bado unanunua! Viatu pair 50!!!!!!! Hadi unaulizwa hivi vote unavaa? Tuwaze uzee wajameni! Ujana maji ya moto! Tuinvest tuishi kwa amani. Kazi za watu hizi zinaisha any time.
 
hii si ungeipost kule lara 1 naona kama ina mahadhi ya kule kwetu songea

ila uliyosema yote ni kweli tupu, tatizo ni kukubali kuachana nayo, ukubali kuwa uko matawi ya chini, ukubali kusemwa kuwa umefulia, ukubali kuwa sitaki attention ya watu ninapoonekana mahali, ukubali kuishi kama wewe na siyo kuendeshwa na hisia za watu. Je, ni wanawake wangapi wako tayari kuwa hivyo?
 
Last edited by a moderator:
Yaani mpendwa umenigusa mimi nafikiri na wengine pia ila nilishajitambua kitambo kidogo, yaani kuna siku nilitumia 1m kwenye viatu,wigs na body lotion sasa kasheshe hayo mafuta ya ngozi yakaniaribujeeee nikaikumbuka Dove body lotion yangu na kujuta juu!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
ime2lia sana, big up endelea kutupatia somo nimeipenda na tupo wengimambo yangu poa sana rafiki zangu wananicheka kuwa siendi saloon yaani outdate lakini na watoto wawl wanasoma shule nzr na kajumba kangu, house girl wangu yuko poa over ninamwanaume nina
 
Hivi lara umewahi kufikiria kuandika kitabu au kuwa na blog yako au hata kuandika kama makala na kuiweka gazetini?!
Hii ni bonge la intellect.
Am sure Shigongo akisoma vitu unavopost lazima akutake part time.
What I mean ni kwamba una kipaji cha uandishi. Anybody can have the same material you have but how to present it in attractive manner mpaka nivutike kusoma mwanzo mwisho bila kuwa bored ndo issue.
 
Nimeona aibu kama unanisema mimi, au unanijua nini ndio unanipa vijembe vya live live?
sijui nianzie wapi kujirekebisha maana najiona too late
 
mwanamke lazima upendeze lakini utapendezaje sasa kama stress ya kufikiria pesa inakuletea makunyanzi usoni. hebu jiulize kabla haujanunuachochote ambacho unacho tena na vingine haujawahi tumia kwa miaka kadhaa sasa do I really need this item? kama hauhitaji just dont buy it hakuna haja ya kuwa na pochi 30 wakati mwaka umeisha haujabeba hata nusu yake. au una kiatu mara ya mwisho kukivaa ilikuwa kwenye harusi ya fulani. hailipi hata kidogo.

Ask yourself this question kazi ikiisha leo unaweza kuishi muda gani bila kuwa na kazi? cha muhimu hapa ni kuweka akiba tu sio kutumia kila shilingi mdada unayoipata.
 
MI YANGU INAISHIA KUNUNUA MAVITU VYA JIKONI!mwe!\
aibu yangu aibu yangu!
yani hakuna kitu kinakula hela yangu kama shopping ya jikoni!cha
sijui nafanyaje walahi!
 
Am happy sijawahi kupitia hili, natizama bajeti kwa darubuni kali sana.

Ila ni kweli kabisa, baadhi ya wanawake/wasichana hawafanyi uwekezaji wala uwekaji wa pesa. Labda kutokana na ile dhana kwamba hawana majukumu makubwa ya kulea familia, majukumu haya ni ya wanamme.
 
lara 1, sio wadada tu.. Wanaume wa kizazi hiki ndio balaa.. Swala la kujenga hadi mwanamke aje akukomalie ndio unakaa sawa.. Usiombe ukutane na mwanamke kama wewe unaemuongelea hapo ndio mshakufa masikini

Kuna mkaka najuana nae anafanya benk moja tu ya kigeni salary ya kawaida sana kama 1m net,,

Sasa amekopa hela kanunua OPA anakatwa kama 350,000 kwa kulipia deni.. Pia amepanga nyumba 250,000 tena nje ya mji huko sema ye karidhika kisa nyumba kali,, kila siku kwenda kazini anatumia mafuta 10,000 so kwa mwezi kama laki 3 hivi ndio budget ya mafuta..

Bado sijampigia budget yake ya chakula kuanzia asubuh, mchana na jioni..

Jamaa alimaliza mbele yetu ana miaka kazaa ofisini lakini hasomeki kabisa,

Ukimwambia swala la kutafuta mwenza na kuoa anaogopa huyo eti maisha magumu, wakati yeye mwenyewe kayafanya magumu..

Ndio starehe muhimu lakini lazima ujiangalie na mbele itakuaje..

Mimi nina principle moja, hela yeyote nikiipata tofauti na mshahara, ni pamba, na good time, maana sikuitegemea..

Hela ya mshahara yote ipo budgeted kabla hata haijapokelewa imeshaisha..
 
Last edited by a moderator:
lara 1 unamsema mkewangu nini? Ngoja nimforwadie link kwenye fb wall yake...
 
Last edited by a moderator:
Kabla sijapata watoto nilikuwa nafanya spending ya ajabu, when the children came nilifikiria mara mbili mbili nikajikuta naanza kusave kidogo kidogo sio kwamba I have neglected myself, nimekuwa na priorities tu.

Na kama ningejua ningeanza kusave mapema kipindi hicho nikiwa na 0 majukumu ningekuwa mbali sana. So gilrs start early na ukizoea haitakuwa ngumu.
 
lara 1, sio wadada tu.. Wanaume wa kizazi hiki ndio balaa.. Swala la kujenga hadi mwanamke aje akukomalie ndio unakaa sawa.. Usiombe ukutane na mwanamke kama wewe unaemuongelea hapo ndio mshakufa masikini

Kuna mkaka najuana nae anafanya benk moja tu ya kigeni salary ya kawaida sana kama 1m net,,

Sasa amekopa hela kanunua OPA anakatwa kama 350,000 kwa kulipia deni.. Pia amepanga nyumba 250,000 tena nje ya mji huko sema ye karidhika kisa nyumba kali,, kila siku kwenda kazini anatumia mafuta 10,000 so kwa mwezi kama laki 3 hivi ndio budget ya mafuta..

Bado sijampigia budget yake ya chakula kuanzia asubuh, mchana na jioni..

Jamaa alimaliza mbele yetu ana miaka kazaa ofisini lakini hasomeki kabisa,

Ukimwambia swala la kutafuta mwenza na kuoa anaogopa huyo eti maisha magumu, wakati yeye mwenyewe kayafanya magumu..

Ndio starehe muhimu lakini lazima ujiangalie na mbele itakuaje..

Mimi nina principle moja, hela yeyote nikiipata tofauti na mshahara, ni pamba, na good time, maana sikuitegemea..

Hela ya mshahara yote ipo budgeted kabla hata haijapokelewa imeshaisha..

hii sasa ni kufuatilia maisha ya watu.
 
Duuh!!umelenga mulemule ni hatari hapa wengine salary zinakata kabla hata hatujaugawa mwezi.mie nimejifunza thru my bros ni wakali hasa kutoa hela yani mpaka imtoke hapo ni kazi haswaa.ukijifanya kuweka kajidiary kuandika wat u spent unaweza dondoka kwa presha cha kufanya ni kuhakikisha unagawa salary kama ndio hiyo unayoitegemea tu unahakikisha unanunua matumizi muhimu ya mwezi basi inayobaki ndo unaisave..!!!!ila hakikisha unajifunza displin ya hela vinginevyoo chalii back to square one..!!!
 
lara 1 uwe unaposti kwa kiswahili tutakuelewa tu
 
Last edited by a moderator:
Thank u lara. Ni vizur kukumbushana hasa kwa masuala ya msing kama haya. Wanawake wa type hiyo tubadilike
 
Kuna shosti wetu ye kazi yake kubwa ni kushinda kupiga pamba, natamani angeiona hii!
 
wewe Lara 1 acha wadada wapendeze. kama ela tutawapa. wewe unataka hivo viatu na mawigs wavae kina nani.

acha wadada wapendeze
 
Back
Top Bottom