Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Tangu asubuhi TBC imekuwa ikitangaza ya kwamba ujumbe wa Tanzania upo Uingereza kufuatia fidia ya malipo ya rada.
Kwa kumbu kumbu zangu hii si mara ya kwanza kwa waziri Membe kutuma ujumbe wa aina hiyo huko uigereza kwaajili ya malipo husika. Suala la kujiuliza ni kwamba kama Membe mwenyewe alikwisha wasilisha suala hilo kwa serikali ya uingereza kwa kupitia waziri wa nje mwenzake wa nchi hiyo, anawezaje tena kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na kampuni husika!
Diplomasia ya aina hiyo aliiona wapi?
Swali lingine kwanini wakati habari zilipoanza kuvuja ya kwamba Tanzania iliuziwa rada kwa bei mbaya, mbona hakuwa anajishugulisha kutoa ushirikiano wake katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo, iweje sasa wakati mambo yamekamilika awe mwepesi kutaka kuvuna asikopanda.
Katika hali halisi kukaa kimya kwa serikali ya Tanzania wakati suala hili linafanyiwa uchunguzi kumeiondolea uhalali wowote wa kudai tuzo iliyotolewa kwa suala hilo. Hivyo wahusika wana haki ya kuunda chombo chao kitakachobuni njia muafaka wa kufikisha tuzo hiyo kwa walengwa ambao ni watanzania.
Katika hali hiyo ni matumizi mabaya ya fedha za umma kuendelea kuingia gharama za mara kwa mara kwaajili ya kwenda uingereza eti kufuatilia malipo hayo wakati tuna ubalozi huko.
===================
KATIKA PICHA:
Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.) akiongea na Naibu Spika wa Bunge la uingereza, Mhe. Nigel Evans (Mb) katikati ni Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania. Ujumbe wa Wabunge wanne wa Tanzania unaongozwa na Naibu spika. (Picha Assah Mwambene)
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiteta jambo na Spika wa Bunge la Kenya walipokutana katika Bunge la Uingereza jana. Waheshimiwa Wabunge wako nchini Uingereza kufuatilia malipo ya zaidi ya paundi milioni 29 kutoka BAE System baada ya Mahakama nchini hapa kuiamuru kampuni hiyo kuilipa Tanzania baada ya kugumdulika kwamba kampuni hiyo iliongeza bei ya ununuzi wa Radar.
Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheheshimiwa Peter Kallaghe akiteta jambo na Waheshimiwa Wabunge wa Tanzania, Jobu Ndugai (Naibu Spika), Mussa Azzan Zungu (Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mhe. Angela Kairuki