FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998. Hata kama huwapendi wamarekani, basi tuwaheshimu tu

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,082
36,018
Huyu Bwana yuko zake Kimara Bucha kwenye kasri au tuite hekalu lake mithili ya ikulu ndogo ya Singida, anakula bata huku akilea wajukuu, ameshazeeka sasa.

Yeye na kizazi chake walipigwa ban wasikanyage USA wala kusogelea ubalazi wao.

Wakati ubalozi wa Marekani unalipuliwa nchini pamoja na Nairobi Kenya, polisi na wapelelezi wetu wakaanza kukamatakamta watu ovyo eti ni washukiwa, watu wasiopungua 200 walikuwa shimoni kule Central Police, DSM.

FBI wakapata taharifa kuwa kuna suspects wamekamatwa wako central, wakaomba kuwaona. Kufika kule wakawaambia polisi wa bongo kuwa waachieni wote hakuna suspect hapa, hakuna gaidi anavaa yeboyebo amepauka kwa njaa, hawa ni vibaka tu, IGP akaambiwa u know anything about terrorism?

Jamaa wakaingia chimbo wakaomba akaunti za wafanyabiashara na vionhozi wote wa kisiasa na wanaharakati ambao wameingiziwa mpunga mrefu ndani ya miezi kadhaa (sikumbuki) Thomas Lyimo mfanyabiashara aliyekuwa na garage yake Kimara bucha na vibanda vya maziwa Dar nzima enzi hizo akajikuta matatani, ni baada ya kuonekana akaunti yake iliingiziwa pesa hazina maelezo, kipindi hicho sheria ya money laundering haijatungwa.

Kufustilia kwa kina ni kweli bomu lililolipua ubalozi liliunganishiwa kimara kwenye garage yake.

Hayo yakifanyika mastermind alikuwa kijana mdogo toka Zanzibar Ahmed Khalfan Ghailan, mshirika wa Alqaeda ambaye baadae anakuja kuwa mtu wa karibu kabisa na Osama Bin Laden, kijana huyu ndie alimuingizia huo mpunga kabla ya kukimbilia Nairobi na uarabuni. Alikuwa kijana mfogo tu wa miaka 24 au 25, kwa sasa bwana Ghailan ni mtu mzima sasa anakaribia miaka 50 yuko Guantanamo Bay Camp chini ya ilinzi mkali.

Huwapendi USA ila una vingi vya kujifunza kwao

Soma pia:

1) Kwa Thomas - Kimara bucha

2) Kwa Thomas - Kimara bucha

3) Kwa Thomas - Kimara bucha

4) Kwa Thomas - Kimara bucha

5) Kwa Thomas - Kimara bucha

6) Kwa Thomas - Kimara bucha

7) Kwa Thomas - Kimara bucha

8) Kwa Thomas - Kimara bucha
 
Madai ya anti Us ni kwamba wanapinga Dhuruma za Us.. Sasa huyu bwana dogo Ahmed Ghailan alidhurumiwa nini na US hadi kwenda kuua watu ubalozi wao.
Wale jamaa wa kibiti wangelichekewa Tanzania ingelikuwa na akina Shekeu wengine.
Ahmed Ghailan alikuwa ni mtumishi au agent wa Alqaeda,so alikuwa kazini,ameshiriki mission nyingi mpaka kuja kudakwa.
Kuna wakati alikuwa bodyguard wa Osama kwa mujibu wa FBI
 
New York

JINSI MTUHUMIWA ALIVYONASWA

Makabrasha ya ushahidi uliowakilishwa mbele ya korti na waendesha mashataka wa U.S. Attorney for the Southern District of New York kesi ya Ahmed Khalfan Ghailani

Gari aina ya Nissan truck ya kijapani ya mvuvi wa pweza pwani ya bahari ya Hindi mwambao wa mashariki ya Tanzania karibu na jiji la Dar es Salaam, gari iliyokuwa na mfumo wa barafu kutunza mazao ya uvuvi yasiharibike ilinunuliwa kwa noti za Marekani cash zilizochoka kisha lilipelekwa gereji Kimara nje kidogo ya jiji kufanyiwa modification kwa ajili ya kuongeza chumba maalum kuweka cylinders/ mitungi ya gesi, TNT, oxygen, fertiliser n.k bila mwenye gereji wala mwenye biashara ya uvuvi kujua njama hizo.

Mtuhumiwa Ahmed Khalfan Ghailani alikuwa akitumia usafiri wa baiskeli kusafiri toka kwenye nyumba kitongoji cha Magomeni kwenda mjini na kurudi kwa ajili ya mipango yake miovu.

Mtuhumiwa alikuwa anajivika hali ya muonekano wa fukura mwenye unyonge kila akiwasili na baiskeli yake ktk hoteli moja alipokuwa akikutana na aliowaita wageni zake waliokula njama naye.

Picha ya unyonge aliyojivika Ahmed Khalfan Ghailani ni kila mara kusisitiza kuwaambia mlinzi na watu waliokaa kijiweni nje ya hoteli kumtizamia baiskeli yake iliyochoka aliyoacha nje isiibiwe na vibaka wa Mnazi Mmoja DSM

FBI walifika baadaye baada ya tukio na kuipata nyumba iliyokuwa inatumika kutengeneza vilipuzi. FBI waliondoka na mazulia pamoja na rangi iliyokwangulia toka vyumba vya nyumba ya Magomeni. Vitu hivyo viliyokuwa na mabaki ya kemikali hivyo vyote vikuwa ni sehemu ya vithibiti vya uhusika njama hiyo mbaya ovu.

WaTanzania kadhaa wasio na hatia lakini walikumbana na wapanga njama bila kujua walichukuliwa mpaka Marekani kutoa ushahidi upande wa mwendesha mashtaka wa Marekani kuhusu tukio hilo baya la ugaidi.

Kesi hii imehifadhiwa mtandaoni na waweza kuisoma yenye mamia ya kurasa ili kuweza kuona umahiri wa uchunguzi uliofanyika na hatimaye Ghailani kukamatwa Afrika ya Kusini akiwa na kazi ya mkanda unga wa ngano katika bekari moja ya kuoka mikate mjini Cape Town, Afrika ya kusini baada ya kukimbilia huko.....

Maafisa wa FBI walifika mjini Cape Town South Africa ofisi ya uhamiaji baada ya fununu kutoka wasiri wao kuwa wafike kuomba kupatiwa majina ya watu waliowasili kuomba ukaazi au ukimbizi kabla kidogo na baada ya August 1998 ndipo waliona alama za dole gumba zinazoshabiana na zilizochukuliwa ktk nyumba ya Magomeni DSM, hoteli ya Mnazi Mmoja pia sehemu zingine na picha ya mtuhumiwa akiwa amejiandikisha ukimbizi kwa jina la bandia kwa ajili ya kupatiwa hadhi ya ukimbizi wa kisiasa ....

FBI wakaambiwa wamsubiri atafika kuripoti ofisi ya uhamiaji ya Afrika ya Kusini kama yalivyo masharti ya wanaoomba hifadhi kuwa lazima kila mwezi wawe wanaripoti ili waendelee kutafutiwa hifadhi ya kudumu waliyoomba ya ukimbizi.

Siku ya miadi ya kuripoti Ghailani alifika ofisi za uhamiaji Cape Town na kuzuiliwa na vyombo vya usalama vya Afrika ya Kusini na kuanza kuhojiwa kwanini ametumia jina bandia huku pia vyombo vya usalama vya Marekani maofisa wao wakisikiliza utetezi za Ghailani

Alipobaini kuwa maji yapo shingoni South Afrika, Ghailani alijaribu kutumia mfumo wa haki jinai (criminal justice system) wa Afrika ya Kusini asisombwe kwa deportation kwenda Marekani kusomewa mashtaka yake , hata hivyo ilishindikana na hivyo akapakiwa ktk ndege baada ya kurupushani za wanasheria ktk korti za Afrika ya Kusini ... soma hapa :
Justia Law
https://law.justia.com › district-courts
United States v. Bin Laden, 156 F. Supp. 2d 359 (S.D.N.Y. 2001)

Even the extradition treaty in force at the time of the arrest and deportation of Khalfan Mohamed did not allow the South African.....



New York

Ahmed Khalfan Ghailani Found Guilty in Manhattan Federal Court of Conspiring in the 1998 Destruction of United States Embassies in East Africa Resulting in Death​

Al Qaeda Terrorist and First Guantanamo Detainee to be Tried in Civilian Court Faces Possible Life Sentence in January​

U.S. Attorney’s OfficeNovember 17, 2010
  • Southern District of New York(212) 637-2600

U.S. Attorney for the Southern District of New York Preet Bharara announced that Ahmed Khalfan Ghailani was found guilty today for his role in the 1998 bombings of the U.S. Embassies in Kenya and Tanzania that took the lives of 224 people, including 12 Americans.

Ghailani, 36, a Tanzanian national, and the first detainee held at the Guantanamo Bay Naval Base in Cuba to be tried in a civilian court, was found guilty of conspiring to destroy property and buildings of the United States, following a five-week trial before U.S. District Judge Lewis A. Kaplan.

Ghailani faces a mandatory minimum sentence of 20 years in prison and a maximum sentence of life on this count. Ghailani was acquitted of the remaining counts against him.
“Ahmed Ghailani was today convicted of conspiring in the 1998 destruction of the United States Embassies in Kenya and Tanzania, causing death as a result,” said U.S. Attorney Preet Bharara. “He will face, and we will seek, the maximum sentence of life without parole when he is sentenced in January.

I want to express my deep appreciation for the unflagging commitment, dedication and talent of the agents who so thoroughly investigated this case and the prosecutors who so ably tried it.”

According to the evidence presented at trial, previous court proceedings in this case, and documents filed in Manhattan federal court:
Ghailani was first indicted on Dec.16, 1998, by a federal grand jury in the Southern District of New York. In that indictment and subsequent superseding indictments, Ghailani was charged with conspiring with Usama Bin Laden and other members of al Qaeda to kill American nationals and with several related crimes in connection with the twin bombings of Aug. 7, 1998, that destroyed the American Embassies in Nairobi, Kenya and Dar es Salaam, Tanzania.

Ghailani was also charged with 224 individual murder counts for each of the victims of the two embassy bombings.

The evidence at trial showed, among other things, that each of the embassies was attacked by suicide bombers driving large truck bombs packed with approximately 1,000 pounds of TNT. Ghailani purchased the truck as well as tanks of oxygen and acetylene gas that were used in the bombing of the U.S. Embassy in Tanzania. He also stored explosive detonators that were used in the bomb at his residence.

The evidence also showed that the day before the bombings, using a fake passport in an assumed name, Ghailani flew from Nairobi, Kenya to Pakistan in a coordinated escape from Africa. Two other al Qaeda operatives, a senior operations leader and an explosives expert who had traveled between Kenya and Tanzania in the weeks before the bombings departed Africa for Pakistan on the same flight as Ghailani. Those operatives were also involved with the bombings.
Ghailani is scheduled to be sentenced on Jan. 25, 2011, at 11:00 a.m. EST.

Mr. Bharara praised the FBI and the National Security Division of the U.S. Department of Justice for their extraordinary work in the investigation of this case. He also thanked the Tanzanian Police for their assistance in the case.

This case is being handled by the Office's Terrorism and International Narcotics Unit with assistance from the Justice Department’s National Security Division. Assistant U.S. Attorneys Michael Farbiarz, Harry A. Chernoff, Nicholas Lewin and Sean S. Buckley are in charge of the prosecution

This content has been reproduced from its original source.
 
Ule uzito wa ule mlipuko sitaweza kuusahau mpaka nakufa.!!!!!!!! Wakazi wa Magomeni watakuwa mashahidi kwenye hili!!!!!!!! Utafikiri lililipuliwa Magomeni!!!!!!!!!!!!!!! Kile kishindo hatari!!!!!!!!!!!!!

What next ndiyo tukajua CIA na FBI ni nani!!!!!!!! Ilala plus Magomeni ule mchakamchaka wake kama movie vile!!!!!!!!!!!!!
 
Ule uzito wa ule mlipuko sitaweza kuusahau mpaka nakufa.!!!!!!!! Wakazi wa Magomeni watakuwa mashahidi kwenye hili!!!!!!!! Utafikiri lililipuliwa Magomeni!!!!!!!!!!!!!!! Kile kishindo hatari!!!!!!!!!!!!!

What next ndiyo tukajua CIA na FBI ni nani!!!!!!!! Ilala plus Magomeni ule mchakamchaka wake kama movie vile!!!!!!!!!!!!!
Kazi iliyotukuka ya mchaga mmoja Thomas Lyimo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom