Fastjet yaanza safari Afrika Kusini

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Fastjet yaanza safari Afrika Kusini





SHIRIKA la ndege la Fastjet limeanza kurusha ndege yake kwa safari za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kuelekea Afrika Kusini.
Ndege ya kwanza ya shirika hilo iliruka Ijumaa iliyopita saa 3:15 asubuhi na kutua uwanja wa ndege wa kimataifa wa O.R Tambo wa Afrika Kusini saa 5:45 asubuhi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Fastjet, Ed Winter, alisema kuanza kwa safari hiyo kutatoa nafuu kwa abiria wanaohitaji kutumia usafiri wa anga.
“Kuanza kwa safari hii ni hatua nyingine katika sekta ya anga nchini. Sasa wateja watakuwa na chaguo zaidi katika usafiri wa anga,” alisema.
Alisema safari kutoka Dar es Salaam kwenda Afrika Kusini zitafanyika mara tatu kwa wiki; Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na kwamba idadi ya safari itaongezeka kutokana na mahitaji.
“Ndege zote kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea Afrika Kusini zitaondoka saa 3:15 asubuhi na kutua uwanja wa ndege wa Afrika Kusini saa 5:45 asubuhi. Pia ndege kutoka Afrika Kusini zitakuwa zikitoka saa 6:45 mchana na kutua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 11:10 jioni,” alisema.
Alisema tiketi za usafiri kati ya Dar es Salaam na Afrika Kusini ni sh 160,000 kabla ya kuwekwa gharama za uwanja wa ndege na kodi za serikali ambazo zinakadiriwa kuwa sh 77,000 kutoka Dar es Salaam au sh 84,760 kutoka Afrika Kusini.
“Kwa miaka mingi, usafiri kati ya Dar es Salaam na Afrika Kusini ulikuwa ukitolewa na kampuni moja, na kukosekana kwa ushindani kumefanya gharama za nauli kuwa juu. Fastjet tutapunguza gharama za safari ili kuwezesha watu wengi kutumia usafiri huo,” alisema Winter.
Alisema ‘booking’ za safari zinaweza kufanywa kupitia tovuti Africa's Low Cost Airline - Fastjet, ofisi yoyote ya Fastjet au kupitia wakala wao na kwamba malipo yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu ama kupitia mtandao wa M-pesa na Tigo Pesa.

 
Wawe makini wasiingie kwenye ushirika wa kimkakati (Strategic Alliance) na makampuni dhalimu kama KQ wasijeishia kubaya kama Precision Air. Otherwise wako safi!!!!!!!
 
hivi nyie mnawasifu hawa fastjet wakati hii safari ya sauzi ndo imefanya ndege ishindwe kuja KIa mpaka saizi atujaondoka toka hapa na abiria ni wengi sana wamemchukua mpaka mfanya kazi wa fastjet wamempeleka police.
 
Back
Top Bottom