Fanya yafuatayo ili uweze kufanikiwa kwenye biashara ya bucha

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,482
40,495
  • Uanzishapo biashara ya bucha, hakikisha pia una kijiwe cha nyama choma.​
  • Hii itakusaidia nyama kutokubaki, na kufanya fedha yako kuwa kwenye mzunguko.​
  • Hakikisha pia una wateja wako angalau kumi wa kudumu, iwe mama ntilie au wachoma mishikaki n.k​
  • Malengo kwa siku, angalau uuze kilo 50 na hakuna haja ya kuchukua/kununua kilo nyingi kwa siku (unaweza kununua kila 70 kwa siku).​
  • Na faida kwa kila kilo ni shilingi 1000; kwa hiyo kama utafanikiwa kwa kila mwezi, utakuwa unapata milioni 1.5, ukitoa gharama za uendeshaji unaweza kubaki na faida yako ya laki 8.​
  • Ukiwa nazo tano, utakuwa unatengeneza milioni 4​
  • Aya ingia mzigoni.​
 
Wamekusikia,shukrani
Sawa mkuu, changamoto niliyoiona kwa wenye mabucha wengi, wao sio sehemu ya walaji wa bidhaa yao; hii inapelekea nyama kubaki na kuona hiyo biashara hailipi.
Hii biashara inalipa na wapo wanaochinja zaidi ya ng'ombe watano kwa siku; muhimu ni kuwa na mkakati thabiti ya walaji wako.​
 
Naheshimu mawazo yako mkuu.
Nadhani wenye akili na mtaji watayafanyia kazi na kuyaingiza katika utekelezaji.
Kuna siku nilikuwa maeneo ya Iringa; bucha ya kitimoto na kwa pembeni wanakukaangia kama utapenda, kwa kifupi wanunuzi walikuwa wakija wanakuta 'stock' imeisha.
Nilitamani kama ingekuwa makazi yangu huko, ningekusanya hizo chenji zao.​
 
Kuna siku nilikuwa maeneo ya Iringa; bucha ya kitimoto na kwa pembeni wanakukaangia kama utapenda, kwa kifupi wanunuzi walikuwa wakija wanakuta 'stock' imeisha.
Nilitamani kama ingekuwa makazi yangu huko, ningekusanya hizo chenji zao.​
Riziki hupatikana pale ilipoandikiwa.
Usikute ungeenda huko mambo yangekuwa holaaaa.
 
Back
Top Bottom