Fanya Kila Siku, Na Baada Ya Siku Thelathini, Utathmini Ilivyokuathiri

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Ninakupa angalizo mapema! Usiliamini hata neno moja katika haya ninayokuambia.

Ukichukua hatua yoyote utakayochukua, ni wewe umeamua hivyo.

Kwanza, ni nani anayeweza kukuambia cha kufanya? Wewe ni mtu mkubwa sana. Wewe ni BIG BOSS.

Kitendo cha KUPEWA ubongo wenye seli zaidi ya bilioni moja, zote hizo kwa ajili ya kukutumikia, si jambo jepesi. Unadhaminika sana.

Wewe na watumishi wako, yaani, seli zaidi ya bilioni moja za ubongo, mtaweza kufikia mwafaka juu ya hatua ya kuchukua.

Wewe na Serikali ya kichwa chako mkiamua kuchukua hatua yo yote ile, ni kwa sababu umeamua wewe.

Lakini nimelenga nini hasa? Ni jambo moja tu, MANENO!

Unaweza usiwe na kitu chochote, lakini kama unao ulimi unaofanya kazi, unaweza kupata vyote, ukiamua.

Maneno ni mtaji. Maneno ni pesa. Maneno ni silaha. Vyo vyote utumiavyo, itakupa matokeo.

Hata Sasa, unakula matunda ya kinywa chako. Yanaweza yakawa ni matamu amu machungu. Vyotevyote vile, ni matunda ya kinywa chako.

Ulivyo leo ni matokeo ya maneno yako ya "Jana", au ya watu wengine, hasa uliowaamini.

Maneno yako, na ya watu wengine, endapo utayaruhusu, yatakufikisha pazuri au pabaya.

Ulishawahi kusoma kitabu cha THE LAW OF SUCCESS? Kimeandikwa na Napoleon Hill.

Ni miaka mingi imepita tokea nisome hicho kitabu. Zaidi ya miaka kumi.

Kuonesha jinsi maneno yalivyo na nguvu, kuna mfano wa mtu mmoja aliyekufa kwa ushawishi wa maneno.

Wataalam wa Saikolojia, nafikiri nchini Ufaransa, waliomba kibali serikalini ya kufanya jaribio la kumwua mtu kwa maneno. Mlengwa alikuwa mfungwa aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Timu iliyokuwa imehusihwa katika hilo jaribio, ilimwendea mlengwa na kumfahamisha kuwa siku hiyo ndiyo hukumu yake inatekelezwa.

Walimziba macho kwa kumfunga kitambaa usoni, sikumbuki kama ni cheusi au chekundu, kisha wakamwongoza kuelekea "machinjioni", eneo la kunyongea wafungwa waliohukumiwa kifo.

Akiwa amelazwa kifudifudi, kichwa kikiwa kimeingizwa kwenye mtambo wa kuulia, waliugusisha shingoni mwake ubao na kisha kuchuruzisha maji ya uvugu vugu kunzia shingoni palipoguswa na ubao kushuka chini mgongoni.

Dakika saba baadaye, daktari alipompima, aliripoti, "DEAD!".

Maneno ya kifo yalimpelekea kubadilishwa jina, akaitwa MAREHEMU!

Maneno yalifanya kazi. Alikufa kikweli kweli!!!

Kulitokea nini? Akili yake ya ndani ilifahamu kuwa mtu aliyekatwa shingo kiasi cha kichwa na kiwiliwili kutenganishwa, hana uchaguzi mwingine isipokuwa kufa tu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo na hatimaye umauti ukachukua usukani, akafa.

Mtambo wa kunyongea ulikuwa na sehemu ya kuingiza kichwa, pembeni kukiwa na "swichi" ambayo ikibonyezwa, upanga hushuka kwa nguvu na kukata shingo kwa kuitenganisha kichwa na kiwiliwili. Ubao ulipogusihwa juu ya shingo yake, alijua tayari, kashakatwa shingo. Kwa sababu hiyo, akili yake ilitimiza wajibu wake, kuhakikisha kuwa anakuwa vile mtu aliyekatwa shingo anavyopaswa kuwa, marehemu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo. Na dakika saba baadaye, ikathibitika kuwa kafa kama alivyoamini.

Unajua unaweza kuilekeza akili yako kwa maneno yako? Akili yako inakuamini kuliko inavyomwamini mtu mwingine yeyote. Na inao uwezo mkubwa sana, ambao ukiutumia alau asilimia kumi ya uwezo huo, utaushangaza ulimwengu.

Inasemekana, neva zinazohusiana na sauti zimeunganishwa kwenye ubongo kwa namna ambavyo maneno ayaongeayo mtu yanaweza kuathiri seli zote za mwili wake.

Neno lolote analolitamka mtu huathiri utendaji kazi wa seli za mwili wake. Kwa mfano, mtu akisema "nimechoka", seli zitapokea maelekezo ya kupumzika badala ya kuwa na utayari wa kuendelea kufanya kazi.

Maneno yako yanafinyanga mtazamo wako, tabia yako, imani yako na maisha yako kwa ujumla. Asemacho mtu mwingine, kitakuathiri pale tu utakapokubalinana naye. Ni kama vile mfungwa alivyoamini maneno ya waliomdanganya akaishia kufa bila kukatwa shingo.

Kuepuka kuandika Uzi mrefu, acha niende moja kwa moja kwenye jambo nililolenga kukushauri kufanya:

1. Chagua kauli unayoitaka ifinyange maisha yako.
Tuchukulie wewe ni mlevi uliyekubuhu ingawa huupendi ulevi, kwamba unywaji wako si kwa sababu ya kupenda bali ni utumwa. Maana yake, unatamani kuiacha pombe ila umeshindwa.

Chagua kauli ambazo zitaielekeza akili yako kuumba tabia itakayoifisha hamu ya pombe. Kwa mfano, ukiwa unakunywa, unaweza kusema HII POMBE NI MBAYA SANA, Au, kila uionapo pombe, sema, "NINACHUKIA SANA POMBE". Au, tamka kwa sauti, "NIMEACHA KUNYWA POMBE", mara nyingi, hata zaidi ya mara elfu moja kwa siku. FANYA hivyo kila siku, hadi mtazamo wako ubadilike kabisa na kuanza kukubaliana na unachokisema. Fanya hivyo, hata kama bado unakunywa. Lengo si kushindana na tabia ya ulevi, bali kujijengea tabia nyingine isiyotaka pombe. Tabia itakayokuwa na nguvu itaifisha dhaifu.

2. Mfano mwingine, inaweza ikawa unataka kukuza kipato chako lakini hujui pa kuanzia. Unaweza kuielekeza akili yako ikusaidie kukupa mawazo ya kukusaidia kufanikiwa. Unaweza kujisemea, "MIMI NI MILIONEA", au "NINAINGIZA MILIONI MOJA KIKA WIKI", au, "BIASHARA YANGU INAKUWA KWA KASI", n.k.

Tamka hivyo kwa sauti, mara kwa mara, mara nyingi, kadiri iwezekanavyo.

3. Unaweza ukawa unataka kuboresha uhusiano wako na mwenzi wako wa ndoa. Labda, hisia zako kwake zimeshuka sana na kumwona kuwa ni wa kawaida sana, kinyume na matakwa yako.

Kama ni mwanaume, unaweza kujisemea mara kwa mara, "NAMPENDA SANA MKE WANGU. HATA NIKIWA KAZINI NAMWONA YEYE TU. NIKITOKA KAZINI NAWAHI NYUMBANI KUMWONA MKE WANGU KIPENZI. MKE WANGU NI MZURI SANA! NINAVUTIWA NA UNYENYEKEVU WA MKE WANGU. NINAVUTIWA NA UMBO LA MKE WANGU. MKE WANGU ANA SAUTI TAMU KUZIDI ASALI", n.k.

Unaweza kuyasema yote hayo, au kauli mojawapo kati ya hizo, au yo yote utakayojiundia, unayoamini itakusaidia kupata matokeo unayoyahitaji.

Kama ni mwanamke, unaweza kufanya linaloendana na hilo, kulingana na matokeo unayoyataka. Cha muhimu, ni kuhakikisha kuwa nia yako haisukumwi na ubinafsi.

Kauli kama hizo zitaathiri kufikiri kwako, na kuanza kuziona fursa ndani ya fikra zako, ambazo zinaweza kubadilisha kabisa maisha yako.

Maneno yatakuumbia picha itakayoratibu matendo yako, na hivyo kubadilisha utakavyohusiana na watu wengine na jinsi watu wengine watakavyohisiana na wewe.

Hiyo ni mifano tu, lakini unaweza ukaamua wewe mwenyewe namna sahihi kwako kulingana na shakuku uliyo nayo.

Unaweza ukaamua vyovyote utakavyoona sawa, ila ujue tu kuwa maneno yana nguvu.

Je! Utayatumia kwa manufaa yako binafsi na ya wale uwapendao? Au utaacha watu wengine wanaojua kutumia vinywa vyao kwa manufaa kukutawala kupitia maneno yao?

Maneno yana nguvu! Maneno yana thamani kubwa kuzidi fedha na dhahabu.

Kuna shuhuda za watu wengi waliotumia maneno yao kama mtaji, na kila kitu kikawa Historia. Uduni uliondoka baada ya "mtazamo" chanya kubisha hodi katika fikra zao.

Kuna ndoa nyingi zilizopona baada ya wahusika kukumbatia kauli sahihi juu ya ndoa zao.

Kuna waliofanikiwa kifedha na kisiasa.

Kuna wengi.

Nani anayefuatia kutoa ushuhuda jinsi alivyobadili maisha yake kupitia kinywa chake? Ni wewe?

Kazi ni kwako!

Chagua kauli uionayo inafaa kwako, na kisha uiseme kika siku. Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na cha kusema. Mtazamo wako haitakuwa kama ulivyokuwa. Kuna utakachokigundua, ama utakuwa umeshaanza kugundua.

Na kufikia hapo, hautahitaji tena kushauriwa kufanya hivyo. Bila kushawishiwa, utaongeza jitihada ili kujionea mwisho wake, ambao kwa hakika, utakuwa mzuri kwa kadiri ya maneno yako yalivyo mazuri.
 
Shukrani! Bandiko zuri sana, tunahitaji ujanja na namna ya kuzitrick hizi akili zetu ili tuyafikie na kuyavuka malengo.

Hata hili suala la ukodishaji wa bandari linaloendelea sasa, shida kubwa ni kuwa akili za wengi zimekubalishwa, tangu kitambo sana, kuwa Arabs si watu wema.
 
Ninakupa angalizo mapema! Usiliamini hata neno moja katika haya ninayokuambia.

Ukichukua hatua yoyote utakayochukua, ni wewe umeamua hivyo.

Kwanza, ni nani anayeweza kukuambia cha kufanya? Wewe ni mtu mkubwa sana. Wewe ni BIG BOSS.

Kitendo cha KUPEWA ubongo wenye seli zaidi ya bilioni moja, zote hizo kwa ajili ya kukutumikia, si jambo jepesi. Unadhaminika sana.

Wewe na watumishi wako, yaani, seli zaidi ya bilioni moja za ubongo, mtaweza kufikia mwafaka juu ya hatua ya kuchukua.

Wewe na Serikali ya kichwa chako mkiamua kuchukua hatua yo yote ile, ni kwa sababu umeamua wewe.

Lakini nimelenga nini hasa? Ni jambo moja tu, MANENO!

Unaweza usiwe na kitu chochote, lakini kama unao ulimi unaofanya kazi, unaweza kupata vyote, ukiamua.

Maneno ni mtaji. Maneno ni pesa. Maneno ni silaha. Vyo vyote utumiavyo, itakupa matokeo.

Hata Sasa, unakula matunda ya kinywa chako. Yanaweza yakawa ni matamu amu machungu. Vyotevyote vile, ni matunda ya kinywa chako.

Ulivyo leo ni matokeo ya maneno yako ya "Jana", au ya watu wengine, hasa uliowaamini.

Maneno yako, na ya watu wengine, endapo utayaruhusu, yatakufikisha pazuri au pabaya.

Ulishawahi kusoma kitabu cha THE LAW OF SUCCESS? Kimeandikwa na Napoleon Hill.

Ni miaka mingi imepita tokea nisome hicho kitabu. Zaidi ya miaka kumi.

Kuonesha jinsi maneno yalivyo na nguvu, kuna mfano wa mtu mmoja aliyekufa kwa ushawishi wa maneno.

Wataalam wa Saikolojia, nafikiri nchini Ufaransa, waliomba kibali serikalini ya kufanya jaribio la kumwua mtu kwa maneno. Mlengwa alikuwa mfungwa aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Timu iliyokuwa imehusihwa katika hilo jaribio, ilimwendea mlengwa na kumfahamisha kuwa siku hiyo ndiyo hukumu yake inatekelezwa.

Walimziba macho kwa kumfunga kitambaa usoni, sikumbuki kama ni cheusi au chekundu, kisha wakamwongoza kuelekea "machinjioni", eneo la kunyongea wafungwa waliohukumiwa kifo.

Akiwa amelazwa kifudifudi, kichwa kikiwa kimeingizwa kwenye mtambo wa kuulia, waliugusisha shingoni mwake ubao na kisha kuchuruzisha maji ya uvugu vugu kunzia shingoni palipoguswa na ubao kushuka chini mgongoni.

Dakika saba baadaye, daktari alipompima, aliripoti, "DEAD!".

Maneno ya kifo yalimpelekea kubadilishwa jina, akaitwa MAREHEMU!

Maneno yalifanya kazi. Alikufa kikweli kweli!!!

Kulitokea nini? Akili yake ya ndani ilifahamu kuwa mtu aliyekatwa shingo kiasi cha kichwa na kiwiliwili kutenganishwa, hana uchaguzi mwingine isipokuwa kufa tu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo na hatimaye umauti ukachukua usukani, akafa.

Mtambo wa kunyongea ulikuwa na sehemu ya kuingiza kichwa, pembeni kukiwa na "swichi" ambayo ikibonyezwa, upanga hushuka kwa nguvu na kukata shingo kwa kuitenganisha kichwa na kiwiliwili. Ubao ulipogusihwa juu ya shingo yake, alijua tayari, kashakatwa shingo. Kwa sababu hiyo, akili yake ilitimiza wajibu wake, kuhakikisha kuwa anakuwa vile mtu aliyekatwa shingo anavyopaswa kuwa, marehemu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo. Na dakika saba baadaye, ikathibitika kuwa kafa kama alivyoamini.

Unajua unaweza kuilekeza akili yako kwa maneno yako? Akili yako inakuamini kuliko inavyomwamini mtu mwingine yeyote. Na inao uwezo mkubwa sana, ambao ukiutumia alau asilimia kumi ya uwezo huo, utaushangaza ulimwengu.

Inasemekana, neva zinazohusiana na sauti zimeunganishwa kwenye ubongo kwa namna ambavyo maneno ayaongeayo mtu yanaweza kuathiri seli zote za mwili wake.

Neno lolote analolitamka mtu huathiri utendaji kazi wa seli za mwili wake. Kwa mfano, mtu akisema "nimechoka", seli zitapokea maelekezo ya kupumzika badala ya kuwa na utayari wa kuendelea kufanya kazi.

Maneno yako yanafinyanga mtazamo wako, tabia yako, imani yako na maisha yako kwa ujumla. Asemacho mtu mwingine, kitakuathiri pale tu utakapokubalinana naye. Ni kama vile mfungwa alivyoamini maneno ya waliomdanganya akaishia kufa bila kukatwa shingo.

Kuepuka kuandika Uzi mrefu, acha niende moja kwa moja kwenye jambo nililolenga kukushauri kufanya:

1. Chagua kauli unayoitaka ifinyange maisha yako.
Tuchukulie wewe ni mlevi uliyekubuhu ingawa huupendi ulevi, kwamba unywaji wako si kwa sababu ya kupenda bali ni utumwa. Maana yake, unatamani kuiacha pombe ila umeshindwa.

Chagua kauli ambazo zitaielekeza akili yako kuumba tabia itakayoifisha hamu ya pombe. Kwa mfano, ukiwa unakunywa, unaweza kusema HII POMBE NI MBAYA SANA, Au, kila uionapo pombe, sema, "NINACHUKIA SANA POMBE". Au, tamka kwa sauti, "NIMEACHA KUNYWA POMBE", mara nyingi, hata zaidi ya mara elfu moja kwa siku. FANYA hivyo kila siku, hadi mtazamo wako ubadilike kabisa na kuanza kukubaliana na unachokisema. Fanya hivyo, hata kama bado unakunywa. Lengo si kushindana na tabia ya ulevi, bali kujijengea tabia nyingine isiyotaka pombe. Tabia itakayokuwa na nguvu itaifisha dhaifu.

2. Mfano mwingine, inaweza ikawa unataka kukuza kipato chako lakini hujui pa kuanzia. Unaweza kuielekeza akili yako ikusaidie kukupa mawazo ya kukusaidia kufanikiwa. Unaweza kujisemea, "MIMI NI MILIONEA", au "NINAINGIZA MILIONI MOJA KIKA WIKI", au, "BIASHARA YANGU INAKUWA KWA KASI", n.k.

Tamka hivyo kwa sauti, mara kwa mara, mara nyingi, kadiri iwezekanavyo.

3. Unaweza ukawa unataka kuboresha uhusiano wako na mwenzi wako wa ndoa. Labda, hisia zako kwake zimeshuka sana na kumwona kuwa ni wa kawaida sana, kinyume na matakwa yako.

Kama ni mwanaume, unaweza kujisemea mara kwa mara, "NAMPENDA SANA MKE WANGU. HATA NIKIWA KAZINI NAMWONA YEYE TU. NIKITOKA KAZINI NAWAHI NYUMBANI KUMWONA MKE WANGU KIPENZI. MKE WANGU NI MZURI SANA SANA! NINAVUTIWA NA UNYENYEKEVU WA MKE WANGU. NINAVUTIWA NA UMBO LA MKE WANGU. MKE WANGU ANA SAUTI TAMU KUZIDI ASALI", n.k.

Unaweza kuyasema yote hayo, au kauli mojawapo kati ya hizo, au yo yote utakayojiundia, unayoamini itakusaidia kupata matokeo unayoyahitaji.

Kama ni mwanamke, unaweza kufanya linaloendana na hilo, kulingana na matokeo unayoyataka. Cha muhimu, ni kuhakikisha kuwa nia yako haisukumwi na ubinafsi.

Kauli kama hizo zitaathiri kufikiri kwako, na kuanza kuziona fursa ndani ya fikra zako, ambazo zinaweza kubadilisha kabisa maisha yako.

Maneno yatakuumbia picha itakayoratibu matendo yako, na hivyo kubadilisha utakavyohusiana na watu wengine na jinsi watu wengine watakavyohisiana na wewe.

Hiyo ni mifano tu, lakini unaweza ukaamua wewe mwenyewe namna sahihi kwako kulingana na shakuku uliyo nayo.

Unaweza ukaamua vyovyote utakavyoona sawa, ila ujue tu kuwa maneno yana nguvu.

Je! Utayatumia kwa manufaa yako binafsi na ya wale uwapendao? Au utaacha watu wengine wanaojua kutumia vinywa vyao kwa manufaa kukutawala kupitia maneno yao?

Maneno yana nguvu! Maneno yana thamani kubwa kuzidi fedha na dhahabu.

Kuna shuhuda za watu wengi waliotumia maneno yao kama mtaji, na kila kitu kikawa Historia. Uduni uliondoka baada ya "mtazamo" chanya kubisha hodi katika fikra zao.

Kuna ndoa nyingi zilizopona baada ya wahusika kukumbatia kauli sahihi juu ya ndoa zao.

Kuna waliofanikiwa kifedha na kisiasa.

Kuna wengi.

Nani anayefuatia kutoa ushuhuda jinsi alivyobadili maisha yake kupitia kinywa chake? Ni wewe?

Kazi ni kwako!

Chagua kauli uionayo inafaa kwako, na kisha uiseme kika siku. Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na cha kusema. Mtazamo wako haitakuwa kama ulivyokuwa. Kuna utakachokigundua, ama utakuwa umeshaanza kugundua.

Na kufikia hapo, hautahitaji tena kushauriwa kufanya hivyo. Bila kushawishiwa, utaongeza jitihada ili kujionea mwisho wake, ambao kwa hakika, utakuwa mzuri kwa kadiri ya maneno yako yalivyo mazuri.
Hili nalo tutalitazama

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kabisa kama mtu anaweza kutrick ubongo wake uamini kuwa mtu huyo yuko katika zoezi la kufanya mapenzi na mfano mwanamke au mwanaume ilihali mtu huyo huko na tango au sabuni ya revloni bafuni, basi unaweza hata kufanya makubwa mno, mimi nina ushuhuda nikiwa napanga niko chuo zamani nilikua nawaambia watu mimi nitajenga nyumba nzuri ghorofa, kila siku niko ghetoni lakini nasema nitajenga ghorofa na ikawa hivyo watu hata familia yangu ilikua inaniona kichaa tu leo naona ghorofa langu limesimama sioni ni jambo jipya bali lilikuwa tayari zamani ni suala la muda tu
 
Bila connection hata useme nini hakitokei.
Uko sahihi! Haiwezi kutokea kwako kwa sababu unaamini hivyo. Uko sahihi kabisa mkuu!!!

Hata maisha yako yalivyo ni kwa kadiri ya imani yako! Uko sahihi kabisa!

Hata neno connection usingeweza kulitumia kama "waliokufundisha" huo msamiati wasingefanikiwa kukuaminisha hivyo!

Iko hivi mkuu, kuamini kuwa itatokea na kuamini kuwa haitatokea, vyote ni sahihi. Inategemeana tu na upande uliouchagua.

Kwa hiyo no problem at all mkuu. Kwako ni kama unavyoamini na kamwe haiwezi kuwa tofauti na hivyo.

Nini ushauri wangu kwako? Endelea kuamini vivyo hivyo kwa sababu hiyo ndiyo njia mojawapo ya uhakika ya kukusaidia kuendelea kuwa kama ulivyo.
 
Whether you think you can, or you cannot, you are right!
 
mimi nina ushuhuda nikiwa napanga niko chuo zamani nilikua nawaambia watu mimi nitajenga nyumba nzuri ghorofa, kila siku niko ghetoni lakini nasema nitajenga ghorofa na ikawa hivyo watu hata familia yangu ilikua inaniona kichaa tu leo naona ghorofa langu limesimama sioni ni jambo jipya bali lilikuwa tayari zamani ni suala la muda tu
Unanikumbusha mzee mmoja jijini Mwanza. Alipokuwa na umri wa kama miaka kumi na tano, aliandika malengo ya maisha yake na akawa anayaelezea kwa ndugu zake. Moja ya ndoto zake zilikuwa ni kuanzisha taasisi kubwa.

Alipoyafikia malengo yake, ndugu zake wa kuzaliwa, walifichua siriekuwa hawakuwa wakiamini kuwa hayo yangewezekana.

Kila alichokiandika kilitimia.
 
Ninakupa angalizo mapema! Usiliamini hata neno moja katika haya ninayokuambia.

Ukichukua hatua yoyote utakayochukua, ni wewe umeamua hivyo.

Kwanza, ni nani anayeweza kukuambia cha kufanya? Wewe ni mtu mkubwa sana. Wewe ni BIG BOSS.

Kitendo cha KUPEWA ubongo wenye seli zaidi ya bilioni moja, zote hizo kwa ajili ya kukutumikia, si jambo jepesi. Unadhaminika sana.

Wewe na watumishi wako, yaani, seli zaidi ya bilioni moja za ubongo, mtaweza kufikia mwafaka juu ya hatua ya kuchukua.

Wewe na Serikali ya kichwa chako mkiamua kuchukua hatua yo yote ile, ni kwa sababu umeamua wewe.

Lakini nimelenga nini hasa? Ni jambo moja tu, MANENO!

Unaweza usiwe na kitu chochote, lakini kama unao ulimi unaofanya kazi, unaweza kupata vyote, ukiamua.

Maneno ni mtaji. Maneno ni pesa. Maneno ni silaha. Vyo vyote utumiavyo, itakupa matokeo.

Hata Sasa, unakula matunda ya kinywa chako. Yanaweza yakawa ni matamu amu machungu. Vyotevyote vile, ni matunda ya kinywa chako.

Ulivyo leo ni matokeo ya maneno yako ya "Jana", au ya watu wengine, hasa uliowaamini.

Maneno yako, na ya watu wengine, endapo utayaruhusu, yatakufikisha pazuri au pabaya.

Ulishawahi kusoma kitabu cha THE LAW OF SUCCESS? Kimeandikwa na Napoleon Hill.

Ni miaka mingi imepita tokea nisome hicho kitabu. Zaidi ya miaka kumi.

Kuonesha jinsi maneno yalivyo na nguvu, kuna mfano wa mtu mmoja aliyekufa kwa ushawishi wa maneno.

Wataalam wa Saikolojia, nafikiri nchini Ufaransa, waliomba kibali serikalini ya kufanya jaribio la kumwua mtu kwa maneno. Mlengwa alikuwa mfungwa aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Timu iliyokuwa imehusihwa katika hilo jaribio, ilimwendea mlengwa na kumfahamisha kuwa siku hiyo ndiyo hukumu yake inatekelezwa.

Walimziba macho kwa kumfunga kitambaa usoni, sikumbuki kama ni cheusi au chekundu, kisha wakamwongoza kuelekea "machinjioni", eneo la kunyongea wafungwa waliohukumiwa kifo.

Akiwa amelazwa kifudifudi, kichwa kikiwa kimeingizwa kwenye mtambo wa kuulia, waliugusisha shingoni mwake ubao na kisha kuchuruzisha maji ya uvugu vugu kunzia shingoni palipoguswa na ubao kushuka chini mgongoni.

Dakika saba baadaye, daktari alipompima, aliripoti, "DEAD!".

Maneno ya kifo yalimpelekea kubadilishwa jina, akaitwa MAREHEMU!

Maneno yalifanya kazi. Alikufa kikweli kweli!!!

Kulitokea nini? Akili yake ya ndani ilifahamu kuwa mtu aliyekatwa shingo kiasi cha kichwa na kiwiliwili kutenganishwa, hana uchaguzi mwingine isipokuwa kufa tu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo na hatimaye umauti ukachukua usukani, akafa.

Mtambo wa kunyongea ulikuwa na sehemu ya kuingiza kichwa, pembeni kukiwa na "swichi" ambayo ikibonyezwa, upanga hushuka kwa nguvu na kukata shingo kwa kuitenganisha kichwa na kiwiliwili. Ubao ulipogusihwa juu ya shingo yake, alijua tayari, kashakatwa shingo. Kwa sababu hiyo, akili yake ilitimiza wajibu wake, kuhakikisha kuwa anakuwa vile mtu aliyekatwa shingo anavyopaswa kuwa, marehemu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo. Na dakika saba baadaye, ikathibitika kuwa kafa kama alivyoamini.

Unajua unaweza kuilekeza akili yako kwa maneno yako? Akili yako inakuamini kuliko inavyomwamini mtu mwingine yeyote. Na inao uwezo mkubwa sana, ambao ukiutumia alau asilimia kumi ya uwezo huo, utaushangaza ulimwengu.

Inasemekana, neva zinazohusiana na sauti zimeunganishwa kwenye ubongo kwa namna ambavyo maneno ayaongeayo mtu yanaweza kuathiri seli zote za mwili wake.

Neno lolote analolitamka mtu huathiri utendaji kazi wa seli za mwili wake. Kwa mfano, mtu akisema "nimechoka", seli zitapokea maelekezo ya kupumzika badala ya kuwa na utayari wa kuendelea kufanya kazi.

Maneno yako yanafinyanga mtazamo wako, tabia yako, imani yako na maisha yako kwa ujumla. Asemacho mtu mwingine, kitakuathiri pale tu utakapokubalinana naye. Ni kama vile mfungwa alivyoamini maneno ya waliomdanganya akaishia kufa bila kukatwa shingo.

Kuepuka kuandika Uzi mrefu, acha niende moja kwa moja kwenye jambo nililolenga kukushauri kufanya:

1. Chagua kauli unayoitaka ifinyange maisha yako.
Tuchukulie wewe ni mlevi uliyekubuhu ingawa huupendi ulevi, kwamba unywaji wako si kwa sababu ya kupenda bali ni utumwa. Maana yake, unatamani kuiacha pombe ila umeshindwa.

Chagua kauli ambazo zitaielekeza akili yako kuumba tabia itakayoifisha hamu ya pombe. Kwa mfano, ukiwa unakunywa, unaweza kusema HII POMBE NI MBAYA SANA, Au, kila uionapo pombe, sema, "NINACHUKIA SANA POMBE". Au, tamka kwa sauti, "NIMEACHA KUNYWA POMBE", mara nyingi, hata zaidi ya mara elfu moja kwa siku. FANYA hivyo kila siku, hadi mtazamo wako ubadilike kabisa na kuanza kukubaliana na unachokisema. Fanya hivyo, hata kama bado unakunywa. Lengo si kushindana na tabia ya ulevi, bali kujijengea tabia nyingine isiyotaka pombe. Tabia itakayokuwa na nguvu itaifisha dhaifu.

2. Mfano mwingine, inaweza ikawa unataka kukuza kipato chako lakini hujui pa kuanzia. Unaweza kuielekeza akili yako ikusaidie kukupa mawazo ya kukusaidia kufanikiwa. Unaweza kujisemea, "MIMI NI MILIONEA", au "NINAINGIZA MILIONI MOJA KIKA WIKI", au, "BIASHARA YANGU INAKUWA KWA KASI", n.k.

Tamka hivyo kwa sauti, mara kwa mara, mara nyingi, kadiri iwezekanavyo.

3. Unaweza ukawa unataka kuboresha uhusiano wako na mwenzi wako wa ndoa. Labda, hisia zako kwake zimeshuka sana na kumwona kuwa ni wa kawaida sana, kinyume na matakwa yako.

Kama ni mwanaume, unaweza kujisemea mara kwa mara, "NAMPENDA SANA MKE WANGU. HATA NIKIWA KAZINI NAMWONA YEYE TU. NIKITOKA KAZINI NAWAHI NYUMBANI KUMWONA MKE WANGU KIPENZI. MKE WANGU NI MZURI SANA SANA! NINAVUTIWA NA UNYENYEKEVU WA MKE WANGU. NINAVUTIWA NA UMBO LA MKE WANGU. MKE WANGU ANA SAUTI TAMU KUZIDI ASALI", n.k.

Unaweza kuyasema yote hayo, au kauli mojawapo kati ya hizo, au yo yote utakayojiundia, unayoamini itakusaidia kupata matokeo unayoyahitaji.

Kama ni mwanamke, unaweza kufanya linaloendana na hilo, kulingana na matokeo unayoyataka. Cha muhimu, ni kuhakikisha kuwa nia yako haisukumwi na ubinafsi.

Kauli kama hizo zitaathiri kufikiri kwako, na kuanza kuziona fursa ndani ya fikra zako, ambazo zinaweza kubadilisha kabisa maisha yako.

Maneno yatakuumbia picha itakayoratibu matendo yako, na hivyo kubadilisha utakavyohusiana na watu wengine na jinsi watu wengine watakavyohisiana na wewe.

Hiyo ni mifano tu, lakini unaweza ukaamua wewe mwenyewe namna sahihi kwako kulingana na shakuku uliyo nayo.

Unaweza ukaamua vyovyote utakavyoona sawa, ila ujue tu kuwa maneno yana nguvu.

Je! Utayatumia kwa manufaa yako binafsi na ya wale uwapendao? Au utaacha watu wengine wanaojua kutumia vinywa vyao kwa manufaa kukutawala kupitia maneno yao?

Maneno yana nguvu! Maneno yana thamani kubwa kuzidi fedha na dhahabu.

Kuna shuhuda za watu wengi waliotumia maneno yao kama mtaji, na kila kitu kikawa Historia. Uduni uliondoka baada ya "mtazamo" chanya kubisha hodi katika fikra zao.

Kuna ndoa nyingi zilizopona baada ya wahusika kukumbatia kauli sahihi juu ya ndoa zao.

Kuna waliofanikiwa kifedha na kisiasa.

Kuna wengi.

Nani anayefuatia kutoa ushuhuda jinsi alivyobadili maisha yake kupitia kinywa chake? Ni wewe?

Kazi ni kwako!

Chagua kauli uionayo inafaa kwako, na kisha uiseme kika siku. Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na cha kusema. Mtazamo wako haitakuwa kama ulivyokuwa. Kuna utakachokigundua, ama utakuwa umeshaanza kugundua.

Na kufikia hapo, hautahitaji tena kushauriwa kufanya hivyo. Bila kushawishiwa, utaongeza jitihada ili kujionea mwisho wake, ambao kwa hakika, utakuwa mzuri kwa kadiri ya maneno yako yalivyo mazuri.
Sahihi kabisa
 
Uko sahihi! Haiwezi kutokea kwako kwa sababu unaamini hivyo. Uko sahihi kabisa mkuu!!!

Hata maisha yako yalivyo ni kwa kadiri ya imani yako! Uko sahihi kabisa!

Hata neno connection usingeweza kulitumia kama "waliokufundisha" huo msamiati wasingefanikiwa kukuaminisha hivyo!

Iko hivi mkuu, kuamini kuwa itatokea na kuamini kuwa haitatokea, vyote ni sahihi. Inategemeana tu na upande uliouchagua.

Kwa hiyo no problem at all mkuu. Kwako ni kama unavyoamini na kamwe haiwezi kuwa tofauti na hivyo.

Nini ushauri wangu kwako? Endelea kuamini vivyo hivyo kwa sababu hiyo ndiyo njia mojawapo ya uhakika ya kukusaidia kuendelea kuwa kama ulivyo.
In case you didn't know am deep down kwenye haya mambo sio mchezo. Nimesoma na kupractice vitabu vingi vya self-help, psychology and manifestation vyote vinasisitiza nguvu ya maneno namna unavyoweza tengeneza kile ukitakacho kwa neno.
Au basi
 
Ninakupa angalizo mapema! Usiliamini hata neno moja katika haya ninayokuambia.

Ukichukua hatua yoyote utakayochukua, ni wewe umeamua hivyo.

Kwanza, ni nani anayeweza kukuambia cha kufanya? Wewe ni mtu mkubwa sana. Wewe ni BIG BOSS.

Kitendo cha KUPEWA ubongo wenye seli zaidi ya bilioni moja, zote hizo kwa ajili ya kukutumikia, si jambo jepesi. Unadhaminika sana.

Wewe na watumishi wako, yaani, seli zaidi ya bilioni moja za ubongo, mtaweza kufikia mwafaka juu ya hatua ya kuchukua.

Wewe na Serikali ya kichwa chako mkiamua kuchukua hatua yo yote ile, ni kwa sababu umeamua wewe.

Lakini nimelenga nini hasa? Ni jambo moja tu, MANENO!

Unaweza usiwe na kitu chochote, lakini kama unao ulimi unaofanya kazi, unaweza kupata vyote, ukiamua.

Maneno ni mtaji. Maneno ni pesa. Maneno ni silaha. Vyo vyote utumiavyo, itakupa matokeo.

Hata Sasa, unakula matunda ya kinywa chako. Yanaweza yakawa ni matamu amu machungu. Vyotevyote vile, ni matunda ya kinywa chako.

Ulivyo leo ni matokeo ya maneno yako ya "Jana", au ya watu wengine, hasa uliowaamini.

Maneno yako, na ya watu wengine, endapo utayaruhusu, yatakufikisha pazuri au pabaya.

Ulishawahi kusoma kitabu cha THE LAW OF SUCCESS? Kimeandikwa na Napoleon Hill.

Ni miaka mingi imepita tokea nisome hicho kitabu. Zaidi ya miaka kumi.

Kuonesha jinsi maneno yalivyo na nguvu, kuna mfano wa mtu mmoja aliyekufa kwa ushawishi wa maneno.

Wataalam wa Saikolojia, nafikiri nchini Ufaransa, waliomba kibali serikalini ya kufanya jaribio la kumwua mtu kwa maneno. Mlengwa alikuwa mfungwa aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Timu iliyokuwa imehusihwa katika hilo jaribio, ilimwendea mlengwa na kumfahamisha kuwa siku hiyo ndiyo hukumu yake inatekelezwa.

Walimziba macho kwa kumfunga kitambaa usoni, sikumbuki kama ni cheusi au chekundu, kisha wakamwongoza kuelekea "machinjioni", eneo la kunyongea wafungwa waliohukumiwa kifo.

Akiwa amelazwa kifudifudi, kichwa kikiwa kimeingizwa kwenye mtambo wa kuulia, waliugusisha shingoni mwake ubao na kisha kuchuruzisha maji ya uvugu vugu kunzia shingoni palipoguswa na ubao kushuka chini mgongoni.

Dakika saba baadaye, daktari alipompima, aliripoti, "DEAD!".

Maneno ya kifo yalimpelekea kubadilishwa jina, akaitwa MAREHEMU!

Maneno yalifanya kazi. Alikufa kikweli kweli!!!

Kulitokea nini? Akili yake ya ndani ilifahamu kuwa mtu aliyekatwa shingo kiasi cha kichwa na kiwiliwili kutenganishwa, hana uchaguzi mwingine isipokuwa kufa tu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo na hatimaye umauti ukachukua usukani, akafa.

Mtambo wa kunyongea ulikuwa na sehemu ya kuingiza kichwa, pembeni kukiwa na "swichi" ambayo ikibonyezwa, upanga hushuka kwa nguvu na kukata shingo kwa kuitenganisha kichwa na kiwiliwili. Ubao ulipogusihwa juu ya shingo yake, alijua tayari, kashakatwa shingo. Kwa sababu hiyo, akili yake ilitimiza wajibu wake, kuhakikisha kuwa anakuwa vile mtu aliyekatwa shingo anavyopaswa kuwa, marehemu.

Haraka sana, akili yake iliyasimamisha mapigo ya moyo. Na dakika saba baadaye, ikathibitika kuwa kafa kama alivyoamini.

Unajua unaweza kuilekeza akili yako kwa maneno yako? Akili yako inakuamini kuliko inavyomwamini mtu mwingine yeyote. Na inao uwezo mkubwa sana, ambao ukiutumia alau asilimia kumi ya uwezo huo, utaushangaza ulimwengu.

Inasemekana, neva zinazohusiana na sauti zimeunganishwa kwenye ubongo kwa namna ambavyo maneno ayaongeayo mtu yanaweza kuathiri seli zote za mwili wake.

Neno lolote analolitamka mtu huathiri utendaji kazi wa seli za mwili wake. Kwa mfano, mtu akisema "nimechoka", seli zitapokea maelekezo ya kupumzika badala ya kuwa na utayari wa kuendelea kufanya kazi.

Maneno yako yanafinyanga mtazamo wako, tabia yako, imani yako na maisha yako kwa ujumla. Asemacho mtu mwingine, kitakuathiri pale tu utakapokubalinana naye. Ni kama vile mfungwa alivyoamini maneno ya waliomdanganya akaishia kufa bila kukatwa shingo.

Kuepuka kuandika Uzi mrefu, acha niende moja kwa moja kwenye jambo nililolenga kukushauri kufanya:

1. Chagua kauli unayoitaka ifinyange maisha yako.
Tuchukulie wewe ni mlevi uliyekubuhu ingawa huupendi ulevi, kwamba unywaji wako si kwa sababu ya kupenda bali ni utumwa. Maana yake, unatamani kuiacha pombe ila umeshindwa.

Chagua kauli ambazo zitaielekeza akili yako kuumba tabia itakayoifisha hamu ya pombe. Kwa mfano, ukiwa unakunywa, unaweza kusema HII POMBE NI MBAYA SANA, Au, kila uionapo pombe, sema, "NINACHUKIA SANA POMBE". Au, tamka kwa sauti, "NIMEACHA KUNYWA POMBE", mara nyingi, hata zaidi ya mara elfu moja kwa siku. FANYA hivyo kila siku, hadi mtazamo wako ubadilike kabisa na kuanza kukubaliana na unachokisema. Fanya hivyo, hata kama bado unakunywa. Lengo si kushindana na tabia ya ulevi, bali kujijengea tabia nyingine isiyotaka pombe. Tabia itakayokuwa na nguvu itaifisha dhaifu.

2. Mfano mwingine, inaweza ikawa unataka kukuza kipato chako lakini hujui pa kuanzia. Unaweza kuielekeza akili yako ikusaidie kukupa mawazo ya kukusaidia kufanikiwa. Unaweza kujisemea, "MIMI NI MILIONEA", au "NINAINGIZA MILIONI MOJA KIKA WIKI", au, "BIASHARA YANGU INAKUWA KWA KASI", n.k.

Tamka hivyo kwa sauti, mara kwa mara, mara nyingi, kadiri iwezekanavyo.

3. Unaweza ukawa unataka kuboresha uhusiano wako na mwenzi wako wa ndoa. Labda, hisia zako kwake zimeshuka sana na kumwona kuwa ni wa kawaida sana, kinyume na matakwa yako.

Kama ni mwanaume, unaweza kujisemea mara kwa mara, "NAMPENDA SANA MKE WANGU. HATA NIKIWA KAZINI NAMWONA YEYE TU. NIKITOKA KAZINI NAWAHI NYUMBANI KUMWONA MKE WANGU KIPENZI. MKE WANGU NI MZURI SANA SANA! NINAVUTIWA NA UNYENYEKEVU WA MKE WANGU. NINAVUTIWA NA UMBO LA MKE WANGU. MKE WANGU ANA SAUTI TAMU KUZIDI ASALI", n.k.

Unaweza kuyasema yote hayo, au kauli mojawapo kati ya hizo, au yo yote utakayojiundia, unayoamini itakusaidia kupata matokeo unayoyahitaji.

Kama ni mwanamke, unaweza kufanya linaloendana na hilo, kulingana na matokeo unayoyataka. Cha muhimu, ni kuhakikisha kuwa nia yako haisukumwi na ubinafsi.

Kauli kama hizo zitaathiri kufikiri kwako, na kuanza kuziona fursa ndani ya fikra zako, ambazo zinaweza kubadilisha kabisa maisha yako.

Maneno yatakuumbia picha itakayoratibu matendo yako, na hivyo kubadilisha utakavyohusiana na watu wengine na jinsi watu wengine watakavyohisiana na wewe.

Hiyo ni mifano tu, lakini unaweza ukaamua wewe mwenyewe namna sahihi kwako kulingana na shakuku uliyo nayo.

Unaweza ukaamua vyovyote utakavyoona sawa, ila ujue tu kuwa maneno yana nguvu.

Je! Utayatumia kwa manufaa yako binafsi na ya wale uwapendao? Au utaacha watu wengine wanaojua kutumia vinywa vyao kwa manufaa kukutawala kupitia maneno yao?

Maneno yana nguvu! Maneno yana thamani kubwa kuzidi fedha na dhahabu.

Kuna shuhuda za watu wengi waliotumia maneno yao kama mtaji, na kila kitu kikawa Historia. Uduni uliondoka baada ya "mtazamo" chanya kubisha hodi katika fikra zao.

Kuna ndoa nyingi zilizopona baada ya wahusika kukumbatia kauli sahihi juu ya ndoa zao.

Kuna waliofanikiwa kifedha na kisiasa.

Kuna wengi.

Nani anayefuatia kutoa ushuhuda jinsi alivyobadili maisha yake kupitia kinywa chake? Ni wewe?

Kazi ni kwako!

Chagua kauli uionayo inafaa kwako, na kisha uiseme kika siku. Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na cha kusema. Mtazamo wako haitakuwa kama ulivyokuwa. Kuna utakachokigundua, ama utakuwa umeshaanza kugundua.

Na kufikia hapo, hautahitaji tena kushauriwa kufanya hivyo. Bila kushawishiwa, utaongeza jitihada ili kujionea mwisho wake, ambao kwa hakika, utakuwa mzuri kwa kadiri ya maneno yako yalivyo mazuri.
Neno la kuponya🙏🙏
 
Motivational Speakee. Mkikutwa huwa mnajiua nyie. Ila hapa uta copy na kupaste maneno ya watu ku motivate wenzio. Pambana hatuhitaji motivational speaker. Tunahitaji Motivationa Doer.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom