Kitukizuri
Member
- Apr 25, 2011
- 21
- 1
Tulikua na kijana wa kazi kutoka iringa,tuliishinae kwa takribani miezi kumi na tatu lakini alikuja kudhihirisha tabia zake za ulevi kupita kiasi,kiasi cha kusahau majukumu yake.mwisho wa siku yeye mwenyewe akaamua kuondoka nakusema anaenda kwao.basi tukampa chake,tukaagana.lakini inasema hakurudi kwao akawa anarandaranda mitaani..sasa leo tumeletewa taarifa amegongwa na gari amefariki.yuko chumba kuhifadha maita.sasa huku hana ndugu.watu wote wanatuangalia sisi.sisi tufanyaje ukizingatia kwao hatuna mawasiliano nao.gharama za kusafirisha kubwa,kwao iringa ndanindani huko hatupajui.