Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage alipinga vikali ukabila na kusisitiza umoja katika taifa letu. Rais Samia Suluhu anaishi falsafa za Mwalimu Nyerere na kuzitekeleza kwa vitendo.

Leo ikiwa ni siku ya kuhitimisha mbio za mwenge wa uhuru uliowaka nchi nzima kumulika maendeleo tukumbushane kuusu falsafa ya mwalimu nyerere kuusu mwenge wa uhuru alisema;

"Sisi tumekwisha uwasha mwenge wa uhuru na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro umulike ndani na nje ya mipaka yetu ulete matumaini pale ambapo hakuna matumaini, ulete upendo pale ambapo pana chuki na heshima mahali palipo jaa zarau" Mwalimu Nyerere

Lakini pia Tujikumbushe falsafa nyingine aliyosema Baba wa taifa ambayo Rais Samia Suluhu anaitumia sana katika uongozi wake

"Kila mtu anataka Maendeleo, lakini si kila mtu anaelewa na kukubali mahitaji ya kimsingi ya maendeleo. Sharti kubwa ni kufanya kazi kwa Bidii." - Julius K Nyerere.
 
Back
Top Bottom