Fahamu jinsi ya kupika pilipili ya kukaanga

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
MAHITAJI
~ Maembe 3 mabichi
~ Nyanya 5 kubwa
~Tomato paste/ tomato ya mkebe kijiko 1&1/2 cha kula
~ Pilipili mbichi takriban 20
~ Vitunguu maji 2
~ Thomu konde 8
~ chumvi kiasi
~ Mafuta ya uto/ ya kupikia vijiko 3 vya kula

MATAYARISHO
~ Osha vizuri mahitaji yanayohitajika kuoshwa, uchambue maganda na ukate kate vipande vya kiasi.
Weka kwenye blender kila kitu isipokuwa tomato paste na chumvi kisha blend vizuri.
~ Bandika motoni sufuria uliotia mafuta
~ Mafuta yakishika moto, weka mchanganyiko ulioblend pamoja na tomato paste na chumvi ukoroge vizuri
~ Funika uache itokote Kwa moto mdogo mdogo Kwa takriban dakika ishirini
~ Funua uone kama ishakauka, kama bado ifunike tena uiache mpaka ikauke vizuri.
~ Pilipili ipo tayari. Andaa Kwa pilau, biriani, wali mweupe au chochote upendacho.

MAELEZO YA ZIADA
~ Hakikisha unachanganya maembe mabichi na yalioiva kidogo ili pilipili isiwe chachu/Kali sana
~ Kama maembe yako yote ni mabichi sana, basi utaongezea na sukari kidogo kama nusu kijiko cha kula.
~ Kama unataka pilipili yako ikae kwa muda mrefu bila kuharibika, weka mafuta mengi.
~ Unaweza ukaongeza achari ya maembe/ ya mbirimbi wakati wa kupika pilipili hii ili ilete ladha tofauti tofauti.

IMG-20190404-WA0007.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom