Uhuru wa imani ya dini 31.-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini. (2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi. (3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya Serikali. (4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini ya taratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii ya kidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii na wa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za nchi. (5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuru wa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki au kuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini. (6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyote itakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongoni mwa wananchi. (7) Neno dini kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwa kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Mamlaka ya Rais yanahitaji ufafanuzi zaidi kwenye RASIMU ya katiba; kuna justification gani kwa Rais kuteua wabunge wakati kuna wabunge wanaowakilisha wananchi?
Hii inawapa mwanya viongozi dhaifu kuteua vimada wao na kuwahonga vyeo at the expense of the country's development.
nijambo la busara sana kuona nchi inayojitawala yenyew3 kuwa na rasimu ya katiba mpya na ni vizuri sana coz tunataka katiba yetu we are tanzania ni hayo 2 cjui ninyi mnasemaje wadau wangu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.