EXCLUSIVE: Download Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya hapa na toa maoni

Mkuu,

Umesaidia sana maana wengine wangesubiri sana au wangesoma nusunusu kupitia post za watu
 
".....Serikali yake inasimamiwa
na Bunge lenye Wabunge waliochaguliwa na wanaowawakilisha wananchi....."Hii ipo kwenye utangulizi wa Rasimu ya Katiba. Ndani wanatoa mamlaka kwa Rais kuteuwa wabunge WATANO...Je hawa wanawakilisha wananchi au Rais?
 
Hii tume ya Walioba tayari ina maoni mengi sana kuhusu katiba zote tatu kwa kuwa wakati wa kukusanya maoni hawakuainisha kwamba kutakuwa na katiba tatu. Hivyo kuunda tume nyingine kwa ajiri ya katiba ya Tanzania
bara au Zanzibar hakutakuwa na tija sana ukilinganisha na gharama za kuendesha tume na hata muda wa kumaliza suala la katiba ili itumike 2015

Mimi ningeshauri kwamba tume hii iliyopo wapate muda waandae draft nyingine hizo na zijadiliwe sambamba na ya muungano katika mabaraza. Nafikiri pia kimsingi hizi katiba za Zanzibar na Tanzania bara ni muhimu zaidi kuliko hata hiyo ya muungano. Wananchi tukizielewa katiba hizi hata hiyo ya muungano itaeleweka kirahisi.
 
Nime-attach kwa mtindo wa PDF
 

Attachments

  • Rasimu%20_Final_%20(1)[1].pdf
    387.8 KB · Views: 199
Habari zenu wanajamii,

Naomba aliye na soft copy ya rasimu ya katiba mpya aitume hapa kwenye jukwaa ili nami niiipate niweze kuipitia kama wantanzania wengine .
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa msaada huo.Nimeingia kwenye website yao sijaipata.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom