EWURA yabariki mafuta yaliyokataliwa Rwanda, sasa kuuzwa nchini

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,209
SHEHENA ya mafuta iliyopelekwa nchini Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imekataliwa katika nchi hizo kwa kukosa ubora na kurudishwa Tanzania ambapo sasa yameanza kuuzwa, Mwananchi Jumapili limebaini.

Licha ya maelfu ya lita za mafuta hayo ya dizeli na petroli kukataliwa katika nchi hizo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Julai 31 mwaka huu ilitoa kibali cha kuruhusu mafuta hayo kuuzwa nchini ikieleza kuwa ilipima na kubaini yanafaa kutumika nchini.

Mafuta hayo yalinunuliwa na kampuni tano za mafuta nchini na kusafirishwa kwenda katika nchi hizo, lakini yalirudishwa baada ya kubainika kuwa hayafai.

Juni 4 mwaka huu, Kamishna wa Huduma kwa wateja wa Mamlaka ya Mapato ya Rwanda (RRA), Richard Tusabe, alimwandikia barua Naibu Kamishna wa Wateja na Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kumweleza kuwa Rwanda imeyarudisha mafuta hayo kwa kuwa hayana kiwango kinachokubalika nchini humo.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba 0654/RRA/CCS/FOD-PMU/12, imeeleza kuwa mafuta hayo yaliyopelekwa Rwanda na malori manne, baada ya kupimwa na kupakuliwa hatimaye yalionekana hayafai, hivyo iliamriwa yarejeshwe nchini.

Kutoka Rwanda malori hayo yalisindikizwa chini ya uangalizi wa RRA hadi katika mpaka wa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, ili hatua za kuyarudisha kwa kampuni zilizoagiza ifanywe na Tanzania.

Barua nyingine iliyoandikwa Mei 30 mwaka huu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango la Rwanda (RBS), Injinia Ntiyamira Patrice ilieleza kuwa, mafuta hayo hayana viwango na kwamba hata DRC pia waliyakataa, baada ya kuyapima na kubaini kuwa hayakuwa na ubora.

Hata hivyo, katika barua yake ya Julai 31, 2012, Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu alitoa idhini ya kuuzwa kwa lita 171,730 za petroli nchini kutoka Rwanda, ikiwa ni sehemu tu ya mafuta hayo yaliyorejeshwa nchini.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili kuhusu suala hilo jana, Masebu alisema mafuta yote yanayopita nchini kwenda nchi jirani hayapimwi na Ewura.

"Sheria za Afrika Mashariki ndiyo zinaeleza hivyo, kama yalikubalika huko yalikokwenda au yalikataliwa sisi haituhusu," alisema Masebu.

Alifafanua kwamba hakuna mafuta machafu yanayotumika nchini na kwamba, ili mafuta yaweze kuingia sokoni ni lazima yawe na ubora unaokubalika nchini.

Chanzo:
Mwananchi Jumapili
 
Kwa sentensi ya mwisho ya Masebu inamaanisha Tz ni kiwango duni. Wengine wakikataa sisi tunasema kwetu ni kiwango, lete! Hivi ni lini tutakua makini na nchi yetu na wananchi wake?
 
Kwa sentensi ya mwisho ya Masebu inamaanisha Tz ni kiwango duni. Wengine wakikataa sisi tunasema kwetu ni kiwango, lete! Hivi ni lini tutakua makini na nchi yetu na wananchi wake?
Tunao TBS kazi yao ni kupima mafuta na kutoa certificates,
wapo pia jamaa wa vipimo kama Intertek na SGS.
Ni UONGO kudai kua hawapimi TRANSIT FUEL, waliyapima na wakatoa vibali. Wanaona aibu kukubali maana kua walilipua upipimaji. Pia itasababisha watumiaji wa mafuta kutokuyaamini!!
 
Tanzania shamba la bibi,Tanzania Jalala! TBS,TFDA,EWURA wamelala usingizi mzito!

hizi mamlaka mkapa alizianzisha kwa malengo mazuri lakini kazi waliyoivamia ya kutafuta mianya ya rushwa na kuitumia kushibisha matumbo yao ndo imetufikisha hapa. Ukiongeza na uamuzi wa kile kichwa cha nazi ndo kabisaa tumeliwa. Hukawii kuona tfda wana ukaribu mkubwa na waingizaji wa vipodozi, madawa feki, mchele mbovu gmo kutoka nje. Bila kubadilika hatusongi mbele! Lazima kila mtu awe anafanyiwa evaluation kwa kazi aliyoifanya in field, siyo kwenye makaratasi na computer.
 
Tunao TBS kazi yao ni kupima mafuta na kutoa certificates,
wapo pia jamaa wa vipimo kama Intertek na SGS.
Ni UONGO kudai kua hawapimi TRANSIT FUEL, waliyapima na wakatoa vibali. Wanaona aibu kukubali maana kua walilipua upipimaji. Pia itasababisha watumiaji wa mafuta kutokuyaamini!!


something is better than nothing . acha yaje tu tutayatumia
 
Jamani ni petrol station gani inaaminika niwe naweka mafuta bajaji yangu full tank?
 
Back
Top Bottom