Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 1,008
- 3,528
Kamishina wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia uchumi Paolo Gentiloni amesema muungano huo umejiandaa vyema endapo Urusi itasimamisha kabisa
usambazaji wa gesi.
Gentiloni amesema hawaogopi uamuzi wa Putin, lakini wanaitaka Urusi kuheshimu mikataba, na kama hilo litashindikana wameajiandaa kwa hali yoyote.
Kampuni kubwa ya gesi ya Urusi ya Gazprom ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba bomba la Nord Stream 1 ambalo linaunganisha Ujerumani na Urusi, litasimama kabisa hadi pale tabaini yake itakapofanyiwa ukarabati.
Moscow ilichukua hatua hiyo baada ya kundi la nchi saba zilizopiga hatua kiviwanda G7 kukubali kuweka ukomo wa bei ya mafuta ya Urusi.
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alikubaliana na pendekezo la Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi kuweka ukomo wa bei ya gesi inayoagizwa kutoka Urusi kupitia bomba hilo.