Eti wanawake 'wametakiwa' kuunga mkono rasimu ya Katiba!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Hivi ni sahihi kusema 'wametakiwa'?! Au 'wameombwa'?! Halafu Sophia Simba na Celina Kombani ni akina nani 'kuwataka' badala ya 'kuwaomba' wanawake kupiga kura ya NDIO kupitishwa rasimu ya Katiba?!!

Halafu Celina anawaambia wanawake waache 'kubweteka', hivi ni kweli wanawake wamebweteka? Kule vijijini akina nani wako mstari wa mbele shambani? Mama ntilie mijini? Hivi yeye amefikaje hapo?!
kombani.jpg


Wanawake nchini wametakiwa kuunga mkono na kuipitisha katiba iliyo pendekezwa kwa asilimia mia moja kwani imezingatia maswala muhimu yanayo husu kuwatambua wanawake na hakizao.
Hayo yamesemwa na waziri wa ofsi ya rais utumishi CELINA KOMBANI wakati wa hafla ya muendelezo wa sherehe za wanawake ambapo amewawata wanawake kutobweteka na kuhakikisha wanaipigia kura za ndio katiba pendekezwa ili iweze kupitishwa .

Naye waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto SOPHIA SIMBA akizungumza katika hafla hiyo amewataka wanawake kujitokeza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake inayofanyika kitaifa mkoani morogoro ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
CHANZO: ITV
 
Wanawake kwa miaka mingi wamekuwa wakidai haki zao za msingi zikiwemo haki za kupata nafasi sawa za uongozi, afya ya uzazi Salama, umri wa mtoto na mambo mengi ambayo yameshughulikiwa katika KATIBA inayopendekezwa. Kuhusu wanawake kutobweteka ni kweli wasimame I mara kiuchumi kwani ukijimudu kiuchumi ni rahisi kupata confidence ya kugombea nafasi za siasa kiuchumi na kijamii ktk Uongozi na kutoa mawazo. Lugha ya kuacha kubweteka Si ngeni Wala kebehi kwa wanawake tumeizoea. Wanawake tuipigie kura ya ndiyo KATIBA, tukisoma, tukaielewa itakuwa POWa kwetu
 
Sasa tatizo hapo nini? Watakiwe au waombwe suala la msingi hapo ni kuipigia kura katiba Pendekezwa kikubwa hapo waisome waielewe na siku ya mwisho waipigie kura ya ndiyo, haya mengine hayana mashiko.
 
Back
Top Bottom