Eric ten hag ameshafeli pale Manchester United ni suala la mda tu.

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,098
12,473
Hari za wakati huu wapenzi na mashabiki wa mpira Tanzania na duniani kote kwa ujumla,

Leo ningependa nitoe maoni yangu kuhusiana na Manchester United kama ifuatavyo:–

Mpira wa sasa ni tofauti na zamani sasa hivi mpira ni biashara kama biashara nyingine ndio maana kuna kila kitengo ambacho kinatakiwa katika kukuza biashara au kampuni na katika mpira kuna vitu vingi ila nitaelezea kwenye vitu vitatu alivyofeli ERIC TEN GAG ambavyo ni muhimu kwa team yoyote ile ili iweze kufanikiwa ambavyo ni managerial level, coaching level,na self confidence and improvement level.

Katika managerial level:–

Eric ten hag ni kocha mkubwa sana lakini amekosea na anaendelea kukosea kila siku kuhusu kwenye kukaa na ku manage wachezaji kwa mfano kwenye sakata la Christian Ronaldo pale ndio niliamini Manchester United wameingia mkenge,
kwasababu alishindwa kulimaliza lile swala ndani ya team mwisho wake Ronaldo alipewa adhabu na hatimaye akaondoka na moja ya kauli yake kocha wa Manchester United alisema 'At least now I can sleep ' kocha mkubwa kama yule kusema hyo hadharani kwa mchezaji ambaye ana mafanikio na background nzuri ya soka kuliko yeye ni makosa makubwa sana.

Hakuishia hapo kwenye suala la Mason Greenwood napo akaboronga kwanza kama team na kocha wake ilimkataa asirudi kambini hatimaye Greenwood akatimkia hispania huko ajabu Anthony alikutwa na sakata kama hilo ila akamtetea na hatimaye amerejea tena kuitumikia team hyo. Kwenye sakata la David de gea aliulizwa kama ana mpango naye ila akasema NO na mchezaji alikuwa tayari mpaka kupunguza mshahara ili asalie ila aligoma na David de gea kutimka Manchester United kumtimua mchezaji kama yule mwenye profile kubwa ambaye alikuwa msaada mkubwa hata team ilipopitia kipindi kigumu kwenye mpira ni kosa kubwa sana.

Sasa hivi Eric ten hag ana mgogoro na winga wake jodan sancho baada ya kutoleana maneno kwenye media na mchezaji kugoma kuomba msamaha anayopitia mchezaji huyo kwenye mpira hakina afya kwa wachezaji waliosalia kwenye team kwani amepigwa marufuku kukanyaga viwanja vya mazoezi na chakula pia anapelekewa nje kwasababu haruhusiwi kwenye canteen ya team yake this is very unfair and unprofessional kwa club kama Manchester United kocha anamsema mchezaji hadharani it's not fair.

Kwenye mpira saikolojia ya mchezaji ni muhimu sana ndio maana unashauriwa kitu chochote ambacho kitaathiri confidence na saikolojia ya mchezaji kama kocha unatakiwa ujiepushe nacho kwa mfano kumfanyia substitution mchezaji dakika 5 au 15 tu za mchezo kwasababu anacheza vibaya kama kocha huruhusiwi kwasababu utaathiri confidence na saikolojia yake ambayo itakuwa ngumu kuirudisha tena kwa wakati hvyo inabidi uangalie alternative nyingine tofauti na hiyo.

Manchester United ilipofikia inahitaji manager na sio kocha Eric ten hag ni kocha tena ambaye hana experience ya kufundisha mastaa wakubwa mfano wa manager ni kama carlo Ancelotti, Jurgen klopp, na Mourinho ambaye aliweza kuishi na mario Balotelli licha utukutu wake. Kwasababu kocha yeye anaangalia matokeo na kiwango cha mchezaji mmoja mmoja wakati manager anaangalia matokeo na kiwango cha team ndio maana Guardiola hawezi kuishi na wachezaji watukutu na aliwatimua wachezaji walionza kujiona ma superstar kama leroy sane na juao cancelo kwasababu hawana managerial skills wao ni self improvement and performance and self discipline.

Manchester United ili ifanikiwe kwanza Eric ten hag anatakiwa atimuliwe halafu aletwe manager mwingine sio kocha watu kama Jurgen klopp, carlo Ancelotti, Didier deschamps wanaweza kuinusuru Manchester United wakipewa mahitaji yao wanayotaka na support kutoka kwa uongozi uliopo kwasababu Jose Mourinho mpaka sasa ndio kocha mwenye mafanikio Manchester United baada ya fergusson licha ya kutotimiziwa mahitaji yake aliweza kuishi na wachezaji watukutu na kupata matokeo bila wengine kujua hata inapotokea wanapotofautiana kwasababu ajax Amsterdam ni tofauti na Manchester United.

Eric ten hag out.
 
Back
Top Bottom