Enzi za chama kimoja

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,231
113,608
Hivi kwa nini enzi zile za chama kimoja tulikuwa tuna uchaguzi wa rais?

Uchaguzi wa nini wakati mgombea alikuwa mmoja tu? Huu ulikuwa ni ujinga wa hali ya juu sana. Yaani mijitu yote hiyo iliyokuwa kwenye chama na serikali haikuona ujingaa huu?

Nyambaaf kabisa. Ndiyo maana mpaka leo tupo kwenye hali tuliyonanyo kwa sababu ujinga wa hali ya juu ni janga la kitaifa.
 
Nyerere alitengeneza mfumo mbovu wa uchaguzi ndiyo maana hata baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa waTanzania wengi walishindwa kuuelwa vyema badala ya wapiga kura kutazama sera za vyama wakabaki kutazama sura za wagombea.
 
Enzi hizo nakumbuka tulikuwa tunapiga kula ya NDIYO au HAPANA akikosekana mgombea wanaweka kivuli
 
Sasa huko ni kumkejeli na kudhalilisha Baba wa taifa.
 
Halafu cha kuchekesha eti kulikuwa na muda wa kufanya kampeni.
 
Sasa huko ni kumkejeli na kudhalilisha Baba wa taifa.

Kwani yeye Mungu?!! Kama kuna m akosa tusiseme...hii ni kumgeuza muumba wako bana..

NN, ndo maana wakina Fundi-RIP, Mtei, Kambona-RIP na wengineo yaliwakuta yaliyowakuta...was so so stupid.
 
Katika yote ,kitu ambacho hatutamsamehe mwalimu ni kutuulia Tanganyika yetu na kututumbukiza kwenye janga kubwa la mgogoro
 
Mwacheni Nyerere apumzike, leo Bungeni Musa Zungu ameteuliwa kama mgombea pekee wa uenyekiti wa Bunge kuziba nafasi ya George Simbachawene, ujinga uleule hata mpaka leo Bungeni.

Ila cha kufurahisha Wananchi wenyewe wameanza kupembuwa pumba na mchele, hapa Nape Nnauye akihutubia Umati wa Wananchi Kilolo Iringa.

[h=6][/h]
 
Back
Top Bottom