Enzi ulipokuwa boarding

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.

Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako, unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.

Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote. Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.

Waligawana msosi wao wawili wakatosheka, baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.

Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!
 
Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa

nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo

wakanielewesha.. nilimind we acha tu.
 
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako,unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote.Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.Waligawana msosi wao wawili wakatosheka,baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!

Umenikumbusha issue kama hiyo ilitokea wakati niko sec., jamaa alivyokwenda kuchukua dishi la wali akatoka nalo mlango mwingine na kukimbilia bwenini ambako alishawapanga washikaji zake, tukabaki tumezubaa, huyu jamaa alikuwa Msukuma alikuwa amepanda na amejaza(miraba minne)ilibidi tuufyate, bahati nzuri wenzetu walituonea huruma wakatuchangia wali kidogokidogo
 
hahahaa siku moja ndani ya PUGU BOY ilikuwa siku ya nyama...njemba moja ikaja katika table ikateua table leader mdau wake waligawana nyamwa washenzi wale,hawakula ugali
 
Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa

nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo

wakanielewesha.. nilimind we acha tu.
ahahahaah!! Bora sisi seminarini hakukuwa na ubabe wa namna hii!
 
Duh, basi mi nakumbuka tukiwa Old Moshi sec...
kwanza ni bifu tulilokkua nalo na Moshi tech...yani kuna siku tulitembea mpaka huko Moshi tech..kuanzisha vita tu!
Ila nakumbuka zaidi nilipoingia form one nikaitwa na majamaa (na walikuwa wakurya.. kutokana na lafudhi zao-afu nikakumbuka stori nlizokua nasikia kuhusu wakurya ati wakija kusoma sekondari ni wababa kabisa na wao vita ni jambo la kawaida kwao)
basi wakaniita nje ya bweni pale Hanang...wakanipa kiatu kinachonuka uvundo..wakasema nipige simu nyumbani nimwambie baba pesa zimeisha...kwa hiyo nikajifanya ninaongea na baba yangu. Basi nikatunga stori nilipokata simu nikawaambia amesema, atanitumia baada ya muda. Hivyo wakajifanya wana huruma sana...wakanipa shilingi mia, wakasema dogo kajinunulie maandazi na soda ila kabla hujanunua uje na maziwa na mkate mkubwa...duh! nilitoka jasho....
ilibidi niingie bwenini nichukue pesa zangu nikawanunulie...!!!!
tangu siku hiyo...mimi na njia ya hanang siendi...
sanasana nilikua natembea na wale majamaa vipofu, ukiwa nao hawakusumbui...hicho ndo kilichonisave....GUD OL' DAYZ....Auld Lang Syne...
 
ahahahaah!! Bora sisi seminarini hakukuwa na ubabe wa namna hii!
we acha tu na hii iliwapata jamaa zangu:

walikuwa wa dodge (hawaendi) paredi wanajificha bwenini. halaf bweni lina milango miwili mwanzon na mwishoni.. mwalimu akija kuwakata wanatokea mlango wa pili wanatokomea vichakani akiondoka warudi na kuanza kujisifu na kutukana mwalimu husika....!!!

basi kuna siku mwalimu akawakurupusha then akaenda moja ya kitanda akashusha net akalala kwenye kitanda huku kajifunika shuka...!!! basi jamaa kama kawa wakaja na kuanza kujisifia; hatuwezi yule ***** hajui sisi ni balaa!! na maneno mengine mabaya!!
basi walipoingia tu wote akaibuka kutoka kitandani..!!!!!!! weeeee walikuwa wadogo kisha ticha akawanote wachache tu anaoajua baadae akawaita. adhabu waliyopata nadhan hawatasahau maisha ya shule
 
Kwa wale waliosoma tanga tech kwa kamanda TETI the headmaster,mi nilisoma advance pale nikiishi bweni la TWIGA.Nakumbuka zile siku za wali a.k.a punje a.k.a chakula cha binadamu tulikuwa tunajiandaa kama unakwenda vitani,unapiga raba,jeans na t-shirt then unajipanga kwa foleni.Mgawaji anapokugawia,huangalii sahani,unamuangalia usoni kwa jazba yaani shari tupu.
 
Umenikumbusha issue kama hiyo ilitokea wakati niko sec., jamaa alivyokwenda kuchukua dishi la wali akatoka nalo mlango mwingine na kukimbilia bwenini ambako alishawapanga washikaji zake, tukabaki tumezubaa, huyu jamaa alikuwa Msukuma alikuwa amepanda na amejaza(miraba minne)ilibidi tuufyate, bahati nzuri wenzetu walituonea huruma wakatuchangia wali kidogokidogo
dah issue kama hii tushafanyiwa na msukuma mmoja(maduhu jilili),tena ilikuwa siku ya sikukuu,jamaa ali sepa na pilau lote,mayai,matunda na nyama za vyuku zooote!
 
dah issue kama hii tushafanyiwa na msukuma mmoja(maduhu jilili),tena ilikuwa siku ya sikukuu,jamaa ali sepa na pilau lote,mayai,matunda na nyama za vyuku zooote!

ahahahahah....enzi hizo Tabora boyz..kulikuwa na chemba moja katika bweni la mkwawa inaitwa university..mle tulikuwa tunalala pipo kama kumi na moja hivi tukiwemo viongozi..mke wa headmasta jina la utan nyumelo alikuwa na tabia ya kuja kutuamsha asubuh na mapema mabwenini..siku hiyo kaja kakuta pipo zote zimelala naked chemban coz tulipanga tumkomoe...ahahah yule mama eti akasema wala hatishiki coz keshaona kubwa zaidi ya zetu..mwee..but atleast alipunguza kuja akawa anaishia bweni kuu...vituko vya mesini hasa siku za nyali aka ubwabwa we acha tu..
 
E bwana shule za bweni ni vituko kweli, Enzi hizo tukiwa f5, tulikuwa na tabia ya kudogde parade, siku moja mwl wa nidhamu akaamua kuwa anapitia kwenye mabweni, basi siku moja tukakutwa tumeamka asubuhi tunapiga stori na kunywa chai, basi ile ticha katokea tu watu tukajisalimisha wengine wakatoka nduki, ila kuna jamaa mmoja yeye akakimbilia kitandani wakati ticha akiwa anamuona na akamwita kwa jina Elia, Elia nimekuona mbona unakimbia, jamaa hakusikia akaenda moja kwa moja kwenye kitanda chake akalala na kujifunika shuka, then ticha ikabidi aanze kukagua vitanda, jamaa akamkuta na kumchomoa! Ila sema ticha hakuwa na noma sana alitupatia adhabu ya vipushapu then tukaenda parade.
 
Nakumbukuka niko sec Siha ,siku moja jioni kuna jamaa kutoka kigoma alienda kujisadia ,na alikuwa na Ada kwenye walet ghafla ikadondoka chooni,alikuwa form 6,akaanza kutindua choo kwa pembeni, akaingia na kuitoa ada ,bahati nzuri kulikuwa na vyoo vya kulenga set mbili.alinyoa nywele zote mpaka kwenye kope,he had a strange personality.
 
Me niliambiwa nenda bweni(jina kapuni) ukwamuulizie jamaa anaitwa Bunsen burner!!! LOH! Nilipofika hapo bwenini jamaa wanistukia kuwa

nimeingizwa mkenge nao wakanambia ametoka nimsubiri kama dakika sita hivi atarudi!! ndugu niliuza chai mpaka nikakoma, baadae ndo

wakanielewesha.. nilimind we acha tu.

duh pole kijana wangu.
 
Duh! nimekumbuka ilikuwa seminarini.

Niliteleza na sinia la makande yenye nyama kama mita kumi hivi nikateguka mkono ila kande lilibaki kama lilivyo bila kumwagika.

Ukiandikiwa barua toka kwa yeyote hutaki uletewe hadi isomwe bwaloni (dining hall) tena kwa sauti ya juu ili wote wasikie na kwa idadi ya barua ulizoandikiwa.

Teheteheteheteheeee,..... siku kukiwa na mashindano ya mpira kati yetu na shule nyingine (mchanganyiko), wasichana wa shule pinzani wanatushangilia sisi badala ya shule yao.

This was 1990s
 
KWA WALE WALIOSOMA IFUNDA NADHANI WANAKUMBUKA SIKU YA TAREHE 1 APRIL!!!!!! Nakumbuka mwaka 1996 ndiyo ilikuwa mwisho wa kugawa makabati kwa form. kabla wa mwaka huo tarehe hiyo form nyoya, njuka walikuwa wanapata tabu sana, maana ni siku ya bakora na kichapo kwa siku ya wajinga..

Lakini kingine ambacho sitasahau ni kuvusha msosi kutoka mess kwenda bwenini na kutengeneza kaangaji ya kufa mtu.... Kwa wale waliomaliza IFUNDA TECH, (IFUTESCO) BILA SHAKA MNAKUMBUKA JIMBO LETU LA SHULE kipindi kile likipigwa mwili mzima unasisimka,,,,,,,,
 
KWA WALE WALIOSOMA IFUNDA NADHANI WANAKUMBUKA SIKU YA TAREHE 1 APRIL!!!!!! Nakumbuka mwaka 1996 ndiyo ilikuwa mwisho wa kugawa makabati kwa form one. kabla wa mwaka huo tarehe hiyo form nyoya, njuka walikuwa wanapata tabu sana, maana ni siku ya bakora na kichapo kwa siku ya wajinga..

Lakini kingine ambacho sitasahau ni kuvusha msosi kutoka mess kwenda bwenini na kutengeneza kaangaji ya kufa mtu.... Kwa wale waliomaliza IFUNDA TECH, (IFUTESCO) BILA SHAKA MNAKUMBUKA JIMBO LETU LA SHULE kipindi kile likipigwa mwili mzima unasisimka,,,,,,,,vipi bus letu la shule aka kiyeuyeu bado lipo?, nalikumbuka maana nalikumbuka sana lilikuwa jiupe kama la kiwanda cha Kioo Dar es Salaam.
 
Nakumbuka Umbwe Sec siku ya kwanza kufika tu, walituita "njuka" jamaa mmoja alinifata nikiwa juu ya kitanda pale dom 4, akaniambia kuwa "oya dogo unanilipa hela yangu lini" nikamuambia ipi, akanijibu , si ya hizi ndala ulizovaa? au ni zako? kuanzia leo hizo ndala ni zangu na nimekuuzia tayari na unipe hela yangu haraka, kwanza nipe sabuni na taulo nikaoge (huku akinivua zile ndala mpya za Umoja - 1997) akazichukua na kutokomea nisikokujua, ila brother mmoja akaniambia kuwa usijali nitakuonesha anapolala utaenda kuzichukua, duh kaka mbona niliona shule chungu.....
 
Kwa wale waliosoma tanga tech kwa kamanda TETI the headmaster,mi nilisoma advance pale nikiishi bweni la TWIGA.Nakumbuka zile siku za wali a.k.a punje a.k.a chakula cha binadamu tulikuwa tunajiandaa kama unakwenda vitani,unapiga raba,jeans na t-shirt then unajipanga kwa foleni.Mgawaji anapokugawia,huangalii sahani,unamuangalia usoni kwa jazba yaani shari tupu.
ahahaha! habar yako bana....salaam zao kwa njeka kiongozi
 
ahahaha! habar yako bana....salaam zao kwa njeka kiongozi
Kwanjeka noma,kuna mother mmoja tulimkamata mwanae kwa wizi wa viatu,alipotonywa kuhusu mwanae kukamatwa na wanafunzi,alikuja mkuku na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine,wote tulitoka nduki tukamwacha yeye na mwanae.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom