Pelekaroho
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 1,599
- 368
Inanikumbusha stori moja nilipokuwa chuo cha .......... mwalimu wangu mmoja alisimulia darasani siku moja, kuwa kuna jamaa walimteka mtu mmoja kwa nia ya kwenda kumuua msituni, lakini walipofika huko kabla ya kumuua wakamwambia kama ana neno la mwisho la kusema na aseme kabla ya kumuua, jamaa akaangalia chini akawaona sisimizi wakiwa kwenye msafara wao kama kawaida.
Jamaa akasema munawona hawa sisimizi, jamaa wakaitikia ndiyo, akawaambia basi hawa sisimizi siku moja watasema kuwa muliniuuwa. Jamaa wakacheka saana!
Na hatimaye wakamuuwa mateka wao na kuondoka. Miaka ikapita mingi tu bila wale wauwaji kujulikana, lakini siku moja, mmojawapo wa wale wauwaji akiwa anakata zake kilevi bar, mara akaona msululu wa sisimizi, akawaangalia saana kisha akaanza kuongea mwenyewe, kwa sauti ya kilevi, yaani nyie ndo mtakuja kusema kwamba eti mimi na akina fulani (akiwataja wenzake) tulimuuwa fulani (akimtaja marehemu).
Basi kwa sababu watu walikuwa wanamsikia anapoongea na wale sisimizi basi alifikishwa kituo cha polisi na upelelezi ukaanzia kwake. Mwisho wa siku wauwaji walipatikana na haki ikatendeka. Ndicho kitakacho tokea kwa Dr. Ulimboka, hata kama itapita miaka mingapi, ukweli utajisimamia wenyewe, na siku moja haki itapatikana.