Elections 2010 Emmanuel Nchimbi amewadanganya wana Songea,kuhusu tatizo la umeme

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Tarehe 10.10.2010 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ndugu Emmanuel Nchimbi ambaye wakati huo alikuwa anagombea ubunge jimbo la Songea mjini aliwaahidi wananchi wa manispaa ya songea kuwa tattizo la umeme songea litakuwa limekwisha kabisa ifikapo Decemba 2010.Hili ni tamko alilolitoa mbele ya bosi wake Jk wakat wakiomba kura kwa wananchi.Kinyume na matarajio ya wengi tatizo la umeme limeendelea kuwa sugu na halina utatuzi tena.Umeme sasa ni wa mashaka na muda wote ni kukatika katika tu tena bila taarifa yoyote.Sijawahi kuon atangazo lolote linalohusu katizo la umeme katika manispaa ya songea.
Ahadi ambayo wengi waliokuwa wamevalia mavazi ya kijani walionekana kushangilia sana.Lakini Emmmanuel Nchimbi hayupo tena songea na wala hajui tatizo hili.Ujinga wa wananchi wengi ulikuwa ni kula pilau zake na kubeba kanga na skafu za ccm.Hakuna mbunge anayetumia pesa zake kuhonga wananchi kama huyu mteule wa kikwete.Ghiliba nyingi anazitumia kupata madaraka.
 
Sio peke yake karibu wote wa CCM,na hii ni kawada yao hata PM anadanganya sembuse yeye sentesi niliyoweka red hasa ndio neno.Tubadilike watanzania tunajiangamiza wenyewe kwa kuwapa watu madaraka ambao ni waongo.
 
Back
Top Bottom