Emanuel Giniki Gisamoda Ashika Nafasi ya kwanza Geneve Marathon (42K), Switzerland Leo.

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
314
288
Mwanariadha Emanuel Giniki Gisamoda ashika nafasi ya kwanza katika Mbio za Generali Geneve Marathon ( 2:10:39) huko Geneva Switzerland Jumapili 15 Mei 2022 katika kilomita 42, ambapo amewashinda wa Kenya na waethiopia.

Giniki ni Mwanariadha pekee anaefanya vizuri katika Riadha hapa nchini, hasa katika Mbio za Kilomita 21K mpaka Sasa hakuna wa kumkamata.

Katika mbio Hizi, amekimbia kilomita 42 yaani Full Marathon na kuibuka mshindi ambapo anatajia kukimbia Mbio za Jumuiya ya Madola (Uingereza) au Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Oregon,Marekani.
 
Ajiandae kuitwa bungeni wakamtie gundu, ataitwa kupongezwa na viongozi wakati utakuta hata visa alipata kwa shida sana na kusumbuliwa na kaenda huko bila support yoyote yaani hata bendera ya taifa hakupata lakini wanasiasa mapoyoyo watajitokeza sasa wasivo na akili.
 
🇹🇿TV za bongo siku nzima ziko busy na SOKA, SIMBA YANGA kila mtu anajifanya mchambuzi, wameua michezo mingine,

🇹🇿Hii soka haijawahi na haitawahi kuiletea sifa Tanzania kwa wimbo wa Taifa kupigwa katikati ya mataifa na bendera yetu inapandishwa

🇹🇿Sijajua ni kwa nini wanalazimisha hili dubwashika linaloitwa football wakati hatuna kipaji nalo. Wajanjawajanja na wasanii ndiko wslikojifichia

🇹🇿Hongera sana Mwanariadha ijapokuwa sikujui ila leo wimbo wa Taifa umepigwa na bendera yetu imepandishwa. Suhiri urudi ndio wakupelele bungeni kwenda kupiga selfie na hao washabiki wa soka ambao ni watungasheria
 
Sasa unawalaumu Vyombo vya habari au Mchezo wenyewe?.

Soka bado ni Mchezo Kinara na si kwa Tanzania pekee bali ni kwa sehemu kubwa ya Dunia kama sio yote...ni Nchi za Kiasia tu zilikuwa nyuma lakini sasa wanalazimika kuitafuta soka.
 
Utaona watakavombilia airport kumpokea viongozi wa serikali na chama wakati anaumia na kuomba msaada wako ziii.

Ila naona now caiptalizing ya Kenya na Ethiopia wajiangalie, juzi Mrundi kawaburuza 3000m
Tanzania ni waongo kila kitu yaani unapendwa ukiwa na kitu lkn sio kukuwekea mazingira mazuri uwe na mafanikio.
 
Mwamba anatuwakilisha vyema

Screenshot_20220515-224927_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom