Elimu ya ziada Inahitajika

georgemwaipungu

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
2,779
588
Anaandika kaka Emmanuel Kihaule

Nawaona vijana wenye uwezo ambao kwa bahati mbaya kwa kukosekana utaratibu wa kunoa vipaji vyao kupitia mifumo na taasisi zilizowekwa kwa makusudi katika awamu ya kwanza kusaidia mamlaka za uteuzi kuwatambua na kuwalea vyema, wameishia kufanya vituko katika uongozi.

Kukosekana hata kwa retreat kwao imekuwa balaa kubwa. Nakumbuka karibuni akiongea kwenye kipindi cha Dakika 46 cha ITV Waziri mwenye mamlaka juu ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa, Mh. Simbachawene alikiri kuwa viongozi vijana walikuwa hawana uzoefu wa kutosha lakini aliwasifia sana kwa kuwa waaminifu.

Sasa hawa wangenolewa na kuandaliwa vyema ni wazi wangekuwa wazuri sana. Sasa pale Magogoni tumepafanya Chuo kikuu cha biashara na hata pale leaders club wanauza supu za utumbo na ulimi hata kwa wapita njia! Sasa viongozi wanaandaliwa au kuangaliwa wapi?

Nimesoma makala ya Mzee Msekwa mahali akisema wakati akiwa mkuu wa chuo pale Udsm kila chuo kikifungwa aliitwa na Mwalimu Nyerere pale Ikulu ili kutoa taarifa ya maendeleo ya chuo lakini pia kutoa taarifa ya vijana wowote ambao walionekana wangeweza kuja kuisaidia nchi katika uongozi.

Hao ndio walikuwa baadae wanapelekwa pale Magogoni kwa ajili ya kunolewa kiitikadi na kimaadili kabla ya kuteuliwa. Sasa siku hizi sijui miujiza gani inafanyika na ndio maana dosari zinaonekana hapa na pale. Sijui lini tutaurudia huu mfumo...
 
Mkuu,umeandika jambo la msingi sana lakini ni nani wa kulifanya hilo? Si chama tawala wala wapinzani ambao wana grooming & molding programmes kwa vijana wao. Kujipendekeza,uongo,uzandiki,unafiki ndio vimekuwa vigezo vikuu vya kupewa nafasi kwenye vyama vyetu mpaka serikalini. Leo muulize mkuu wa mkoa ambaye ni so called kada akwambie Mhe. JPM anatumia itikadi gani na Taifa ni itikadi gani,hawajui. DED hajui hata ahadi zilizohaidiwa na Mh. Raisi kwenye eneo lake atawezaje kuleta maendeleo..
 
Back
Top Bottom