EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi

INSIDER MAN

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
1,755
16,046
Kiukweli nimeshangaa sana ni nini kimemtuma Majizzo kuomba msamaha kwenye public? Kuna jambo lolote baya kutoka kwa Hando? Maana yeye alisema binafsi hafurahishwi na serikali kukopa kopa kama raia wa nchi ana haki ya kuishauri serikali na kutoa dukuduku lake kama katiba inavyosema.

Kwani Hando kuna sehemu kadanganya? Si kweli tunakopa? Kama hakuna ubaya kukopa kwanini Majizzo anaomba msamaha? Kama taifa tuna safari ndefu sana.

IMG_8207.jpg
 
Majizo amfukuze kazi Hando, EFM ni kituo kizuri sana Cha Radio, tatizo Hando anaingia akiwa amelewa chakari halafu anaruhusiwa kuingia hewani, aweke vipimo vya kilevi mlangoni.

Na akianza kuweka kipimo hicho, akipita Hando, kitapiga alarm ambayo itafika mpaka Morogoro, na kipimo kinaweza kupiga shoti hapohapo na kuharibika
 
Majizo amfukuze kazi Hando, EFM ni kituo kizuri sana Cha Radio, tatizo Hando anaingia akiwa amelewa chakari halafu anaruhusiwa kuingia hewani, aweke vipimo vya kilevi mlangoni.

Na akianza kuweka kipimo hicho, akipita Hando, kitapiga alarm ambayo itafika mpaka Morogoro, na kipimo kinaweza kupiga shoti hapohapo na kuharibika
Kwamba hando mtu wa mionzi sana
 
Uongozi wa E-FM umetangaza kumchukulia hatua Gerald Hando kutokana na kauli yake aliyoitoa kupitia E-FM kuwa hapendi Serikali inavyokopakopa hovyo na kusababisha ugumu wa maisha.

Hili suala la Mikopo ya Serikali ni jana tu hapa tulijadili sana kwamba Bunge liitake Serikali ije na maelezo ya mikopo iliyochukua kama ina baraka za Bunge au laa ili wananchi wote pamoja tuwe na picha ya pamoja kuhusu mikopo.

Kwani kuna malalamiko makubwa yaliyo sasa ni kwamba mikopo mingi imechukuliwa nje ya Bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mujibu wa Sheria.

Gerald Hando leo amechukuliwa hatua kwa kuhoji kuhusu Mikopo, Ndugai aliondoka kwenye kiti ya Spika kwa sababu ya kuhoji mikopo, Luhaga Mpina alikatwa jina kugombea NEC kwa sababu alihoji mikopo bungeni.

20221231_181825.jpg
 
Nilimpenda Magufuli kwenye mambo mengi lakini kwenye hili la kupenda kusifiwa tu ameharibu Sana mfumo. Nchi imegeuka ya hovyo mtu akikosoa tu anaonekana adui,atasakamwa na kesi za uhujumu nchi atapewa.
Mama amerithi na kuiendeleza tabia mbovu na ya hovyo Sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom