Kwako Komredi Lowassa ,
Sina imani kama unanifahamu kwa sura ila nafahamu fika huwa unasoma maandiko yangu ukipata wasaa, kama si wewe basi wafuasi wako. Napenda kukumbusha kuwa one month ago niliandika article yenye kichwa cha habari "The Fact; Lowassa Is About To Unfold It" ambayo ukiisoma kwa makini utabaini kuwa nilitabiri kile ambacho ulikifanya jana pale Monduli mbele ya waandishi wa habari na Dunia nzima.
Binafsi sikubaliani na hoja yako ya kuwa CCM itapita salama katika huu mtikisiko wa sasa hivi unaotokana na uzushi kama ulivyoeleza, naomba soma maandishi ukutani kisha nijibu huo "USALAMA" unaosema utatoka wapi? mimi naona hapa kuna mantiki iliyopinda au hujaeleweka vizuri, endelea kunisoma nikudadavulie.....watu ni chama na chama ni watu, CCM ni wanaccm na wanaccm ni CCM, usalama wa Wanaccm ni usalama wa CCM yenyewe, sasa na imani kuwa hata wewe na chama chako hamko salama, unajua kwanini? MALUMBANO YASIYO NA TIJA YAMETAWALA NDANI YA CCM, je ikiwa umepoteza zaidi ya nusu saa kujibu kile kinachoitwa kuchafuliwa kwa jina lako badala ya kujadili wanavyuo watapata wapi mikopo? huo usalama unaousema UTATOKA WAPI? au UKO WAPI? TUONYESHE HUO USALAMA. Komredi Lowassa utake usitake kuna kitu "WATANZANIA " wanataka kusikia lakini hujakisema, sasa kwa maneno nataka uniruhusu, JE NITABIRI TENA?